Je, sheria inaruhusu kumuua mtuhumiwa wa ujambazi asiye na silaha anayewakimbia Polisi?

Je, sheria inaruhusu kumuua mtuhumiwa wa ujambazi asiye na silaha anayewakimbia Polisi?

Mkuu kisheria ni kwamba polisi anaweza kutumia deadly force anapoona maisha ya raia au yake yapo hatarini,sasa kama mtuhumiwa anakimbia away from crime scene polisi HARUHUSIWI KUTUMIA SILAHA YA MOTO bcs hasababishi raia ya yeyote kuwa hatarini.

Ni jukumu la polisi (ndio maana wamepewa nyenzo nyingi amkamate mtuhumiwa ) sio kumpiga risasi za mgongoni but elewa tumo ndani ya shithole country haya yanatokea na hakuna kitakachotokea unless umo ndani ya ile 2%ya wateule,nkuu wa usalama wa taifa,anapigwa risasi na kuuliwa akidhaniwa ni jambazi

Dada yetu Akwilina anapigwa risasi hakuna kinachofanyika(hata ballistic test haikufanywa) na maisha yanaendelea kama kawaida.tusubirie next generations zitakazo weza kurudisha jinsi ya kuishi kwa mujibu wa kisheria.

Kama uko serious kwa hiki ulichoandika weka kifungu cha sheria kinachoelekeza namna ambavyo polisi ata deal na mtuhumiwa anayekimbia au matumizi ya silaha kwa polisi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Adhabu ya kukimbia sio kifo Ila mazingira ya kukimbia yanaweza kupelekea kifo.

Sent using Jamii Forums mobile app
But is it necessary katika mazingira niliyotaja? mtu hana silaha na anakimbia away from you, why kill him? na kwanini walivyomtoa kituoni hawakumfunga pingu mikono kwa nyuma? mtu aliyefungwa pingu anaweza kukushinda mbio? balance ya kukimbia anatoa wapi? Hii ishu ina maajabu mengi sana, tutajua tu ukweli
 
Kwahiyo mtuhumiwa ameshageuka jambazi tena? Hivi maana ya mtuhumiwa ni nini? Na hata kama ni jambazi, adhabu ya kukimbia ni kifo? kwa hukumu ya mahakama ipi?

Raia mwema kwa kawaida huwa hawezi kukimbia akiamriwa na askari mwenye silaha. wengine hata haja ndogo huwatoka wanapoamrishwa hivyo.

Miaka mingi iliyopita nikiwa ninaendesha gari maeneo ya mwananyamala nilitoka kwenye starehe na nikamsindikiza rafiki yangu nyumbani kwake.

Kabla sijafika mbali nilisimamishwa na askari wa doria ambao walikuwa na Landrover 110. Nilisimama lakini mitutu ya bunduki kama 10 hivi ilikuwa imelengwa kwangu. Nilitoka mikono ikiwa juu [pombe zote ziliyayuka]. Wakanihoji kitemi kabisa nami niliwajibu kistaarabu wakaomba kadi ya gari pamoja na kitambulisho changu nikawapo. Baada ya ukaguzi huo waliniomba radhi na kuniruhusu kuondoka.

Baadaye nilikuja fahamishwa kuwa walikuwa wamemlia dago mtaalam mmoja wa ujambazi ambaye alikuwa na gari iliyofanana sana na yangu.[Siku ya pili nilipomhadithia rafiki yangu aliniambia kuwa jana yake baada ya kuachana nami risasi zilirindima eneo lilie kwani na kuna jambazi ambaye alikuwa anatafutwa, kwa siku nyingi aligoma kusimama na kujaribu kukimbia basi wakaamua kumwasha kwa risasi na alifia hapo hapo..
 
Raia mwema kwa kawaida huwa hawezi kukimbia akiamriwa na askari mwenye silaha. wengine hata haja ndogo huwatoka wanapoamrishwa hivyo.
Miaka mingi iliyopita nikiwa ninaendesha gari maeneo ya mwananyamala nilitoka kwenye starehe na nikamsindikiza rafiki yangu nyumbani kwake.
Kabla sijafika mbali nilisimamishwa na askari wa doria ambao walikuwa na Landrover 110. Nilisimama lakini mitutu ya bunduki kama 10 hivi ilikuwa imelengwa kwangu. Nilitoka mikono ikiwa juu [pombe zote ziliyayuka]. Wakanihoji kitemi kabisa nami niliwajibu kistaarabu wakaomba kadi ya gari pamoja na kitambulisho changu nikawapo. Baada ya ukaguzi huo waliniomba radhi na kuniruhusu kuondoka.
Baadaye nilikuja fahamishwa kuwa walikuwa wamemlia dago mtaalam mmoja wa ujambazi ambaye alikuwa na gari iliyofanana sana na yangu.[Siku ya pili nilipomhadithia rafiki yangu aliniambia kuwa jana yake baada ya kuachana nami risasi zilirindima eneo lilie kwani na kuna jambazi ambaye alikuwa anatafutwa, kwa siku nyingi aligoma kusimama na kujaribu kukimbia basi wakaamua kumwasha kwa risasi na alifia hapo hapo.].

Asee ulivyo simama ndo ilikuwa pona yako, mara nyingi watu wanakufa kufungwa bila hatia.
 
Yaani tuchukulie mtuhumiwa wa ujambazi amekamatwa na Polisi, halafu wakati anawapeleka mafichoni kwa wenzake akaanza kuwakimbia Polisi huku akiwa hana silaha yoyote na akipiga makelele, je kuna uhalali/ulazima wowote wa kumpiga risasi ya mgongoni na kumuua? Je, ndugu zake wanaweza kudai fidia au ni hatua gani za kisheria wanaweza kuchukua?

Nauliza tu.
Kwa nchi zenye utawala wa sheria haitakiwi kumpiga risasi mgongoni
ila kwa asshole nations inaruhusiwa japo sio kisheria
 
Kwa nchi zenye utawala wa sheria haitakiwi kumpiga risasi mgongoni
ila kwa asshole nations inaruhusiwa japo sio kisheria
Waambie hivyo wamarekani[ambapo wengi wenu mnasifia demokrasi yao] hivyo nao watakwambia 'you are a dead horse'
 
kisheria ndio wanaweza kudai ILA sio kwa nchi hii ya kwetu,wajibu wa kisheria haupo kabisa na mbaya zaidi kama haupo kwenye ile 2% ya wanaotawala nchi hii,kwa nchi za wenzetu zinazoheshimu sharia hili haliwezi fanyika maana suspect was running away kwa hiyo hakuwa threat kwa yeyote,polisi wangelazimika kuomba back up ili suspect aweze kukamatwa ,ila kama alikuwa anakimbia na silaha hapo may be deadly force ingeweza tumika maana kuna uwezekano suspect angeitumia kudhuru raia.kuishitaki serikali yetu wakati watawala ndio wanauteua majaji ni ngumu mno,ni rahisi kupata majozi ya kuku kuliko la kuishitaki serikali.
Sasa angekimbia si angeendelea kufanya uhalifu.
Inawezekana amekuwa msumbufu anakamatwa na kuachiwa wakaona story isiwe ndefu bora kumaliza mchezo

Hit direct to the Ntonku
 
Waambie wewe

Mimi sipo Marekani
nipo Mbezi kwa Msuguri
Umezungumzia nchi ambazo wewe unaziona zinatumia utawala wa sheria nami nikakueleza kistaarabu kuwa hata Marekani Ujerumani n.k jaribu kukimbia wakati umesimamishwa na askari mwenye silaha.
 
Ni kosa kubwa kumuuwa
Kama ni mtuhumiwa kwanini asifungwe pingu?
Hili wanalijua kabisa kuwa pingu ni moja ya zana walizopewa kuzitumia sasa iweje hazitumiwi? Au kama ile staili ya USA
Mtu mweusi anaulizwa kitambulisho akiingiza mkono mfukoni wanamuwasha risasi
Kesi: He was reaching for a gun

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Polisi hataki kutoka jasho kukimbizana na mwizi.. Ukikimbia unakula shaba tu wakati huo yee yupo juu ya difenda katuloa tu
 
Umezungumzia nchi ambazo wewe unaziona zinatumia utawala wa sheria nami nikakueleza kistaarabu kuwa hata Marekani Ujerumani n.k jaribu kukimbia wakati umesimamishwa na askari mwenye silaha.
Nitajaribu usiku huu hapa maeneo ya Magogoni
 
Back
Top Bottom