Je, Simba SC inaweza kujenga uwanja kwa njia ya kuchangishana?

Je, Simba SC inaweza kujenga uwanja kwa njia ya kuchangishana?

Bilioni 50 na uwanja utoshe kwa derby ua Simba na Yanga?? Haiwezekani.Iwanja wa Taifa umejengwa kwa Billioni 229 na kuna wakati hautoshi kwa idadi ya mashabiki,Bilioni 50 ni kitu gani??
Simba hajengi uwanja kwa lengo la kuutumia kwenye mechi ya watani, game ya watani inaweza kuendelea kuchezwa uwanja wa Mkapa mkuu, ata Yanga kama watajenga uwanja hawawezi kukurupuka kujenga uwanja wa watu elf 60, kujenga huo uwanja lazima uingie bank kukopa na hivi vilabu sio vya watu binafsi kama ilivo kwa Azam

Kujenga uwanja wa ukubwa wa Mkapa ni matumizi mabaya ya pesa maana ili kuujaza ule uwanja unahitaji matukio machache sana ambayo ni Simba day, dar Derby, game za kubwa za club bingwa, sa ukiangalia hizo mechi ni almost 15% tu ya mechi zote ambazo Simba anacheza
 
Uwanja wa Taifa wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 60,000 ulijengwa kwa gharama ya Tsh 128,912,000,000 (129 Billion) Kwa mchango wa 2B inabaki 127B.Je fedha hizi wanasimba wataweza kukamilisha? Nadhani kama Mmiliki wa club angeongeza dau kiasi cha kutosha na wanasimba wachangie kiasi chao ili azma hii iweze kùfanikiwa
Usiwaamini wanasiasa hizo polojo umaijua bilion mia ww
 
Simba hawezi kujenga uwanja wa kuingiza mashabiki 60000 kama cha Mkapa, wao wanasema angalau mashabiki 30000, lakini pia kuna sababu nyingi ambazo zinapelekea kutofautisha gharama za ujenzi, uwanja wa Mkapa umetumia USD 56ml na unaingiza watu 60000 ila ubora wake ni mdogo sana compared na viwanja ambavyo vimecost USD 40 tu huko uarabuni

So kuna viwanja vimetumia less than that na vinaingiza mashabiki wachache zaidi au wengi zaidi, kwhyo inategemea material, design na wajenzi wenyewe plus budget ya wahusika, wanaweza jenga kiwanja kama cha Azam ila tofauti ikaja kwenye capacity tu

Japokuwa kiuhalisia hiyo 2b aliyoahidi Mo bado ni kiasi kidogo Kweli ila inawezekana ni kwa sababu hakuna actual amount ambayo teyari imetolewa kwa kufanya tathmini, maana ata kama watasema wajenge uwanja wa cheapest kabisa gharama inaweza range kwenye 30-40b kwahiyo bado ni ndogo
Mnapigaje hesabu mpaka kufikia hizo hela yaani kuzungusha Uzio tu kuna kata helo yote hiyo au kuna mengine
 
Kiongozi nazungumzia ulichoasema hapo juu yakuwa uwanja wa mkapa kumaliza hizo pesa inawezekanaje?
Anyway, hizo 128b unaweza ukaziona ni hela nyingi Sana na of course ni pesa nyingi sana ila inategemea zimetumika kwenye issues gani, hizo pesa kwenye miradi mikubwa ya ujenzi ni pesa ndogo Sana mkuu, wakati wewe unaona USD 56 ni nyingi Sana kwa uwanja wa Mkapa hapo kwa mabida Wana kiwanja kimejengwa kwa USD 600 can you imagine?

kama unashangaa kuona 128b imetumika kwenye ujenzi wa kiwanja cha mpira napata tabu kuamini kama ushawahi kuona nyumba ya kuishi mtu imecost 2b? Inawezekana hujawahi kuona na ata ukiskia nyumba inauzwa 500ml itakuwa waga unashangaa Sana na kuona watu wanaibiwa

Najua utakuwa ushaskia mradi wa ujenzi wa reli kwa ajili ya treni ya umeme, unajua unacost shngapi mkuu? Tanzania imekopa zaidi ya 3 trillion ili kutekeleza huo mradi, kwahiyo Mkuu Kila pesa ni nyingi na Kila pesa ni ndogo inategemea tu inatumika katika nyanja gani na inatumiwa na mtu wa aina gani
 
Sawa mkuu kumbe tatizo lipo kwenye hawa wahusika wanaopewa hizo tenda[emoji120][emoji120][emoji120]
 
Mo ana ziangua ana miliki 49% ya hisa anatoa 2b labda katoa kama mwanachama then Mo interprises ije itoe kama shareholder
 
Tangu jana mwekezaji wa Simba alipopost kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii kuwa amesikia kilio cha mashabiki wa Simba cha kutaka klabu yao iwe na uwanja wake wa kuchezea mechi za nyumbani na kuahidi kuchangia bilioni 2 kumeibuka mijadala kwenye redio na mitandao ya kijamii,kama ilivyo kawaida yetu Waafrika weusi wengine wanaunga mkono, wengine wanapinga, wengine wanaona haiwezekani na wengine wanadhihaki.

Wachambuzi wengi wa redio niliowasikiliza tangu jana na leo wanasema hakuna uwanja uliojengwa kwa fedha za harambee lakini viwanja vya CCM kama Kirumba, Majimaji, Sokoine, Ali Hassan Mwinyi na vinginevyo vilijengwa kwa wananchi kuchangishwa fedha, wafanyakazi walikatwa fedha kutoka kwenye mishahara yao na wananchi wengine walichangia kwa njia nyingine. Majengo na ofisi za TANU na CCM wananchi walichangishwa, majengo ya makao makuu ya Simba na Yanga wanachama na wapenzi wa timu hizo walichangishana na kujenga majengo hayo.

Wachambuzi wetu wanadai Simba inatakiwa iende kwenye makampuni na kuingia ubia au kuuza jina la uwanja kama walivyofanya Arsenal kwa Emirates,hii njia inaweza ikawa ngumu kuliko kuchangishana, makampuni na mashirika mengi yamepitia kipindi kigumu cha mtikisiko wa uchumi uliosababishwa na Covid 19,pia kuna kampuni gani inayoweza kutoa bilioni 50,au 100 kwa ajili ya kujenga uwanja wa Simba, ligi kuu yenyewe kupata mdhamini wa bilioni 3 tu ni kazi kubwa,ukiona kampuni kama Vodacom inajitoa kudhamini ligi kuu ujue bado mpira wetu hauvutii wawekezaji...haulipi.

Pia uchumi wetu hausapoti uwekezaji wa aina hiyo,na ndiyo maana haya mambo ya makampuni kujenga viwanja unayaona Ulaya na Afrika Kusini tu,kwa sababu biashara zao ni kubwa na uchumi wao ni mkubwa.

Simba wanaweza kujenga uwanja kwa njia ya kuchangishana ila wanatakiwa kujua kujenga uwanja si kazi ndogo,wanachotakiwa kufanya ni kujenga kwa awamu huku wakiendelea kuutumia,Simba haiwezi kushindwa kujenga uwanja wa nyasi bandia,wenye taa huku watazamaji wakiwa wamekaa kwenye majukwaa ambayo hayana viti kama wanavyofanya KirumbMa Majimaji, Sokoine,Samora na vingine.Kitu cha muhimu uwanja ujengwe kwa kuruhusu marekebisho, upanuzi nk.

Kitu kingine kwenye kuchangishana wanaweza kukusanya fedha kwa kuweka viwango na motisha fulani kwa wachangiaji mfano wanaweza kusema anayechangia kuanzia 100,000 anapewa cheti kama kumbukumbu na shukrani hii itasaidia watu wengi wapate morali ya kuchangia,pia majina yao yaandikwe na yawekwe nje ya uwanja.Wale wanaotoa kuanzia milioni 10 ,wanapewa viti maalum vya kukaa uwanjani yaani VVIP,nk.

Faida za kumiliki uwanja ni
kupata fedha zaidi,niliwahi kusikia wanalipia milioni 20 kwa kila wanavyocheza mechi uwanja wa Mkapa,wakiwa na uwanja wao hizi fedha hawatalipa.
Wataweza kupata fedha kwa kukodisha majukwaa na mageti kwa ajili ya matangazo,mfano geti A linaweza kukodishwa kwa kampuni X na kuitwa Gate X,badala ya geti A.Jukwaa kuu wanaweza kulikodisha kwa kampuni ya Dcom na wakaliita jukwaa la Dcom nk.

Kwahiyo Simba wanaweza kujenga uwanja kwa njia ya kuchangishana na ninawatakia kila la heri,maneno ya wakosoaji yanatakiwa yawe mbolea ya kuanza kujenga uwanja.
Naona baby wake baada ya kutolewa nje ya uwanja kakasirika katoa 2bil na kuanzisha harambee za kutengeneza uwanja.

Na sasa hivi kila kitu utawasikia "GSM hao.......".
 
Mo ana ziangua ana miliki 49% ya hisa anatoa 2b labda katoa kama mwanachama then Mo interprises ije itoe kama shareholder
Jaman muwe mnafuatilia vitu kwa undani ndipo mharishe hapa.
Mo alisema kwa kuanzia natoa 2b, neno kwa kuanzia nyie mnalielewaje? Mbona alitumia kiswahili kilichonyooka kabisa wapi mnakwama nyie watu?
 
Jaman muwe mnafuatilia vitu kwa undani ndipo mharishe hapa.
Mo alisema kwa kuanzia natoa 2b, neno kwa kuanzia nyie mnalielewaje? Mbona alitumia kiswahili kilichonyooka kabisa wapi mnakwama nyie watu?
Nmeuliza anatoa kama muwekezaji au kama mwanachama?
 
Back
Top Bottom