ASIWAJU
JF-Expert Member
- Nov 18, 2022
- 1,938
- 1,632
Heri ya siku ya Uhuru Watanganyika wote.
Habari za saa wanachama wote natumai ni njema, moja kwa moja niende kwenye dhumuni la mada hii.
Mada hii inazungumzia Muafrika na akili , kama ambavyo kichwa cha mada kiulizavyo. Je, waafrika hatuna akili ?kweli au sikweli jibu langu kama mleta mada ni sikweli.
Sikweli kwamba waafrika hatuna akili, jambo ni kuwa waafrika tuna akili Ila sababu kuu ambayo inatufanya sisi waafrika tuonekana hatuna akili ni “Kukosa uhuru wa kuhoji mambo mbalimbali”.
Hari ya sisi waafrika kukosa uhuru wa kuhoji mambo mbali mbali inaathiri mpaka uwezo wetu wa kufikiri, uwezo wa kufikiri ukiisha athirika usitegemee jamii hiyo kuwaza vitu mbalimbali kitofauti kulingana na jamii inavyo vitafsiri.
Uwezo wa kuhoji wa waafrika waliowengi umeathiriwa na mambo yafuatayo:-
i, Elimu isiyo bora
ii, Dini/ kasumba ya dini
iii, Tamaduni mbalimbali
iv, Mifumo ya Kiutawala
Haya ni baadhi ya mambo makuu yanayo minya uhuru wa kuhoji wa mwafrika kitu ambacho hupelekea kuathiri uwezo wa kufikiri wa mwafrika na kupelekea kuonekana kama ni mtu asiye na akili.
Mpaka sasa waafrika hatujawa tayari kupambana na haya mambo yanayo minya uhuru wetu wa kuhoji kitu ambacho kina athiri uwezo wetu wa kufikiri kwa kiwango kikubwa.
Jamii yoyote inayo kosa uhuru wa kuhoji baadhi ya mambo ni ngumu kutambua baadhi ya mambo kwa kina na kwa ubora zaidi.
Waafrika tuta endelea kutambulika na jamii mbalimbali za duniani kama ni watu tulio kosa akili kama hatuta kubali kubadilika na kubadili misimamo yetu juu ya hayo mambo mbalimbali niliyo orodhesha yanayo minya uhuru wetu wa kuhoji.
Elimu tupatayo imeshindwa kumuweka mwafrika kuwa huru kuhoji mambo, tamaduni nazo zina minya uhuru wa kuhoji uhalali wa baadhi ya mambo, dini ndio kabisa zina tengeneza kizazi cha hofu kuliko kizazi cha kuwa huru kuhoji mambo, tawala nazo zina minya kwa kiwango kikubwa uhuru wa kuhoji.
Tuna safari ndefu sana kujenga kizazi bora cha mwafrika kama hatuta taka mabadiliko kwenye hayo mambo baadhi niliyo orodhesha ambayo ni kikwazo kwetu.
Karibuni kwa maoni yenu wadau.