Je, Tanzania ipo tayari kukabilian na vikwazo kutoka umoja wa Ulaya?

Je, Tanzania ipo tayari kukabilian na vikwazo kutoka umoja wa Ulaya?

Kesho wataanza kujadili vikwazo watakavyoiwekea Tanzania. BBC swahili.
Vikwazo huwekwa na nchi husika sio bunge la jumuiya wewe

Ni bunge la nchi husika wenye pesa zao
Acha na waswahili wenzio hao BBC swahili

Weupe vichwani kama wewe mwenyewe
 
Kwa muda mrefu hawa watu wanazuia mazao ya chakula yasiuzwe nje ili wananchi wasikose chakul. Hii ni sababu kuu inayowafanya wakulima wa Tanzania wawe masikini. Vikwazo vitaamsha kila mtu usingizini.
 
Kama M7 anapeta -- basi hakutakua na jipya
 
vikwazo huwa havigusi vigogo, vinasubisha walala hoi, eti ili wananchi wa-riot kuikataa serikali.
Mapanki (Kim Jong Un)amewekewa vikwazo vikali,, wananchi wa kawaida ndyo wanakula nyasi na matunda pori, KIM na vigogo wake wanakula bata
Kuli kwa Kim hata ukiwaza tu kuandamana kabla hujafungua mdomo kuhamasisha wenzako uko chini ya Kikosi kazi na unapata mkung’uto.

Basi na sisi tuwaambie Jumuia ya Ulaya hatuitaki Demokrasia.
 
Kwa jinsi hali ya hewa ya kisiasa ilivyo nchini ni wazi kuwa kuna vikwazo vinakuja huko mbele.

Je, Tanzania inaweza kukabiliana navyo?
EU wenyewe Hali zao si nzuri...! Wamelikoroga kwa Russia na kiasi kwa China Hata kwa US ni mguu ndani nguvu Nje ! Hata hivyo, na sisitiza masuala yetu kama nchi tuyamalize sisi wenyewe tuachane na utegemezi. Utegemezi ndiyo umeiua Libya!
 
Kwa muda mrefu hawa watu wanazuia mazao ya chakula yasiuzwe nje ili wananchi wasikose chakul. Hii ni sababu kuu inayowafanya wakulima wa Tanzania wawe masikini. Vikwazo vitaamsha kila mtu usingizini.
Huelewi mifumo ya vikwazo inavyofanya kazi huwa hawaweki kienyeji eti kisa Lisu su siasa

Wao huweka vikwazo wakinyimwa fursa na watawala wa kiafrika

Fursa wakipewa hawahangaiki
 
Kwa jinsi hali ya hewa ya kisiasa ilivyo nchini ni wazi kuwa kuna vikwazo vinakuja huko mbele.

Je, Tanzania inaweza kukabiliana navyo?

Wazungu hawawezi kuwekea vikwazo nchi inayowalisha au nchi waliyoipita sana kiuwezo...
 
Ulaya wanamjadili Trump
Ila wakiijadili Bongo basi ni kinafiki tu
Na wakiweka vikwazo watu wataishi tu kama Iran na nchi zingine

Na wa kijijini hataona mabadiliko yoyote
Vikwazo ndio vitawasha umeme wakiachia? Au maji yanapatikana sasa au madawa
 
Hilo ni bunge la ulaya, kwa umoja wao huo hawana nguvu kumbuka sio ulaya yote inatupatia mokopo, hapa kuna kina Norway, Denmak, Sweden, Uingereza (ambaye sio kivile sana kwenye umoja wao) hao wengine hawana msaada wowote kwetu

Sijui Serbia, Uhispania, Ureno nk
Na pia hii sio mara ya kwanza kutujadili tuko mark my word utarudi kunikumbusha kama kuna kitu kitatokea
Kawaulize Zimbabwe, Rais wao alikua anaenda China na Singapore, kwingine Hapana.
Na Nchi ni kama imevamiwa na Wachina kila kitu. Pity
 
Basi na sisi tuwaambie Jumuia ya Ulaya hatuitaki Demokrasia.
Kwani tulushawahi kuwaomba watupe demokrasia hao Jumuiya ya Ulaya?
Kila nchi ina mifumo yake ya utawala .Hakuna nchi duniani huandika barua kwa nchi nyingine au jumuiya nyingine kuwa tunaomba mfumo wenu wa demokrasia
 
Hilo ni bunge la ulaya, kwa umoja wao huo hawana nguvu kumbuka sio ulaya yote inatupatia mokopo, hapa kuna kina Norway, Denmak, Sweden, Uingereza (ambaye sio kivile sana kwenye umoja wao) hao wengine hawana msaada wowote kwetu

Sijui Serbia, Uhispania, Ureno nk
Na pia hii sio mara ya kwanza kutujadili tuko mark my word utarudi kunikumbusha kama kuna kitu kitatokea
Kwa taarifa yako EU ni donor namba 2 kwa kuchangia budget yetu baada ya US kisha inafuata World Bank kama namba 3.
Hivyo adhabu yeyote ya EU itakuwa na athari kubwa.
Ila viongozi wa ccm kwa ubinafsi wao wanaweza wasijali maana wao hawaumii. Labda tuombe Mungu wabunge wa EU waligundue hilo kisha waamue kuwawekea vizuizi binafsi viongozi
 
Huelewi mifumo ya vikwazo inavyofanya kazi huwa hawaweki kienyeji eti kisa Lisu su siasa

Wao huweka vikwazo wakinyimwa fursa na watawala wa kiafrika

Fursa wakipewa hawahangaiki
Stay there, wenzako wanaangalia uvujwaji wa haki za binadamu. Lissu anawakaza sana macho eeh.
 
Back
Top Bottom