Nchi ambazo ziko tayari kutoa misaada kwa Africa bila masharti ziko tatu sasa hivi Russia,China na UAE
Wazungu wanazidi kupoteza ushawishi Africa.Hizo nchi tatu zina kasi ya ajabu kuishika Africa
Hujui unachoongea:
Weka hapa takwimu, Russia, China na UAE, zote kwa pamoja zimeisaidia au kuikopesha Tanzania kiasi gani katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, linganisha na kiasi ambacho Tanzania imepokea toka nchi za Ulaya.
Watu huwa mnaropoka tu. Urusi huwa haitoi msaada wowote wa kifedha isipokuwa nafasi tu za masomo. Urusi bado ina kundi kubwa la watu maskini, nao wanapambana kupunguza umaskini wa watu wao. Nchi za Uarabuni japo per capita income yao ni kubwa lakini GDP zao ni ndogo kiasi kwamba hawawezi kutoa msaada mkubwa kwa nchi nyingine kwani uchumi wao hauna sustainability kwa sababu ya kutegemea zaidi chanzo kimoja, mafuta.
Cbina bado ina kundi kubwa la watu wake wanaoishi kwenye umaskini. China haizisaidii nchi za Afrika bali inaenda kuvuna kwenye nchi za Afrika, sawa na hizo nchi za UAE.
Yafahamu yafuatayo:
Ulaya ndiyo uchumi mkubwa wa pili Duniani baada ya marekani. Ufahamu kuwa Ulaya yote kwa jumla ina watu milioni 744 tu, chini kuliko idadi ya wachina au wahindi, lakini ina pato kubwa kuliko China na India.
The European Union's total GDP is estimated to be $19.99 trillion (nominal) in 2025. It's the second largest economy in the world in nominal terms, after the United States.
Ukizungumzia masuala ya uchumi, utakuwa mjinga sana umaidhatau USA, Ulaya na China. Lakini mafungamano ya Ulaya na America yanaifanya China kutokuwa na uwezo wa kushindana na hizo blocks mbili, Ulaya na America.