Mheshimiwa Rais,
Kwa sasa sijasikia ukizungumzia Tanzania ya Magufuli ni Tanzania ya Viwanda, ambayo itatoa ajira kwa vijana kulingana na wingi wa viwanda hivyo, vijana ambao wako mtaani licha ya kuhitimu fani mbalimbali, sasa nilitaka nifahamu ile Tanzania ya Viwanda uliyoinadi 2015 imeshakamilika?
Kama imekamilika unapozunguka katika kampeni waeleze wananchi Tanzania yako ya viwanda uliyoahidi imeshakamilika ili ujizolee kura nyingi, kwa vijana ambao wamepata ajira katika viwanda hivyo ulivyoahidi.