Je, Tanzania ya Viwanda imeshakamilika?

Ya wasiojulikana, ukiwataja watu wasiojulikana unaambiwa unashirikiana na mabeberu
 
Tayari siku nyingi kilichobaki ni Tanzania kuwa ULAYA[emoji1787][emoji1787]
 
Nilipo mm sijaona kiwanda kipya kilicho jengwa vipo vile vile vya miaka yote sayona, vya bia, coca cola, PepsiCo's n.k

Usiamini maneno ya wanasiasa yeyote
 
Toka Mh. Mwijage, Waziri wa Viwanda atenguliwe, hata vile viwanda 4000 vya cherehani nne havizungumzwi Tena wala ajira za vijana haijulikani zilipotelea wapi hata nguo bado tunavaa mitumba toka kwa mabeberu. Lile Bomba la Mafuta toka Uganda mpaka Tanga hata wenzetu wa Kagera linakoingilia hawasemi limefika wapi ili tujiandae kula bata vijana wakianza kazi.

Stiegler's Gorge umeme ni viongozi tu ndo tunaonyeshwa wanaotembelea mradi lakini kazi ilipofikià hawaonyeshi Ila tunaambiwa trilioni zilizotumika na asilimia ya kazi iliyofikiwa.

Vivyo hivyo SGR ilikuwa ikamilike mpaka Morogoro mwezi November mwaka jana haijulikani imefika wapi Sasa ingawa wanasema ujenzi hmefikia asilimia 70. Kweli hapa kazi tuu!
 
😆😆😆😆
 
Viwanda 100 kila mkoa
 
Tatizo lenu ni kuwa; Hamtaki basi hata kumsapoti ili atuelekeze namna ya kufikia hiyo level ya ulaya. Kila kitu mnaona haiwezekani. Hebu fikiria, Kama tungeweza kuzibiti madini yetu yote vizuri. Mawe kama yale ya Laizer yakiuzwa na serekali si tutainua uchumi? Kama tukiamua kusaga unga tukauza unga badala ya mahindi, je ajira isingelikuwepo? Mtachukua mda mrefu sana kabla hamjamuelewa kiongo wetu
 
Mkuu Tanzania ya Nyerere ilichukua takribani miaka 25 kujenga viwanda 400 tu.Viwanda si majengo tu,ni nguvu kazi,wataalamu,mabingwa,mitambo,nishati,miundo mbinu,masoko na mitaji.
Viwanda siyo rahisi kama like ya Facebook.
Wale waliouza au kuhujumu viwanda vya Nyerere ndio wajinga na malofa waliotufikisha katika hali hii.
 
Mkuu Sasa simumsaidie Muheshimiwa ili tuone hivyo viwanda?.
 
Kama kwa kusema wamejenga viwanda 8,000 wanamaanisha vyerehani na mshine za kukoboa, basi wamefanikisha.
 
Hii ishu ya viwanda na ajira ni fimbo nzuri ya kumchapia Magu na Ccm yake. Wanefeki big time. Viwanda viko wapi?
 
Ni uwekezsji gani mkubwa wa kiwabda hata kimoja tu cha maana ambacho serikali hii inaweza kujivunia? Mfano wa wa kiwanda cha Dangote? Tylipaswa leo walau tuwe na uwekezaji mkubwa wa kiwanda kama cha Dangote si chini ya vitano!
 
Kama ulimsikiliza JK kwenye msiba wa BWM wazo la kuwa na viwanda kwa mujibu wa 2025 vision lililenga kuongeza competitiveness ya Tanzania kwenye regional and global markets.Hili Jambo lilikuwa jema Ila aliyekabidhiwa alishughulikie uwezo hana, Jambo hili la viwanda lilihitaji kutengenezewa strategy na kuweka thinking behind it na si kupayuka tu kwenye majukwaa ya kisiasa.prove kwamba hii issue iko juu ya uwezo wake akaamua kugeukia stend za mabasi,masoko,zahanati na taa za barabarani. Rais wa petty issues
 
Viwnda siyo lazima vijengwe na serikali tumieni akili japo kidogo. Mradi wa umeme wa Mwalimu na Nyerere na SGR ni zaidi ya viwanda 200 kwani ajira itakayotolewa ni kubwa sana.

Leo nilikuwa natoka sokoni majira ya jioni nikapambana na wanafunzi wa sekondari wanarudi nyumbani. Hapo hapo nikajiuliza hivi tuna wanafunzi wangapi kwenye mashule yetu alafu nikafikiria hao wote wakimaliza shule wanaingia kwenye labour market watapata kazi gani hawa?

Kila nchi duniani inalia na unemployment zinazopishana ni rate tu kwa sababu hao wenye viwanda vingine vinafungwa vingine vinapunguza wafanyakazi mfano tu British airways wanapunguza wafanyakazi zaidi ya asilimia arobaini zaidi ya wafanyakazi 6600, Kenya airways nao wanapunguza marubani zaidi ya asilimia thelathini. Kwa nchi za ulaya ni ujerumani tu ndio wamefanikiwa kutoa ajira nyingi kwenye viwanda mpaka kwa raia wa nchi za EU
 
Viwnda siyo lazima vijengwe na serikali tumieni akili japo kidogo. Mradi wa umeme wa Mwalimu na Nyerere na SGR ni zaidi ya viwanda 200 kwani ajira itakayotolewa ni kubwa sana...
Nani kasema viwanda vinajengwa na serikali? Tunazungumzia mazingira wezeshi ili kuvutia wawekezaji!
 
Usije ukakaa ukajidanganya kumuamini.Amekuwa na ahadi Lukuki za uongo na maneno mengi ya uongo. Milioni50 kila kijiji? Laptop kwa kila mwalimu.

Dodoma huku alituahidi hospital tangu 2017 hadi leo Hospital ya uhuru
Uwanja wa kisasa kwa ufadhiri wa mfalme wa Morroco chali

Miradi yote kujengwa kwa fedha za ndani
Juzi katuambia kuwa nyerere alitawala miaka 27. Nk nk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…