Je, teknolojia ya roboti wanaoongea ilikuwepo wakati wa Musa na Haruni kama Kurani?

Kwanini leo hakuna wengine wanaoandika vitabu vikoangezwa kwenye Biblia? Tatizo nini?

Sent using my NOKIA torch

Naona huna uelewa kuhusu ni nini maana ya maandiko matakatifu.Toka Yesu aondoke, watu wameandika sana juu ya ujumbe ule ule kwamba Mungu ni nafsi tatu,kwamba Yesu ni nafsi ya pili ya Mungu, aliyekufa na kufufuka na kwamba atarudi kuwahukumu wanadamu wote, akiwemo na Muhammad na kwamba Yesu hakuwahi kumtabiria Muhammad utume.Sasa fikria yote hayo yaliyoandikwa na watu maelfu, vitabu vyao vimeongezwa pamoja katika vile vya Biblia hali ingalikuwaje? Unafikiria winchi isingalitumika katika kuinyanyua Biblia?
 

Kusoma na kuacha kuchangia hakumaanishi kwamba watu hawajaupata ujumbe stahiki.Kusoma ni jambo moja na kuamua kuchangia ni jambo jingine.Maana ya chapisho ni kufikisha maudhui.Maudhui yamefika na si lazima watu wajibu humu.Wengine wanaweza kujibu kwa kwenda kuandika vitabu au kwa kujipatia ukweli tu na kisha kuufanyia kazi.
 

Umeandika vizuri sana hasa reference ya Wasamaria , Lakini napata shida kujua nia yako hasa ni nini ? unataka kufanikisha nini kwa hii post . Kwa mkristo wa kweli huwa role model wake ni Yesu . Yesu alihubiri Upendo kama amri kuu na alionyesha kwa matendo yake . Nafikiri umeisoma biblia vizuri Luka 6:42, Pia Mathayo 7:5, Tujiweke vizuri kwanza na kwa matendo yetu mema tuwavute wengine watufuate kwani kutengeneza chuki hakuna faida yeyote soma Mithali 18:19
 

1. Nakushukuru kwa kukumbuka kwamba Yesu alifundisha upendo.Je,unakumbuka kwamba kabla ya kuonyesha upendo huo kwa kuuishi,Yesu alianza kwa kufafanua maana ya upendo huo? Unakumbuka alianza kwa kufundisha kuwa Amri kumi(Decalogue) ni mahusiano chanya kati ya mwanadamu na Mungu wake kwa upande mmoja na mahusiano chanya kati ya mwanadamu na mwanadamu kwa upande mwingine?

2. Kwa staili ya uandishi wako, inaelekea wewe ni Mkristu na tena pengine u Mkatoliki.Je,umewahi kujiuliza,kwa uweza wa Kristu aliokuwa nao kama Mungu, ni kwa nini alipofika duniani hakuamua kuhubiri kwa njia ya maisha yake pekee, bali alieleza yote aliyotumwa na Baba yake kwa njia ya maneno na mawazo?

3. Je,kwa kiwango cha uelewa mkubwa ambao nimeuona katika uandi wako, umeshindwa kabisa kuelewa maudhui ya uzi huu na nyuzi zingine ambazo nimeshazipandisha humu?
 

Nadhani wengine tunaelewa vibaya maana ya Role Model.Kuna namna mbili za kuonyesha kuwa mfano:mosi,kwa kufundisha na kufafanua mambo chanya na yale hasi dhidi ya huo uchanya na pili,kwa kuishi kuelekea huo mtizamo chanya.Sasa kwa post hii umeona mimi siishi maisha chanya ya Kikristu?
 
Utapata tabu saaaaaaaaaana

Tabu ipi tena? Tabu ni changamoto tu katika maisha na mara zote hulenga kumbainishia mwanadamu uelekeo sahihi kimaisha.Je,wewe unaoziogopa taabu? Bila taabu dunia isingalikuwa inapendeza namna hii.Suala sio taabu maishani, bali kuziona taabu sio fursa katika maisha bali ni taabu tu.
 
Too much thinking of the unthinkable, stay on your lane.
 
Nimefika ulamaa gwiji kwanza tunashukuru ile ya wadudu kuongea UMEELEWA sasa umekuja na ROBOT kabla sijaanza kueleza jambo kuhusu aya 20:85-96 nataka kufahamu mtoa mada ROBOT unalielewaje?
 
Halafu nimeona mahali unasema mohamadi kaguswa nyayo na samaria ww mzee mbona unaleta mambo yasiyo kuwepo unafahamu tafsiri ya nyayo hapo? halafu unaweza kuthibitisha ni za mtume? nakusubir mada hii naimaliza mapema tu kama ile wadudu kuongea
 
If you don't dare thinking much, then the difference betweeen a live man and a dead body is not in position.If further thinking too much was not taken into existence,then the World in view would not be existing.
Nimefika daktari bingwa unafahamu nini kuhusu ROBOT ? kabla sijakusaidia tatizo lako
 
Nimeshakwambia biblia sio rejea ya QURAN kwasababu biblia inamakosa mengi na biblia HAIJAKAMILIKI mambo mengi mmeyaacha
 
Kwanza hapa umekosea....waislam hawategemei biblia kuthibitisha utume wa muhammad. Quran yenyewe inamueleza muhammad ni nani.

Sent using my NOKIA torch
Huyu bwana anaisoma Quran kama gazeti la shigongo sasa nataka nimuweke sawa humu awezi kuleta uongo kama mimi nipo hai
 
Ahahahajaaha biblia tunaitumia kukupa mifano huweze kuelewa kirahisi maana akili yako bila mifano madhubuti utazurura sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…