Je, tukemee udini, ukanda na ukabila au? Je, neno Sukuma Gang si neno la kibaguzi? Mnaonaje tukiungana kukemea ubaguzi wowote kwa jina lolote?

Je, tukemee udini, ukanda na ukabila au? Je, neno Sukuma Gang si neno la kibaguzi? Mnaonaje tukiungana kukemea ubaguzi wowote kwa jina lolote?

Hivi yule aliopanda jukwaa la kanisani akawaponda wa Zanzibari yuko wapi? Unamkumbuka?

Mwenyezi Mungu hafanyiwi utani, haikupita muda Mzanzibari akaoa binti yake, haikupita muda, Mzanzibari akawa Rais wake.


Yuko wapi? Au umemsahau?
Yupo anabana bana pua tu,alichezewa karata tatu hana hamu.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Anajaribu kupotosha kweli kuwa katika watu wabaguzi Magufuli anaongoza, siyo Magufuli aliyewabomolea nyumba wakazi wa kimara lakini kwa sababu ile ile akasema wakazi wa Mwanza wasibomolewe, huu siyo ubaguzi?
Na Pascal hili hakemei kwa sababu lumefanywa na msukuma mwenzake.
That is the kick of a dying horse, Pascal ni mnafiki hakuwahi kukemea maovu ya Magufuli bali kuyatetea.
Alijitahidi kuanzisha nyuzi za kumtetea anapokosolewa na taasisi za nje.
Now he is crying foul anasahau what goes around comes around, kuna waliolizwa na ubaguzi wa Magufuli hakuwaona ila sasa godfather wao hayupo wanalia.
Sukumagang ni kundi wanufaika wa itikadi na utendaji wa Magufuli in power, has got nothing to do with wasukuma kama kabila bali wanufaika ambao bahati mbaya wengi ni wasukuma
Yule alikuwa shetani katika umbile la binadamu. Mungu aepushie mbali tusijepata mtawaza sampuli ile tena.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Wanabodi,

Kama kawaida yangu kila nipatapo fursa, huja na makala hizi za "Kwa Maslahi ya Taifa" ambazo hizileta kwa mfumo wa swali fikirishi na mimi kutoa tuu maoni yangu lakini kukupa wewe msomaji fursa ya kufikiri, kushauri na kutoa majibu unayoona yanafaa.

Swali la leo ni kuhusu kuibuka na kuchopuka kwa viji sentiments vya viashiria vya ubaguzi wa udini, ukanda na ukabila, sasa jee ni tuunganishe nguvu kukemea au roache tuu ukiisha ota na kukomaa ndipo tuukate?. Ubaguzi Ubaguzi huu wa kisasa unafanywa kwa viji neno neno vya kibaguzi, je neno Sukuma Gang, sio neno la kibaguzi?. ni neno tuu la kawaida tuliache au ni neno la kibaguzi linalostahili kukemewa?. Je mnaonaje kama Watanzania tukiungana kukemea vijineno neno vyenye viashiria vya Ubaguzi wa aina yowote kwa jina lolote?

Nimeileta hoja hii kufuatia as days goes by, hizi issues za hii kitu inayoitwa Sukuma Gang is escalating to the point of unbecoming!. Sukuma gang ni itikadi siyo kabila

The Mkuu Sexless , kwanza nikupongeze kuileta hoja hii, pili japo ni kweli neno Sukuma Gang ni itikadi tuu, lakini si kweli kuwa iliasisiwa na Magufuli!. Tumwacheni Magufuli apumzike kwa amani!. Voices From Within: Je, wajua yuko Peponi, Mbinguni, Kwa Baba yake? Why kumshutumu, kumsakama na kumsimanga? Aachwe apumzike kwa amani

Neno Sukuma Gang ni a fictitious Group that doesn't exist in reality lililobiniwa na yule Kigogo wa Twitter na watu wajinga wajinga wenye akili fupi wakaamini hili kundi ni kweli lipo!. Kiukweli kabisa Sukuma Gang sio kundi la kweli, halipo popote and don't exist anywhere in reality except ndani ya vichwa vya watu waliofilisika kisiasa!

Pia sii kweli! bali baada ya Kigogo wa Twitter kuliasisi kundi hili fictitious, akatumia nguvu kubwa kulifanyia indoctrination kuwa hili kundi does real exist, hivyo wale watu wa Magufuli na watu wote wanaomsupport Magufuli wakawa pointed kuwa ni members wa Sukuma Gang, hata mimi ni Msukuma, na namsupport Magufuli na sio Sukuma Gang!

Hakuna kitu kama hiki, ila kwa vile indoctrination ya existence ya uwepo wa kundi hili imefanyika na watu wenye akili fupi waliofilisika kisiasa wakaamini', kama na wewe unaamini kuwa kundi la Sukuma Gang kweli lipo and does exist in reality, ujijue ni akili fupi and muflis kisiasa kama wale muflis wengine wote wanaoamini ujinga huu!

Hapa nakuunga mkono!

Kumchukia mtu yoyote kwasababu yoyote sio jambo jema! Dini zinatufunza hata adui mpende!. Hivyo it's not right kumchukia mtu yoyote!

Japo hii shana ya the existence of the Sukuma Gang ni dhana tuu, na the Sukuma Gang ni just a fictitious Group that doesn't exist in reality, lakini kufuatia indoctrination iliyofanywa na yule Kigogo wa Twitter, watu wenye akili ndogo, akili fupi na waliofilisika ki fikra, wakaamini, hivyo chuki dhidi ya Wasukuma is real!. Hili sio jambo jema!.

Kufuatia kabila la Wasukuma kuwa ndilo kabila kubwa Tanzania kuliko makabila yote, zikitokea nafasi zozote za uongozi, na watu wote wako huru kugombea, obviously Wasukuma pia lazima watakuwepo.

Kulitokea nafasi fulani za uongozi ndani chama fulani, wakajitokeza wagombea 186 kugombea nafasi 8 aa uongozi. Miongoni mwa waliojitokeza walikuwepo Wasukuma wengi tuu ila mimi nawajua kulikuwa na Wasukuma wawili ambao kama wangepitishwa wangetupatia wawakilishi wazuri the best of the best.

Ikasemekana kuwa mmoja kati ya hao Wasukuma wawili ni member wa the Sukuma Gang!. Then kwenye mchujo ikaelezwa kuwa wamepewa maelekezo hatua ya kwanza kabisa ni kuwakata Wasukuma wote waliojitokeza!. Na kweli Wasukuma woote tukakatwa eti ni Sukuma Gang! This is not fair at all! Taifa linakosa uwakilishi wa watu wazuri kwa ubaguzi wa kijinga kabisa!

Na katika hili naomba na mimi nijiunge kwenye kukemea hii sumu ya ubaguzi mbaya kabisa ya kuwabagua Wasukuma kwa kisingizio cha Sukuma Gang, na naomba kutamka kama kuna Msukuma yoyote popote ameadhibiwa au kubaguliwa kwa kisingizio ni member wa the Sukuma Gang, then dhambi hiyo ya ubaguzi, itawatafuna wabaguzi hao kupitia kitu kinachoitwa karma! Karma haina mswalie Mtume wala haijali nani ni nani!

Paskali
Hilo ni neno la kibaguzi,kikabila hasa.In fact nashangaaa wanasiasa na mashabiki wao badala ya kusimama na walio hai,wanadeal na waliokufa.

Kila ukiongea hoja ya kukemea mabaya ya serikali ya sasa utaitwa hilo jina,ukionekana ni wa kanda ya ziwa utaitwa hilo jina,binafsi siamini kama kuna mwanasiasa ana nia njema na nchi hii tofauti na maslahi binafsi kwanza.

Sio kuwa serikali hii ina mabaya tu,ina mazuri mengi,lakini kama taifa hatuko sawa tukiendelea na vimaneno vya hivyo.Hivi hao wasukuma wanajisikiaje ndani ya nchi yao kwa kuitwa jina jina hilo au lenye maana mbaya kwa mlengo wao?.
 
Tuwaite BANYAMULENGE

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
Nani hao wakosoaji wa Samia na wakosoaji wa maridhiano ya Samia na Chadema? Maana kuna member ni chadema kindakindaki ila utofauti wao wa mawazo kwenye maridhiano ya Samia na Chadema inafanya aitwe Sukuma gang.

Siku hizi wakosoaji wamekuwa wanaitwa sukuma gang.
 
Hawapondwi Wasukuma bali wanapondwa wafuasi wa yule Mhutu ndiyo maana nimependekeza waitwe BANYAMULENGE.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
Hilo neno sukuma hapo halipo kwa bahati mbaya, haingii akilini et wafuasi wa Magufuli ufikirie kuwaita sukuma halafu useme haihusiani na kabila la wasukuma. Yani mie niwaite mashoga wote kuwa ni wapemba gang halafu niseme haihusiani na wapemba nitaeleweka?
 
Na katika hili naomba na mimi nijiunge kwenye kukemea hii sumu ya ubaguzi mbaya kabisa ya kuwabagua Wasukuma kwa kisingizio cha Sukuma Gang, na naomba kutamka kama kuna Msukuma yoyote popote ameadhibiwa au kubaguliwa kwa kisingizio ni member wa the Sukuma Gang, then dhambi hiyo ya ubaguzi, itawatafuna wabaguzi hao kupitia kitu kinachoitwa karma! Karma haina mswalie Mtume wala haijali nani ni nani!
Mkuu umestuka muda huu?
===
Nilikemea jambo hili humu (JF) mara tu baada ya kuanza kukubaliwa na moderators!!! Wakati huo nadhani nilionekana kituko kwa walio wengi!
 
..Kwa mfano, kuna siku Raisi Magufuli alikuwa ktk ziara na akasimama kusikiliza matatizo ya wananchi. Yuko mama mmoja badala ya kuwasilisha shida zake kwa Kiswahili, alizungumza na Raisi kwa lugha ya kabila lao.

..Je, mwananchi huyo alikuwa hajui Kiswahili? Au mwananchi huyo aliamini kuwa Raisi Magufuli anaingilika kwa " angle " ya ukabila? Kwanini?




..Matendo na mwenendo wa Magufuli kama kiongozi wa nchi ndiyo yaliyopelekea kuzuka kwa jina " Sukuma Gang. "

Aisee kwa hapa nilipoku quote umenishangaza sana,hivi kwa akili yako unaamini kila mtu anafahamu kiswahili? Kuna ubaya gani kwa huyo Mama kuongea Kisukuma? Bibi na Babu yangu wote hawafahamu Kiswahili,ingetokea wamekutana na JPM na wanafahamu ni Msukuma wangeongea nae kwa lugha ipi? So unawahukumu Wasukuma kuwa ni watu wabaguzi kwakuwa tu yule Mama aliongea na Rais kwa kisukuma?

Kwamba matendo ya JPM ni pamoja na kuongea na yule Mama kwa kisukuma kwako wewe ilikukera sana? Mnajaribu kujificha kwa kuzunguka zunguka lakini deep down mna chuki na ubaguzi mkubwa na Wasukuma.
 
Magufuli alikuwa nafanya Serikali kama Mtei alivyo kuwa Boss wa CRDB.Mtei amejaza wachaga CRDB unaweza ukahisi ni Bank ya Wachaga-kati ya Wafanyakazi 10 wa CRDB 8 ni Wachaga.
Samahani mkuu waweza kunitajia Full Ministries achana na Manaibu wa5 tu ambao walikuwa wasukuma kipindi cha JPM ili tulipe uhalali bandiko lako mkuu
 
Elewa kinachojadiliwa, mie nazungumzia hayo madai yenu ya kusema hamna tatizo na kabila la wasukuma wakati huo huo mmewabatiza watu jina la sukuma gang mkikusudia ni watu wabaya.
Kwa sababu huna akili hebu kwanza tupe uthibitisho kuwa asilimia kubwa ya mashoga Tanzania ni wapemba?

Pili hii yako siyo ubaguzi ila inakukera tu sukumagang? Sukumagang ni kundi wanufaika wa matendo ya dikteta Magufuli aliyeamua kuwajaza wasukuma wenzake kwenye nafasi za uongozi serikalini.

Mwisho kwa matendo ya Magufuli na kundi lake maarufu sukumagang bila shaka ni watu wabaya. Hakuna walioumizwa na utawala wake na wateule wake kama akina Sabaya?
 
Back
Top Bottom