Kabisa .
Inaonekana ako na husuda kali sana ambayo ni hatari kwa afya yake.
Kaka mm ni mtu anataka mageuzi kuliko wewe pengine. Lakini mageuzi yetu yataletwa na wakati sio mtu kama Lissu au Mbowe au kikundi. Wakati ukifika mageuzi hayatazuilika.
Kwanini? Watanzania Wana nafuu kwenye Kila kitu chao (amani, utulivu, malazi, matibabu, chakula, shule, barabara, usafiri, bamdari , ardhi, fursa) kuliko majirani wetu wanaotuzinguuka. Hatujutii Bado kuwa hivi tulivyo sasa.
Mbowe, Lissu, mtikila na wengine walipigwa na kutiwa mahabusu kwa siku kadhaa lakini hakukuwa na nguvu ya umma iliyowatetea kuonyesha kuwa umma haujawa tayari kukumbatia mageuzi na wanamageuzi; muda bado, muda bado muda bado kabisa kwakuwa watanzania Bado Wanazo options nyingi kuliko majirani zao Kenya. Hapa kwetu kiongozi wa upinzani atategemea utetezi wa wazungu zaidi kuliko umma wa watanzania pale mambo yake yatakapomwendea vibaya kisiasa.
Kifupi watanzania hawataki vurugu za kisasa Bado, maana wanavyo vingi vya kupoteza; they have properties to safeguard.
Kama mtu haamini maneno yangu Hebu ajaribu kuitisha maandamano aone wangapi watahidhiria na wangapi wako tayari kusogelea bomu za machozi.
Tusidanganyane, Lissu na familia yake wote Wanazo passport za kusafiria na kuishi ubelgiji bila shida, na watoto wake inawezekana kuwa hawako Tanzania kabisa.
Lissu atasababisha chadema kifutwe kwenye daftari la msajili wa vyama kwasababu zitakazotolewa na ofisi ya msajili na kusiwe na cha kufanya. JPM alisitisha shuguli zote za vyama vyoooote vya siasa na sikuona nguvu ya umma iliyopinga sembuse chadema TU.?