Je, Tundu Lissu atakutana na Rais Samia Suluhu Ubelgiji?

Kama sio kukutana na Lissu basi anawapeleka wale watu wake aliosema hawawezi kumpiga mtu risasi tatu wakamkosa
 
KIVULI CHA JINAMIZI LA KUKOSEKANA HAKI CHAZIDI KUKUA

Hili jinamizi la Tundu Lissu kushambuliwa na watu wasiojulikana mpaka leo vyombo husika kushindwa kukamilisha uchunguzi, Kesi namba 16/ 2021 ya ugaidi inayomkabili Freeman Mbowe na wenzie watatu, kuminywa kwa demokrasia, kukabwa kwa uhuru wa kupashana habari, utendaji usioridhisha wa vyombo vinavyohusika uchunguzi wa tuhuma pia kutoa haki ni jinamizi linalozidi kuongezeka kivuli chake kiasi kila mdau ndani na nje anaona kivuli hicho kikubwa cha ukiukwaji wa haki na kuhoji kulikoni.

 
Wakati mama anapanga kufanya hiyo ziara ulipasa kumuuliza kama katika ziara yake anampango huo
 
Mkuu kila kitu kipo chini ya usimamizi imara sana .

Kumbuka kuwa cdm ni taasisi kubwa sana hapa nchini.

Anza kuhesabu toka juzi kesi ya mh Mbowe ina ahirishwa na jamhuri kufunga ushahidi wake kabla ya hesabu yao kukamilika.

Hesabu na leo hii mama Samia kukutana na makamu mwenyekiti pale ubelgiji.

Tuendelee kuvuta subira kama kawaida yetu.

Ila hili ni pigo kubwa sana kwa sukuma gang na wale kina kajamba nani pale lumumba.
 
Mkuu Erythrocyte, hongera sana kwa bandiko hili, uliona mbali. Hii inaitwa trends reading.
Hongera sana.
P
 
Maandamano ni "janga" utakuwa umetoka safari ya chooni!
 
16 February 2022
Brussels, Belgium

LIVE : TUNDU LISSU MAKAMU MWENYEKITI WA CHADEMA ANA 'SHARE' NASI NINI WALIZUNGUMZA NA MH. RAIS SAMIA HASSAN KWA MUDA WA SAA MOJA MJINI BRUSSELS


Source : Nadj Media Centre
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…