Je, ualimu ni kwa ajili ya watu maskini?

Je, ualimu ni kwa ajili ya watu maskini?

Prakatatumba abaabaabaa

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2022
Posts
1,842
Reaction score
6,087
Leo nimejisikia vibaya Sana baada ya kumsikia Mzazi mmoja akimgombeza Mtoto wake aliyekua na ndoto ya kusomea ualimu, maongezi yao yalikua hivi.

Mtoto: baba Mimi nataka kusomea ualimu.

Baba: hivi umechanganyikiwa? yaani uende ukawe Mwalimu? Walimu Wana maisha gani? Eeeh! Wana kipi Cha maana? Sitaki kusikia hizo habari zako Bora ukaombe chuo Cha diploma uombe hata clinical officer nitalipa ada.

Yale maneno yamenifanya nitafakari Sana, kundi la walimu linaonekanaje? Mbona wapo wengi wenye uwezo? Hivi Kuna mtu yoyote anatamani angelikua Mwalimu? Je kutopewa heshima kwa walimu inasababishwa na nini? Je ni ugumu wa kazi? Au salary ni ndogo? ..

Mwisho, unaweza kuruhusu mtoto wako asomee ualimu?
 
Ukifuata maoni ya watu hakuna kazi isiyokosolewa, kikubwa jiamini na kazi yako ata kama ni kazi ya kusafisha vyoo. Wapo watu wametoka familia zenye uwezo mkubwa kiuchumi na wanazunguka na mabahasha miaka ajira hawapati. Ishu ni mindset tu hakuna kazi mbaya
 
Uzuri ni kwamba hata wawaponde walimu kiasi gani, kila mwaka vyuo vya ualimu vinasajiri wanafunzi wengi sana kuanzia certificates hadi degree,.. Penda na heshimu kazi yako mkuu asitokee mtu wa kukukatisha tamaa, kuna walimu wako mtaani wana vyeti wanatamani hata wapate mahali wafundishe part time lakini wamekosa...Jivunie ulichonacho💪💪
 
Leo nimejisikia vibaya Sana baada ya kumsikia Mzazi mmoja akimgombeza Mtoto wake aliyekua na ndoto ya kusomea ualimu, maongezi yao yalikua hivi.
Mtoto: baba Mimi nataka kusomea ualimu.
Baba: hivi umechanganyikiwa? yaani uende ukawe Mwalimu? Walimu Wana maisha gani? Eeeh! Wana kipi Cha maana? Sitaki kusikia hizo habari zako Bora ukaombe chuo Cha diploma uombe hata clinical officer nitalipa ada.

Yale maneno yamenifanya nitafakari Sana, kundi la walimu linaonekanaje? Mbona wapo wengi wenye uwezo? Hivi Kuna mtu yoyote anatamani angelikua Mwalimu? Je kutopewa heshima kwa walimu inasababishwa na nini? Je ni ugumu wa kazi? Au salary ni ndogo? ..

Mwisho, unaweza kuruhusu mtoto wako asomee ualimu?
Bila mwalimu, nani angefundisha mwanafunzi sasa?, Huyo mzazi akili yake haina akili,
 
Kwa ujumla ni namna maisha ya waalimu yanavyoonekana katika jamii. Ila wakicheza na mikopo na kuwa na nidhamu ya pesa watatoboa.
Inabidi hazina waongeze nguvu Sasa kwenye mikopo yao ya halmashauri, zipunguze ukiritimba ili ziwasaidie walimu, kuliko kwenda kukopa NMB,CRDB unakopa Million 20 unarudisha million 38 Sasa si wizi huo?
 
Vitoto vyangu 2 sijawahi kusikia wameropoka kuwa wanataka kuwa walimu.
Yaani bora kazi yangu ya kushika bunduki huyu wa miaka 7 anaipemda sana.
Najitahidi kumkemea ila kakomaa hayumbishwi.
Nadhani ni utoto.
Ila ni heri MWALIMU kuliko askari.
Utofauti wao ni uhuru labda, lakini ualimu naona Kama hauna issue nashuhudia watu wapo kwenye kada mwaka wa 20 lakini akikosa nafasi ya kusimamia mtihani ni mgogoro.
 
Back
Top Bottom