Ualimu ni fani moja nzuri na yenye soko kubwa kama utajua namna ya kujiongeza. Kwasababu kila siku watu kuna jambo wanataka kulifahamu so watahitaji mwalimu wakuwafundisha.
Tatizo ni kuwa vijana wengi wanaohitimu ualimu wanabaki kuwa waalimu wa masomo waliyosomea chuo utasikia mimi mwalimu wa jiografia mara kiswahili au sayansi, wameshindwa kutumia ujuzi na maarifa yao ya kufundisha kufundisha wqtu mambo mbali mbali.
Mfano, kama mtu kasoma ualimu alafu akajielimisha juu ya matumizi ya AI labda ChatGTP au hata sanaa fulani kama muziki au jambo lolote akawa na ufahamu wa hilo jambo anauwezo wa kuhamisha ufahamu au ujuzi wake huo kwa watu wakamuelewa na kumlipa.
Kifupi ukisoma ualimu ukahitimu wafundishe watu vile unavyovifahamu au kuwa na kipaji navyo serious kwa kutumia maarifa ya ufundishaji uliyonayo.
Najua ni ngumu na pengine nikaonekana motiveshno spika ila bila kuwqza nje ya box mwqlimu hauwezi kutoboa japo ndio fani yenye wateja wengi kuliko fani zingine zote.
Umeshindwa yote anzisha basi twisheni au homework aider kwa njia ya digitali uwe unafanya mambo kama mtaaluma sio mbabaishaji, watu wana smartphone wanaweza kutumia na watoto wao. Ujue sio kila mzazi anajua kutafuta kipenyo a kipeuo, why asijiunge na program yako kama inamuondolea aibu ndogo ndogo na mwanae anapata elimu.
Watakulipaje, jisajili Lipa kwa simu kuwa na website na App ya android na Ios fanya kazi kama msomi. Vaa vizuri, eneo la ofisi smart, tumia kamera quality, set up nzuri usikike vizuri, engage na mteja wako. Nusu saa Tsh. 200 hapo una wateja 10+
Ila uandae mtaji wa kama milioni tatu, maana hakuna biashara ya maana isiyo na mtaji wa pesa.
Kwa atakayeokota jambo haya, kila la heri ndugu mwalimu