Prakatatumba abaabaabaa
JF-Expert Member
- Aug 2, 2022
- 1,842
- 6,087
Bila mwalimu, nani angefundisha mwanafunzi sasa?, Huyo mzazi akili yake haina akili,Leo nimejisikia vibaya Sana baada ya kumsikia Mzazi mmoja akimgombeza Mtoto wake aliyekua na ndoto ya kusomea ualimu, maongezi yao yalikua hivi.
Mtoto: baba Mimi nataka kusomea ualimu.
Baba: hivi umechanganyikiwa? yaani uende ukawe Mwalimu? Walimu Wana maisha gani? Eeeh! Wana kipi Cha maana? Sitaki kusikia hizo habari zako Bora ukaombe chuo Cha diploma uombe hata clinical officer nitalipa ada.
Yale maneno yamenifanya nitafakari Sana, kundi la walimu linaonekanaje? Mbona wapo wengi wenye uwezo? Hivi Kuna mtu yoyote anatamani angelikua Mwalimu? Je kutopewa heshima kwa walimu inasababishwa na nini? Je ni ugumu wa kazi? Au salary ni ndogo? ..
Mwisho, unaweza kuruhusu mtoto wako asomee ualimu?
Yeah, hii ndio point naona zingine ni motivation tu.Ni kweli.
Uliona mtoto wa tajiri gani anasomea ualimu!!
Inabidi hazina waongeze nguvu Sasa kwenye mikopo yao ya halmashauri, zipunguze ukiritimba ili ziwasaidie walimu, kuliko kwenda kukopa NMB,CRDB unakopa Million 20 unarudisha million 38 Sasa si wizi huo?Kwa ujumla ni namna maisha ya waalimu yanavyoonekana katika jamii. Ila wakicheza na mikopo na kuwa na nidhamu ya pesa watatoboa.
Akifika kazi mnayo Aloooh ahahaha jamaa hapend maticha yule aloo acha kabisaHuu uzi tuombe sana usionwe na Mpwayungu Village
Utofauti wao ni uhuru labda, lakini ualimu naona Kama hauna issue nashuhudia watu wapo kwenye kada mwaka wa 20 lakini akikosa nafasi ya kusimamia mtihani ni mgogoro.Vitoto vyangu 2 sijawahi kusikia wameropoka kuwa wanataka kuwa walimu.
Yaani bora kazi yangu ya kushika bunduki huyu wa miaka 7 anaipemda sana.
Najitahidi kumkemea ila kakomaa hayumbishwi.
Nadhani ni utoto.
Ila ni heri MWALIMU kuliko askari.
Nadhani alilenga kwenye pesa, maana alimkazia kwamba je Kuna mwalimu gani mwenye pesa? Nikawa najiuliza hivi huyu mzee mtoto wake anaweza kuchumbiwa na Mwalimu kweli?Bila mwalimu, nani angefundisha mwanafunzi sasa?, Huyo mzazi akili yake haina akili,