Je, Uchawi una mchango wowote katika kukuza Biashara?

Je, Uchawi una mchango wowote katika kukuza Biashara?

Nimeishi kigoma, pangani, tanga mjini, sumbawanga, namanyere, lyambamfipa, shinyanga, bariadi huko wanasema kuna mlango wa kuzimu, pemba na mafia kote huko nk nk lakini sijawahi kukwamishwa jambo langu kwa namna yoyote ile ya kichawi labdq figisu tu za kuchongeana kwenye majukumu. Mm siamini katika utajiri ni nguvu za shetani bali naamini utajiri ni katika juhudi na mawazo yetu katika kufanya kazi.
Imani nzuri kabisa! Stress free zone
 
Hakuna uchawi, juhudi binafsi katika utafutaji ndio daraja litaloweza kukufikisha kwenye point ya utajiri

Africa tuko kwenye rank za juu kabisa katika mabara yenye imani za kishirikina, lakini hatujaweza kutoa hata mchawi mmoja kwenye top 10 ya mabilionea

Swali la kizushi kwa wewe unayeamini uchawi

Utachukua reaction ganu siku ambayo umemuajiri mtu akuuzie duka lako halafu baada ya siku kadhaa akaja kukuambia ule mtaji wote umesombwa na wachawi kupitia chuma ulete??
Uyo napiga nagalagaza kwenye moto! But hata wazungu wanafanya hizi makitu
 
Sizungumzii kwa wengine, ila kwangu binafsi.

Nafanya biashara ya kifedha (za mtandao na benki). Mwaka 2018 nilipigwa tukio na wakulungwa wakaondoka na 28+ Million cash, simu na mashine za benki.

Nilimpigia simu mama yangu kumueleze maswaibu yaliyonipata. Alishangaa sana nimesurvive vipi zaidi ya miaka 5 bila kuzindika eneo langu la biashara.

Akanitaka niende nyumbani kwa mwitikio wa haraka. Baada ya kuandika maelezo polisi, jioni nikazama nyumbani.

Akanipeleka kwa mzee mmoja. Wala siyo mchawi, ila ni mtaalamu wa kuzindika.

Kuzindika siyo uchawi. Nikampeleka mjini. Akafanya yake akarudi.

Nimeshakosa majaribio matatu ya kuvamiwa.

Na ripoti zote nazipata kutoka polisi. Wakivamia na kukamatwa, wakihojiwa wanasema walipanga kuja kuniibia. Ila mikakati yao inafeli.

Zindiko ni muhimu sana.
Zindiko linampa Nani mamlaka ya kulinda bness? Je, ukishazindika nini kinatoa ulinzi hapo? Kama ni Majini basi ni Uchawi huo
 
Huu ushahidi bado haujitoshelezi mkuu, mm nilifikiri baada ya ripoti kufika kwa mtaalamu pesa zikarudi katika mazingira ambayo na wewe ya kuliacha katika wakati mgumu bila kuelewa nini kilitokea.
Walirudishaje?
 
Huu ushahidi bado haujitoshelezi mkuu, mm nilifikiri baada ya ripoti kufika kwa mtaalamu pesa zikarudi katika mazingira ambayo na wewe ya kuliacha katika wakati mgumu bila kuelewa nini kilitokea.
Hii ya kurudisha mali iliyoibwa ipo. Kuna sehemu panaitwa baraki(mara) kulikuwa kuna bibi mmoja mjaruo (sijui kama bado yupo hai) kama ukiibiwa ukaenda kwake anakwambia ulete udongo au mchanga wa sehemu kile kitu ulkipokuwa umekiweka kabla ya kuibiwa. Ndan ya siku 2-3 utamkuta yule aliye iba amekirudisha anakusubiria akukabidhi.
 
Ngoja nikupe elimu kidogo kuhusu utajiri
Kwanza kuanzia Leo utambue hili, Mungu alipomuumba Adam na Eva aliwapa utajiri wote wa duniani na fahari zake wazimiliki, lakini walipohasi kwa Mungu kwa kumsikiliza shetani, utajiri wote wa duniani ukawa ni Mali ya shetani, wanadamu hatumiliki tena utajiri wa hapa duniani.
Sasa ili kuwa tajiri una options mbili tu
(1) umuombe shetani akupe sehemu ya utajiri anaomiliki, hii inawezekana kama ukikubaliana na masharti yake, na siku ukienda kinyume anakunyang'anya.
(2) umuombe Mungu akupe sehemu ya utajiri alioushikilia Shetani, na hii inawezekana kama utakuwa muombaji sana na mtakatifu haswa, kumyang'anya shetani sehemu ya utajiri wake si rahisi kihivyo.

Usijidanganye kama unaweza kuwa tajiri kwa kufuata seminar za motivation speaker peke yake, utajiri wote anao shetani, ni either uungane naye au upambane kumyang'anya.
Kweli tupu mzee baba, umetisha sana
 
Wiki iliyopita nilitoka Moshi nikaenda kumtembelea classmate wangu pale Arusha. Jamaa ni engineer wa computer. Jpili baada ya kula Ibada Safi na kwaya kali pale St. Theresa tuli-mount XR 250 na tukaenda kufunga Camera za usalama kwa nyumba mpya ya Tajiri mmoja wa Kanda ya Ziwa. Huyu mjuba kajenga mjumba wa kuishi wa ghorofa mbili. Pale kwake pazuri asee, kama Ikulu ati.

Basi tukiwa tunakomaa na kazi (mie sio mtaalam but nilikua Nampa kampani msela) jamaa alikuja na Range lake kutuletea Vifaa kadhaa. Baada ya kukabidhi alisepa. Basi jamaa yangu akawa ananiongelesha kwa kispanish chetu cha kuunga unga na solotepu. Akanambia huyu mjuba ni mchawi balaa. Pale kwake tulikuta watoto wawili wa kiume mandondocha wanatematema udenda tu. Jamaa akanambia ni watoto wake wa kuzaa kabisa na ndo wanalinda business zake. Yes, jamaa Ana biashara kubwa ya Hardware na electronics. Nasikia pia Ana Real estate bila kuhesabu biashara nyingine huko kwao! Pale tu nilihesabu magari 4 makali bila kuhesabu maroli ya biashara. Alikua na chale Kadhaa usoni na mikononi. Inasemekana biashara zake kazizindika kwa makafara balaa!

Sasa tujiulize, je, Uchawi una nafasi gani katika kukuza Biashara? Kuna ukweli wowote katika kuinua biashara?

Je, kwa nini tusiusome ktk masomo ya vyuoni kwa maendeleo ya umma?
Huyo jamaa ni Mpare au Mchagga maana hawa watu wana vitu vya hajabu sana na hawaoni hasara kuharibu ama kuua watoto wao ili tu wapate kuwa matajiri.
 
Ngoja nikupe elimu kidogo kuhusu utajiri
Kwanza kuanzia Leo utambue hili, Mungu alipomuumba Adam na Eva aliwapa utajiri wote wa duniani na fahari zake wazimiliki, lakini walipohasi kwa Mungu kwa kumsikiliza shetani, utajiri wote wa duniani ukawa ni Mali ya shetani, wanadamu hatumiliki tena utajiri wa hapa duniani.
Sasa ili kuwa tajiri una options mbili tu
(1) umuombe shetani akupe sehemu ya utajiri anaomiliki, hii inawezekana kama ukikubaliana na masharti yake, na siku ukienda kinyume anakunyang'anya.
(2) umuombe Mungu akupe sehemu ya utajiri alioushikilia Shetani, na hii inawezekana kama utakuwa muombaji sana na mtakatifu haswa, kumyang'anya shetani sehemu ya utajiri wake si rahisi kihivyo.

Usijidanganye kama unaweza kuwa tajiri kwa kufuata seminar za motivation speaker peke yake, utajiri wote anao shetani, ni either uungane naye au upambane kumyang'anya.
Sad truth
 
W
Hujui chochote wewe na kama kukumbatia hiyo imani yako utaendelea kuwa masikini daima, labda nikuulize ulishawahi kufanya kazi na wachina wanaojenga barabara unajua nini huwa kinafanyika ili kukamilisha ujezi? Sasa wale hata hawafichi watoa kafara live bila chenga
Wachina wana nini naskia skia tu
 
Ngoja nikupe elimu kidogo kuhusu utajiri
Kwanza kuanzia Leo utambue hili, Mungu alipomuumba Adam na Eva aliwapa utajiri wote wa duniani na fahari zake wazimiliki, lakini walipohasi kwa Mungu kwa kumsikiliza shetani, utajiri wote wa duniani ukawa ni Mali ya shetani, wanadamu hatumiliki tena utajiri wa hapa duniani.
Sasa ili kuwa tajiri una options mbili tu
(1) umuombe shetani akupe sehemu ya utajiri anaomiliki, hii inawezekana kama ukikubaliana na masharti yake, na siku ukienda kinyume anakunyang'anya.
(2) umuombe Mungu akupe sehemu ya utajiri alioushikilia Shetani, na hii inawezekana kama utakuwa muombaji sana na mtakatifu haswa, kumyang'anya shetani sehemu ya utajiri wake si rahisi kihivyo.

Usijidanganye kama unaweza kuwa tajiri kwa kufuata seminar za motivation speaker peke yake, utajiri wote anao shetani, ni either uungane naye au upambane kumyang'anya.
Utajiri una siri nying sana ndani yake
 
Back
Top Bottom