S.M.P2503
Platinum Member
- Nov 25, 2008
- 3,689
- 7,145
Hilo litafanyika dakika za mwisho kwa hati ya dharura na uchaguzi utasogezwa mbele hadi kesi ya msingi iamuliwe... ndio maana ya No reform na election, wewe waache CCM wajimwambafai, lakini sarakasi za wanasheria wa Chadema zitakuja muda si mrefu...Vielelezo vyote vimewekwa wazi, na sasa ni dhahiri kabisa, kwa mujibu wa katiba ya CCM, kwamba ugombea wa kiti cha Urais wa Mh. Samiah Suluhu Hassan ni HARAM.
Sasa je, haiwezekani ‘Concerned members’ wa. CCM kwenda kuweka zuio la muda la ugombea wake hadi ule uharamu wake utakapoamuliwa na mahakama?
Itakuwa ni shangwe, vigeregere na vifijo kwa wana ccm wote waliotemwa kama uchaguzi utasimamishwa kwa hati ya dharura... hiyo ndio namna moja wapo ya kuuzuia uchaguzi... kesi itaenda hadi mahakama ya rufaa na inaweza chukua hadi miaka 4 kabla ya kusikilizwa...
Utakuwa ntanange mtamu sana huu ( Kama wa simba na Nyanga) ... wao wanawazuia wapinzani wao kwa kuwafungulia kesi za magumashi, na wapinzani wao pia watatumia mahakama hizo hizo kuuzuia uchaguzi, hivyo ngoma droo...