Je, ulifika Third floor(30s) bila kuwa na familia? Hali ilikuwaje?

Mkuu hapa naongelea kwa mwanamke na siyo mwanaume, kwenye jamii zetu mwanaume ndiye anayeamua ndoa na si mwanamke, sasa kama mwanaume labda ana wanawake watano halafu akaamua kuoa mmoja wanne akawaacha unategemea hao wafanye nini
Kadhalika nilichokiandika kinamgusa mpaka Mwanamke, sababu wapo Wanawake makini na Wana elimu ya kujua au kumjua mtu sahihi, na hawabahatishi. Kwani na wao wanaamua waolewe na nani
Hata sisi wake zetu waliamua waolewe na sisi. Bali wengine wapo walio ona au kumuona mtu sahihi, wakamfata au kuagiza mtu amfikishie ujumbe muhusika na ikawa.
 
Kwanini unaandika uongo ? Unajua Dunia ilipita katika kipindi cha mfumo jike ? Yaani mwanamke alikuwa na Wanaume wengi, wote akawa ana jamiiana nao, ilipofika wakati wa ujauzito na kujifungua, alikuwa anamchagua mwanaume mmoja katika wale alio kuwa anayo mwenye sifa bora luwazidi wenzie na kumpa mtoto. Unajua nini kilikuwa kinatokea baadae ?

Uhalisia unagusa jamii zote.
 
Wazi afande

Sent from my SM-G998B using JamiiForums mobile app
 
Kama mimi mzee nakomaa na ada ya dogo yupo chuo nikioa sitaweza mlipia.
 
Siyo kweli.

Mahusiano ni ya mwanamke yeye ndiye anaye ruhusu au kukataa.

Ni sawa na kusema mwanamke ni mwajili, mwanamme ni mwajiliwa.

Ulishawahi omba kazi sehemu ambayo hawajatangaza nafasi za kazi?

Tatizo lenu huwa mnajifanya innocent.

Hata kutongoza, anaye initiate ni mwanamke.

Suala la kuolewa anayetengeneza mazingira ya kuolewa ni mwanamke.

Behaviour na characters zako ndizo zitanifanya nikuoe au nikuteme. Na pia nyie huwa mnajua kabisa kubehave kulingana na mwanamme unaye date naye.

Acha kabisa kukimbia majukumu yenu, yaani uwe na tabia mbovu nikuache lawama unipe mimi?

Na naweza kuwa nao watano na nisioe hata mmoja kama wote wana tabia mbovu.
Mkuu hapa naongelea kwa mwanamke na siyo mwanaume, kwenye jamii zetu mwanaume ndiye anayeamua ndoa na si mwanamke, sasa kama mwanaume labda ana wanawake watano halafu akaamua kuoa mmoja wanne akawaacha unategemea hao wafanye nini
 
Namaanisha matendo yako ya maisha, isije kuwa huna huruma na watu walio kinyume na wewe..

Kuna Jamaa yetu hapendi mziki, Basi ana chukia watu wote wasio penda muziki.
Mkuu siyo kila ninachokijadili humu kuhusu mahusiano basi maana yake nakifanya au kimenitokea, mimi huwa sipendi watu wanaotukana wanawake wote kwa makosa ya baadhi, mbona sisi hatutukani wanaume wote kwa makosa ya baadhi na mbona ninyi hamkemeaneni makosa yenu
 
Wanaobishana na huyo hawamjui. Watakesha. Hiko kifaa.
Tunatofautiana wewe kama unaona ni sawa hizi nyuzi zinazoanzishwa kila siku za kudhalilisha wanawake wote mimi sioni hivyo, yani wanaume wakitukana wanawake it's okay ila wanawake tukijitetea ni kosa mara tuitwe feminists mara wabeijing mara vifaa, you can call us whatever you want but misogynism is one thing some of us can't tolerate in here
 
Ndio nikakuuliza kwa mfano mwanamke anataka kuolewa na mwanaume fulani ila huyo mwanaume hataki kumuoa huyo mwanamke anafanyaje hapo
 
Dah Eti wabeijing😆😂, sema misogynism sio kitu nzuri
 
Sasa kati ya mimi na wewe ni nani ameandika uongo niambie ni lini 'dunia nzima' ilipitia kwenye mfumo jike, wakati wote tunajua tangu dunia inaumbwa imekuwa katika mfumo dume (with the exception of some few inferior societies) hadi hivi sasa, halafu unajua hadi sasa hujajibu maswali yangu badala yake umeamua kutunga tu mada yako
 
Ndio maana niliuliza swali rahisi, kwamba je wanawake wote wenye tabia njema wanaolewa na wote wanaoachwa wana tabia mbovu, na je una uhakika walioolewa wote wana tabia njema tuanzie hapo
 
Ndio maana niliuliza swali rahisi, kwamba je wanawake wote wenye tabia njema wanaolewa na wote wanaoachwa wana tabia mbovu, na je una uhakika walioolewa wote wana tabia njema tuanzie hapo
Mi nadhani hiki kitu hakieleweki, maana kama wote walio olewa wana Tabia njema.
Tusinge ona Wanawake waki chepuka nje ya ndoa.

Lakini pia Kuna baadhi Hawaja olewa, Kutokana na tofauti tofauti.
👉Aidha wakati huja fika, au ni uchaguzi wao wa kipuuzi.
👉Kupotezewa muda na wanaume
 
Jadda wabeijing maana yake nini??
Kuna mkutano ulifanyika Beijing huko China uliokuwa unahusu women empowerment na gender equality, basi ndio wanaume wengi wa kiafrika mwanamke yeyote anayekemea makosa yao wanamuita mbeijing alias feminist sasa sijui hata kama wanaelewa maana yake, yani wanaume wengi wanataka wakitukana wanawake tuwaache tu tukijitetea basi ndio tutaishia kuoga kila aina ya ad hominem attacks kama hivyo badala ya kujadili hoja iliyoko mezani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…