Je, ulifika Third floor(30s) bila kuwa na familia? Hali ilikuwaje?

Je, ulifika Third floor(30s) bila kuwa na familia? Hali ilikuwaje?

Mkuu hapa naongelea kwa mwanamke na siyo mwanaume, kwenye jamii zetu mwanaume ndiye anayeamua ndoa na si mwanamke, sasa kama mwanaume labda ana wanawake watano halafu akaamua kuoa mmoja wanne akawaacha unategemea hao wafanye nini
Kadhalika nilichokiandika kinamgusa mpaka Mwanamke, sababu wapo Wanawake makini na Wana elimu ya kujua au kumjua mtu sahihi, na hawabahatishi. Kwani na wao wanaamua waolewe na nani
Hata sisi wake zetu waliamua waolewe na sisi. Bali wengine wapo walio ona au kumuona mtu sahihi, wakamfata au kuagiza mtu amfikishie ujumbe muhusika na ikawa.
 
Hivi unaposema mwanamke kuwa na wanaume wengi ni habari umamaanisha kwenye jamii gani na uhalisia upi, mbona kwenye jamii za wazungu mwanamke kuwa na wanaume wengi siyo habari na inaonekana kawaida tu, mkuu ninaposema madhara nataka unitajie madhara kwa wanawake wote duniani na siyo wa jamii fulani tu hapa naomba tujitahidi kuwa objective badala ya subjective
Kwanini unaandika uongo ? Unajua Dunia ilipita katika kipindi cha mfumo jike ? Yaani mwanamke alikuwa na Wanaume wengi, wote akawa ana jamiiana nao, ilipofika wakati wa ujauzito na kujifungua, alikuwa anamchagua mwanaume mmoja katika wale alio kuwa anayo mwenye sifa bora luwazidi wenzie na kumpa mtoto. Unajua nini kilikuwa kinatokea baadae ?

Uhalisia unagusa jamii zote.
 
Kuna kitu nahitaji kuwafunza mabinti ambao hawajafika 30.

Ukipata mpenzi ukamuona ana hofu ya Mungu, maisha yake yapo wazi hasa tabia zake, anakupenda kwa dhati, yupo tayari kukutambulisha kwa ndugu zake na kwa familia yake.

Yamkini asiwe na kipato kikubwa sana ila ana uwezo wa kufanya wote mle na mkalala, ISHI HAPO.

Acha tamaa za kutaka uolewe na mwanaume mwenye pesa, anayefanya kazi TRA, bandari, mfanyabiashara mkubwa, mwenye muonekano fulani n.k mwisho mtakuja kuangukia kwa wanaume za watu au kwa wanaume ambao wataishia kukuchezea. Kumbuka sehemu kubwa ya mwanaume mwenye pesa, ngono anachukulia starehe tu, kwahiyo atakuchukua na kukutumia baada ya kukutamani akijua anapiga na kupita zake.

Binti yangu, huyo mwanaume wa mtu unayemuona ana pesa, hazijaja tu hivi hivi, alianza chini kabisa kama huyo kijana ambae kwa sasa wewe unamdharau.

Kama umewahi kumnyanyasa kijana wa watu kisa masikini, yeye sijui hana umbo zuri n.k moyo wake ukaumia, katafute suluhu naye sababu huenda kuna mambo yako yakafunguka.

Mabinti sio kwamba mnakosa watu wa kuwaoa ila tamaa za maisha zimekuwa zikiwatesa wengi, (kumbuka Hawa alidanganywa kwa kutamani pale bustani ya edeni, mwanamke ukiishinda tamaa una sehemu kubwa sana ya kuishi maisha ya furaha duniani). Mnapenda smartphones, kila wiki msuke, utolewe out n.k mnaishi maisha ya udangaji kisa mna uzuri wa sura au mna matako makubwa, kwa bahati mbaya sana, ukishazoea kudanga, mwanaume yeyote atakujua tu, udangaji ni kama ngozi, HAIJIFICHI na hata ukijitahidi, mtu atasikia tu stori zako.

Sasa hivi kijana wa 30, 31, 32 ambapo kwa sehemu kubwa ndo vijana wengi walau kwa sehemu wanaanza kuona mwanga ktk eneo la uchumi hawezi kuwa na mwanamke wa 30, lazima atafute wa 24, 25 au 26 unless awe mpumbavu.

Girls kuweni makini sana na umri, uliowatupa kisa hawana ela, wakipata ela na wao watakuona wewe sio hadhi yao. Tafuta kijana mwezio mtakaopendana, mtie moyo ktk utafutaji, mpende sana na kumpa heshima hata pale ambapo anapungukiwa, mwanaume huyo hatokusahau.
Wazi afande

Sent from my SM-G998B using JamiiForums mobile app
 
Maisha maisha, ukiyaelewa maisha hutamuuliza mwenzio kwanini huna hiki, kwa nini huna kile. Kuna watu huwaona wenzao wenye umri sawa na wao kuwa wanamapungufu kwa kuwa hawajaolewa au kuoa. Kuna watu huwakejeli wenzao kwa kuwa hawana vile walivyo navyo wao hata kwenye uzi huu nimesoma comments nyingi za watu wa namna hio.

Ukijua kuwa tunatofautiana kimalezi na familiabtulizo toekea huwezi kumuona mwenzio mwenye hatia kisa hana kile ulicho nacho wewe. Kuna watu ni wabinafsi sana na kuna sisi ambao changu ni cha familia zetu tulizotokea. Kuna watu wana attack sana wenzao kisa hawajaoa wala kuolewa. Ila maisha ni fumbo kubwa sana.

Mimi ni me niko early 30s sijao na sina mtoto. Wapo watu hunishangaa kidogo kwanini sijaoa na ninaonekana kuwa na kauchumi japo kadogo. Ukiniona mimi sio mtu wa ku lialia njaa, ni yule mtu wa kuishi kulingana na kipato changu. Wasichokijua mimi nimeokea familia fukara sana, nyumba ya nyasi choo cha makuti cha kulenga. Nilipoanza kujitegemea niliapa kujenga nyumbani kwanza kisha nijenge kwangu ndio nioe.

Mungu akanisimamia, nilijenga home nikamaliza, nilirudi home tukapika pilau tukala tukazindua nyumba mama akachoma ndani japo ilikua haijaisha vizuri. Sasa nikaanza kujipambania mwenyewe kutimiza ndoto zangu. Bahati nzuri nilikua nimeshanunua viwanja viwili, nikaanza kujenga hekalu langu mdogo mdogo. Mama aliishi miaka mitano akafariki.

Nilipoenda kwenye msiba, baada ya kuzika nikaanza kuzurula. Nikaja kugundua vijana wenzangu wengi wameoa na wana familia ila hawakujenga kwao, sazazi wao bado wanaishi kwenye udongo na nyasi. Nikakumbuka maneno ya mama aliwahi niambia, "mwanangu iku ukioa sijui nitakua nakimbilia kwa nani" alimaanisha nikioa nitakua bize na familia yangu kama vijana wengine.

Ninachotaka kusema ni kuwa, kuna watu tunafukiria na wenzetu sio sisi pekee. Sasa namalizia hekalu langu niweke mtoto ndani. E MUNGU NISAIDIE.
Kama mimi mzee nakomaa na ada ya dogo yupo chuo nikioa sitaweza mlipia.
 
Siyo kweli.

Mahusiano ni ya mwanamke yeye ndiye anaye ruhusu au kukataa.

Ni sawa na kusema mwanamke ni mwajili, mwanamme ni mwajiliwa.

Ulishawahi omba kazi sehemu ambayo hawajatangaza nafasi za kazi?

Tatizo lenu huwa mnajifanya innocent.

Hata kutongoza, anaye initiate ni mwanamke.

Suala la kuolewa anayetengeneza mazingira ya kuolewa ni mwanamke.

Behaviour na characters zako ndizo zitanifanya nikuoe au nikuteme. Na pia nyie huwa mnajua kabisa kubehave kulingana na mwanamme unaye date naye.

Acha kabisa kukimbia majukumu yenu, yaani uwe na tabia mbovu nikuache lawama unipe mimi?

Na naweza kuwa nao watano na nisioe hata mmoja kama wote wana tabia mbovu.
Mkuu hapa naongelea kwa mwanamke na siyo mwanaume, kwenye jamii zetu mwanaume ndiye anayeamua ndoa na si mwanamke, sasa kama mwanaume labda ana wanawake watano halafu akaamua kuoa mmoja wanne akawaacha unategemea hao wafanye nini
 
Namaanisha matendo yako ya maisha, isije kuwa huna huruma na watu walio kinyume na wewe..

Kuna Jamaa yetu hapendi mziki, Basi ana chukia watu wote wasio penda muziki.
Mkuu siyo kila ninachokijadili humu kuhusu mahusiano basi maana yake nakifanya au kimenitokea, mimi huwa sipendi watu wanaotukana wanawake wote kwa makosa ya baadhi, mbona sisi hatutukani wanaume wote kwa makosa ya baadhi na mbona ninyi hamkemeaneni makosa yenu
 
Wanaobishana na huyo hawamjui. Watakesha. Hiko kifaa.
Tunatofautiana wewe kama unaona ni sawa hizi nyuzi zinazoanzishwa kila siku za kudhalilisha wanawake wote mimi sioni hivyo, yani wanaume wakitukana wanawake it's okay ila wanawake tukijitetea ni kosa mara tuitwe feminists mara wabeijing mara vifaa, you can call us whatever you want but misogynism is one thing some of us can't tolerate in here
 
Kadhalika nilichokiandika kinamgusa mpaka Mwanamke, sababu wapo Wanawake makini na Wana elimu ya kujua au kumjua mtu sahihi, na hawabahatishi. Kwani na wao wanaamua waolewe na nani
Hata sisi wake zetu waliamua waolewe na sisi. Bali wengine wapo walio ona au kumuona mtu sahihi, wakamfata au kuagiza mtu amfikishie ujumbe muhusika na ikawa.
Ndio nikakuuliza kwa mfano mwanamke anataka kuolewa na mwanaume fulani ila huyo mwanaume hataki kumuoa huyo mwanamke anafanyaje hapo
 
Tunatofautiana wewe kama unaona ni sawa hizi nyuzi zinazoanzishwa kila siku za kudhalilisha wanawake wote mimi sioni hivyo, yani wanaume wakitukana wanawake it's okay ila wanawake tukijitetea ni kosa mara tuitwe feminists mara wabeijing mara vifaa, you can call us whatever you want but misogynism is one thing some of us can't tolerate in here
Dah Eti wabeijing😆😂, sema misogynism sio kitu nzuri
 
Kwanini unaandika uongo ? Unajua Dunia ilipita katika kipindi cha mfumo jike ? Yaani mwanamke alikuwa na Wanaume wengi, wote akawa ana jamiiana nao, ilipofika wakati wa ujauzito na kujifungua, alikuwa anamchagua mwanaume mmoja katika wale alio kuwa anayo mwenye sifa bora luwazidi wenzie na kumpa mtoto. Unajua nini kilikuwa kinatokea baadae ?

Uhalisia unagusa jamii zote.
Sasa kati ya mimi na wewe ni nani ameandika uongo niambie ni lini 'dunia nzima' ilipitia kwenye mfumo jike, wakati wote tunajua tangu dunia inaumbwa imekuwa katika mfumo dume (with the exception of some few inferior societies) hadi hivi sasa, halafu unajua hadi sasa hujajibu maswali yangu badala yake umeamua kutunga tu mada yako
 
Siyo kweli.

Mahusiano ni ya mwanamke yeye ndiye anaye ruhusu au kukataa.

Ni sawa na kusema mwanamke ni mwajili, mwanamme ni mwajiliwa.

Ulishawahi omba kazi sehemu ambayo hawajatangaza nafasi za kazi?

Tatizo lenu huwa mnajifanya innocent.

Hata kutongoza, anaye initiate ni mwanamke.

Suala la kuolewa anayetengeneza mazingira ya kuolewa ni mwanamke.

Behaviour na characters zako ndizo zitanifanya nikuoe au nikuteme. Na pia nyie huwa mnajua kabisa kubehave kulingana na mwanamme unaye date naye.

Acha kabisa kukimbia majukumu yenu, yaani uwe na tabia mbovu nikuache lawama unipe mimi?

Na naweza kuwa nao watano na nisioe hata mmoja kama wote wana tabia mbovu.
Ndio maana niliuliza swali rahisi, kwamba je wanawake wote wenye tabia njema wanaolewa na wote wanaoachwa wana tabia mbovu, na je una uhakika walioolewa wote wana tabia njema tuanzie hapo
 
Ndio maana niliuliza swali rahisi, kwamba je wanawake wote wenye tabia njema wanaolewa na wote wanaoachwa wana tabia mbovu, na je una uhakika walioolewa wote wana tabia njema tuanzie hapo
Mi nadhani hiki kitu hakieleweki, maana kama wote walio olewa wana Tabia njema.
Tusinge ona Wanawake waki chepuka nje ya ndoa.

Lakini pia Kuna baadhi Hawaja olewa, Kutokana na tofauti tofauti.
👉Aidha wakati huja fika, au ni uchaguzi wao wa kipuuzi.
👉Kupotezewa muda na wanaume
 
Jadda wabeijing maana yake nini??
Kuna mkutano ulifanyika Beijing huko China uliokuwa unahusu women empowerment na gender equality, basi ndio wanaume wengi wa kiafrika mwanamke yeyote anayekemea makosa yao wanamuita mbeijing alias feminist sasa sijui hata kama wanaelewa maana yake, yani wanaume wengi wanataka wakitukana wanawake tuwaache tu tukijitetea basi ndio tutaishia kuoga kila aina ya ad hominem attacks kama hivyo badala ya kujadili hoja iliyoko mezani
 
Back
Top Bottom