Na kwanini ionekane kama jamii kuharibika ni makosa ya wanawake na si matatizo ya wanaume kushindwa kuendana na hali halisi ya ulimwengu wa sasa, sikia bro hizo enzi za bibi zetu zilishapita na hakuna mwanamke ambaye atakuwa tayari kurudi huko hata dunia ibadili mzunguko wake, na nadhani hali halisi ya tunakoelekea umeshaanza kuiona wanawake wengi siku hizi hawajali tena kuhusu mitazamo ya jamii wanajali furaha yao kwanza
Kadiri mnavyozidi kuwatandika viboko ndivyo nao wanavyozidi kutafuta namna ya kuwa masugu ili visiwaumize na siyo kutafuta namna ya kuvikwepa, and trust me ikifikia hiyo hatua wanawake wote wakawa masugu basi wanaume mtashuhudia the worst era tangu dunia iumbwe, wanawake wameshachoka wao kutakiwa kusacrifice furaha yao kila siku kwa ajili ya wanaume kama mnaona ni rahisi anzeni ninyi kusacrifice furaha yenu halafu mje hapa tuongee lugha moja
So kilichobaki hapa ni either ninyi wenyewe wanaume ndio muanze kubadilika mkubali kucompromise au muendelee kulalamika hadi mwisho wa dahari, lakini wanawake hawatakubali tena kuendelea kuburuzwa na kuwa watumwa in the name of maadili sijui ustawi wa jamii hilo ni jukumu la jinsia zote, kama ninyi ndio mnaumizwa sana na uharibifu wa jamii basi tunategemea ninyi ndio muanze kubadilika siyo tena mzigo wote muwasukumizie wanawake tu