Binadamu huwa hatukomi...nakumbuka nilishawahi kutoa haibu zilizonipata siku za nyuma katika hii thread. Cha kushangaza, mwezi uliopita tu nilishikwa na haibu nyingine ya mwaka. Kuna mdada mmoja anamiliki saluni pale mtaani kwetu, huyu mdada nilihisi tunapendana ama mimi tu nilijichanganya mwenyewe. Maana kila tukionana alikuwa na tabasamu za hajabu kiasi kwamba nilishindwa kujizuia kusimama na kumsalimia, yaani ana heshima ya hajabu kwangu na mchangamfu mno kana kwamba tuna mazoea fulani hivi kumbe hakuna kitu. Mdada anaridhisha kwa sura ila tabia zake ndizo zilinichanganya mpaka nikaanza kumfuatilia. Siku ya siku nikamfungia safari kwa saluni yake na bahati nzuri nilimkuta. Nikasimama na kuingia mle ndani kumsalimia na kumtongoza/kumpa hisia zangu kwake. Mdada alikuwa kasimama kwenye counter huku akiangalia nitokapo, yaani mlangoni. Namtongoza na kumwambia jinsi ninavyojisikia nikimuona, naona mdada ananikodolea mimacho na kushikwa na ganzi kana kwamba yale maneno yanamchanganya akili. Kidogo naona mtu (mwingine) ananyanyuka kutoka chini ya counter. Nilipatwa na kigugumizi hata kukimbia nilishindwa maana yule mtu mwingine alikuwa ni rafiki wa wife wangu pale mtaani. Yule demu akanitambulisha kuwa yule ni wifi yake, nami kwa unyonge nikasalimia mke wa rafiki yangu kama vile nimekimbiwa na mke wangu, yaani kwa unyonge wa hajabu. Yaani nilikuwa mpole karibia wiki mbili na sikuwa na hamu kabisa na yule rafiki wa mke wangu. Uzuri ni kwamba, naye alikuwa na busara kwani baada ya hizo wiki mbili tulikutana kanisani na akaniambia nisiwe na wasiwasi, tufanye hajasikia chochote ila alimkanya tu wifi yake juu ya lile tukio. Jamani kina Mama mnatuchanganya wenzenu mpaka tunakosa heshima mitaani.