Je, ulishawahi kuaibika katika mazingira mabaya?

Je, ulishawahi kuaibika katika mazingira mabaya?

mhhhh kidogo nikatwe miguu na lift za ngazi pale Mayfair/shopaza. kumbe unatakiwa uwahi kutoa miguu sasa Mimi nilidhani itasimama then nishuke.kulikua na watu kadhaa na nilitaka kuanguka.yaan niliona aibu na mpaka Leo naogopa lift za ngazi
kituko kingine wakati naenda kuchukua admission letter Udsm si niliposikia kituo mlimani nikashuka kumbe ni m/city.kwenda ndani naona maduka tuu hamna dalili ya chuo ikabidi niulize Askari.sasa huyo Askari sio kunielekeza kwa nguvu jamani watu wanapita wanasikia.ikabidi nitoke nje km nilivyoelekezwa.yaan niliona aibu
[emoji23]pole
 
Yaani hauna hata miezi 3 ila kasumbufuuuu.. tutakugawa insta sasa hivi wewe na aunt yako
[emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12]
Lkn babu unanionea kwani mm nimefanyaje????

Cc:espy
 
Nikiwa safarini kwenda Brunei nilishuka nchi moja ya kiarabu. I had a job ya miezi 2 pale. Sasa wadada wa nchi ile hupati hata wa kujituliza. Pale kulikuwa na sheria kali na I was limited in my moves. Sasa siku moja nikapata ka trip kwa hotel moja ilikuwa na Casino na lot of wadadas. Ile naingia tu nikakutana na waarabu wawili wapo watupu wakaja kunikarimu just kunikaribisha, nilihisi mwili unazimia mbele kidogo nikaona balaa jipya, dish likayumba kabisaaa.....nikastuliwa na mlinzi akiniambia Mr your trousers is making mountan!!!
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
aisee mi sitasahau 2010 kipindi nipo form 6 pale jitegemee. nilikua sikai hostel za ndani ila nna washkaji zangu mle, basi nilikua na ki'ipod naendaga nacho kina miziki na mapichapicha ya kina beyonce. siku 1 nikamwachia jamaa wa hostel aling'ang'ania alale nacho, basi bwana jamaa si akadakwa nacho sijui na afande gan huko! kubananishwa akanitaja mimi! kesho yake ticha wa darasa kanipa barua kumuita mzazi dahh! kesi ikafika hadi kwa mwl mkuu msaidiz(nimesahau jina), nikaambiwa nisubiri nje mama akaingia ofisini. badae nikaitwa ndani huku najua kesi ya kawaida tu. mara naambiwa kosa lako ni kusambaza picha za ngono shuleni!! na nitaje wenzangu tunaoshirikiana kuharibu watoto wa hostel!! kusema ukweli kile kidude kilikua na picha za kawaida tu za wasanii. basi kesho yake ilikua alhamis nikaitwa mbele pale assemble,njuka hadi form6 wote wapo wananikodolea hadi demu wangu na rafike zake dahh! nikatangazwa eti mimi ndo saplaya mkubwa wa picha za uchi! nikabamizwa mbata 4 mubashara na discipline master (ndiamkama). halafu eti nikapewa mic ni'confess dahh! nikatoa wosia huku nna hasira kilo 100!! yule ticha (ndiamkama) alivyo mkuda sasa, nimemaliza kuongea akanisukumizia bonge la kofi mgongoni eti "nenda nikukute ofisini kwangu"...nikatoka nduki km hamorapa. huko nyuma nasikia wanafunzi wanacheka kwikwikwi!!
dahh siwezi kuisahau siku ile! kibaya zaidi demu wangu alikuja kunipa pole class dahh niliona noma nikataman niache shule!! kantini ndio ilikua balaa yani acha tu!!
 
Ukifika unauliza chai bei gani? Wali nyama bei gani? Japo ushamba
sawa mkuuu ushamba nao tatizo .....mfano uko na manziii unafanyaje na we unataka kujifanya kibosile mapesa[emoji27] [emoji27] [emoji27]
 
Asante mpendwa yaan ni aibu, halafu mi sipendi ukimuuliza mtu akuelekeze bas atakuelekeza kwa nguvu dah na mikono yote na mwili wote unakuelekeza jamani

Pole Sana Mtoto Mzuri [HASHTAG]#MNANSO[/HASHTAG]
 
Nakumbuka primary darasa la 5 huko unyakyusani kwa bibi yangu kyela vijijini. Shule nzima tulikua tunaongea kinyakyusa ikabidi waanzishe kampeni ya kuzuia matumizi ya kinyakyusa shuleni. Walitengeneza ubao ambao mwanafunz ukiongea kinyaki unavalishwa na viboko juu, hali ikawa ngumu sana kwetu tusiojua kiswahili vizuri.

Kuna siku nilipiga chafya ya kinyakyusa darasani (ejooo) hata haikuisha vizuri mtu huyo hapa na ubao wa kunivalisha shingoni, japo nilibisha bila mafanikio.
Hatari sanaaaaa
 
Binadamu huwa hatukomi...nakumbuka nilishawahi kutoa haibu zilizonipata siku za nyuma katika hii thread. Cha kushangaza, mwezi uliopita tu nilishikwa na haibu nyingine ya mwaka. Kuna mdada mmoja anamiliki saluni pale mtaani kwetu, huyu mdada nilihisi tunapendana ama mimi tu nilijichanganya mwenyewe. Maana kila tukionana alikuwa na tabasamu za hajabu kiasi kwamba nilishindwa kujizuia kusimama na kumsalimia, yaani ana heshima ya hajabu kwangu na mchangamfu mno kana kwamba tuna mazoea fulani hivi kumbe hakuna kitu. Mdada anaridhisha kwa sura ila tabia zake ndizo zilinichanganya mpaka nikaanza kumfuatilia. Siku ya siku nikamfungia safari kwa saluni yake na bahati nzuri nilimkuta. Nikasimama na kuingia mle ndani kumsalimia na kumtongoza/kumpa hisia zangu kwake. Mdada alikuwa kasimama kwenye counter huku akiangalia nitokapo, yaani mlangoni. Namtongoza na kumwambia jinsi ninavyojisikia nikimuona, naona mdada ananikodolea mimacho na kushikwa na ganzi kana kwamba yale maneno yanamchanganya akili. Kidogo naona mtu (mwingine) ananyanyuka kutoka chini ya counter. Nilipatwa na kigugumizi hata kukimbia nilishindwa maana yule mtu mwingine alikuwa ni rafiki wa wife wangu pale mtaani. Yule demu akanitambulisha kuwa yule ni wifi yake, nami kwa unyonge nikasalimia mke wa rafiki yangu kama vile nimekimbiwa na mke wangu, yaani kwa unyonge wa hajabu. Yaani nilikuwa mpole karibia wiki mbili na sikuwa na hamu kabisa na yule rafiki wa mke wangu. Uzuri ni kwamba, naye alikuwa na busara kwani baada ya hizo wiki mbili tulikutana kanisani na akaniambia nisiwe na wasiwasi, tufanye hajasikia chochote ila alimkanya tu wifi yake juu ya lile tukio. Jamani kina Mama mnatuchanganya wenzenu mpaka tunakosa heshima mitaani.
 
Niliwahi kwenda na rafiki yangu kwa ndugu zake ilikuwa Area c Dodoma sasa kumbe rafiki yangu alikuwa amebanwa tukapiga hodi tukakaribishwa wenyeji tukawakuta sebuleni.Rafiki yangu alisalimia na haraka haraka akaendelelea na safari ya kwenda chooni mie nami nikachanganya supu namfuata mwenyeji akauliza na wewe unakwenda wapi? mwenzio anaenda chooni! nilipata aibu ya mwaka nikakoma kufuatafuata watu.
Hahahahahahah
 
Back
Top Bottom