Je, ulishawahi kuaibika katika mazingira mabaya?

Siku moja natoka zangu bush naelekea town na tu kandambili twangu , sasa nilipofika centre ya Town yenyewe, kutokana na kushanga shanga midoli iliyo kaah kama watu bahati mbaya nikajikwa, ebwana wee kandambili moja ikakatika, ikawa hakuna namna, na tuhela twangu niliokuwa nimeuza kuku nikawa nimeweka M-pesa, bas ikabidi nianze kutembea Kandambili moja mkononi na moja mguuni mpaka nilipo ipata kituo cha kutolea na kuanza kutafuta fundi anishonee.

Yani ilikuwa igizo si igizo.
 
Rai don't you believe kuna hotel za bei hiyo bongo??
Oasis ya morogoro navyoongea now kahawa 1 cup ni 4500. Na ni hotel ya kawaida saana kwa wanaoifahamu...
hahahahah umenikumbusha tulienda sehem fulani kula piza na mchizi wangu,Pizza mbili.mishikikaki na juice zetu jioni ikawa imeisha tukaomba bili......tobaaaaa kitu kikasoma 49500. Hahahaha. Mkononi kuna hamsini likabaki jero,wacha tuukanyage kurudi majumbani.....hahahahaha........
 
Huu Uzi bwana! kila nikiupitia huwa nacheka mpaka machozi yananitoka .....lol
 
Yaan sitaki hata kukumbuka nilivyo aibika lol[emoji18]
 
Ha haaa haaaaa aisee! ahsante kwa kuniongezea siku nimecheka sana aisee
 
Hehehe na hao masela wako wangekua ndo wanamuamkia huyo manzi basi usingeshindwa kumuamkia ukaitikia mwenyewe and i bet ulikua umekaa pale kwenye mapultable mengi mashine3

form1
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€......Dah,NOMA SANA AISEE!
 
.
Naufufua tena huu uzi
 
Me niliwah kugombania daladala yan ule mbanano na mvutano wa mlangoni mpaka nafika kwenye siti vifungo vya blauzi vyote vimetatuka brazia hii hapa
Daaar Maskin pole ,hapa nmevuta taswira nkaona kabsa ulivyokua ,pole sana mpendwa
 
hahahaha, sijui kama hii inastahili kuitwa ushamba, ila ni aibu iliyotokana na ukauzu.

likizo moja ya advance tulirudi home na tukajikuta classmates wa o level tuko mtaani. basi matembezi ya mida kama saa 8 mchana, mob kama ya watu wa4 tukasema tupite kwa classmate wetu pia aitwa clara(sio jina lake halisi). bahati nzuri au mbaya na mama clara pia alikuwepo. haya yalikuwa mazungumzo yetu.

mama clara: karibuni wanangu, hamjambo?
sisi: hatujambo mama shikamoo?
mama clara; marhaba, mmekuta tumemaliza kula ngojeni niwaandalie.
baadhi yetu; Usijari mama tumeshakula.

basi zikaendelea mazungumzo ya hapa na pale, sisi na clara, baadae mama clara nae katujoin ili kuzisikia habari za boarding na advance (maana tuliosoma advance na kuishi wilayani 'nyakati hizo' ilikuwa ni respect of some kind mtaani na kwenye familia).

Ghafla katika hali isiyotarajiwa mwenzetu mmoja aitwaye Patrick akasonya na kusema, 'Mama mimi nikuambie tu ukweli, mchana hatujala na tunanjaa mno'. hahahha. tulipigwa butwaa ila msela kakaza sura, nakisha kutuuliza kwani nyie mmekula.

kwakweli kwao clara palikua 'ushuani' sana na mama clara alikua na 'ulokole fulani'. pale pale mama akasema ngojeni niwaandalie chakula wanangu. ilibidi mama achambue mchele atupikie lunch.. msosi tulikula lakini hali ya kichwani haikua sawa kutokana na fedheha niliyoifeel.. ila 'msela' Patrick kigumu yeye akapiga sahani mbili kabisa. tumetoka hapo njiani sikutaka hata kumsemesha. πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Me niliwah kugombania daladala yan ule mbanano na mvutano wa mlangoni mpaka nafika kwenye siti vifungo vya blauzi vyote vimetatuka brazia hii hapa
Nimecheka kwa sauti[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Hahaha aisee unanikumbusha mbali sna

Nilienda town one day na jinsi yangu nyeupe yaani Nimefunga pamba fresh

Si nije kuteleza ktk mtaro wa maji taka yaani jinsi yote na flana full maji taka na mfkoni sna ata hela ya kununua nguo zengine na home sio karibu

Daah ilinibidi nipige boda to boda la mitaa kwa mitaa yaan nilizunguka ili nijifiche wachizi na watoto wakali wanaonijua wasije kuniona

Ilikua balaa hadi nafika home
 
Noma sana aisee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…