Je, ulishawahi kuaibika katika mazingira mabaya?

Dah.. Mmenikimbusha mwaka 2006 nikiwa form 3 kaingia ticha wa hesabu kashusha example za kutosha akauliza mmeelewa.. Darasa zima tukaitikia tumeelewa wakati huo sijaelewa chochote...

Ticha akatoa swali akanichagua nifanye mimi.. Kufika ubaoni sijui hata cha kuandika nikasingizia chaki ndogo nikapewa chaki mpya mara ubao ukajaa jasho kama lote maana nilikuwa naandika vitu vya ajabu afu nafuta

Aisee sio kwa jasho lile ticha akauliza mbona unapaka maji ubaoni mtu mzima sina la kujibu

Ilikuwa aibu ya millenia maana class wanajua jamaa mwamba ..nikaambiwa nenda ukakae ilibidi nizime na vitamba vya kujifutia
 
Hahaha!!! Raha ya sigara ujiachie
 
We jamaa umeniacha hoi sana
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] dah
 
Eti lipia mdogo angu tukufungie [emoji23] [emoji23]
 
Hahhaa
 
Wakati huo nilikuwa form one nimekuja mjini 'daslam' kumsalimia mpwa wangu aliyekuwa anaishi kota za udsm geti maji. kimbembe kwenda chooni nikakuta vyoo ni vile vya kukaa bwana, hapo sijawahi kuvitumia hata mara moja maishani mwangu nikaona isiwe tabu nikaenda zangu kumaliza shida zangu msikiti wa chuo cha maji ule njia ya msewe.

Nilikuwa naomba likizo iishe kusema kweli nirudi zangu mkoani maana mwezi mzima nilikuwa nashusha 'kubwa zangu' msikitiniiiii ambako nilihisi nitakua comfortable.
 
Nakumbuka iyo siku nimetoka kukoga na futa geto limeisha ikabidi nivae suruali fasta nifate mafuta duka lilipo jirani na nipoishi,nikavaa na kuchomoka haraka nilipofika dukan nikakosa mafuta niliyokuwa nahitaj nikazingunga kama maduka3 hivi yalipo mbali kidg nikapata duka moja wapo sasa ile narud tu home ile nataka fungua kifungo cha suruali kujicheki maeneo ya zipu kupo wazi na jimuwa linaonekana kabisa live bila chenga,nikakumbuka kuna baadhi ya maduka niliyopita kuna kinadada walikuwa wakiangua vicheko pacpo mimi kujua nn kiliwafurasha.....OGOPA SANA KUSAHAU KUFUNGA KUFULI.
 
Na afazali waone mwili wa dushe na sio kichwa cha dushe
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Siku moja nilianguka darasani wanafunzi walicheka sana badala ya kunipa pole,na nilikuwa sister du balaa,nilibinuka skert ikanifunika kichwa ilikuwa charanga.
wakaona yaliyomo?
 
Kumbe ndio wewe mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…