Je, ulishawahi kuaibika katika mazingira mabaya?

Je, ulishawahi kuaibika katika mazingira mabaya?

Dah.. Mmenikimbusha mwaka 2006 nikiwa form 3 kaingia ticha wa hesabu kashusha example za kutosha akauliza mmeelewa.. Darasa zima tukaitikia tumeelewa wakati huo sijaelewa chochote...

Ticha akatoa swali akanichagua nifanye mimi.. Kufika ubaoni sijui hata cha kuandika nikasingizia chaki ndogo nikapewa chaki mpya mara ubao ukajaa jasho kama lote maana nilikuwa naandika vitu vya ajabu afu nafuta

Aisee sio kwa jasho lile ticha akauliza mbona unapaka maji ubaoni mtu mzima sina la kujibu

Ilikuwa aibu ya millenia maana class wanajua jamaa mwamba ..nikaambiwa nenda ukakae ilibidi nizime na vitamba vya kujifutia
 
Nakumbuka siku moja navuta sigara kwa siri siri nikavuta ndefu moja mara mbele uso kwa uso na shangazi yangu nikaubana ule moshi alf sigara nikaizimia mfukoni ile kunisemesha tu nkakosa cha kufanya kuongea moshi wote nje aibu kubwa sana alf wakijua hom msala
Nilitimua mbio hizo ili nisiulizwe maswali
Mashtaka yalipo fika nilikana hatari nkasema nilkua na jamaa nmekutana nae rafk ndo alkua anavuta sitokaa nisahau
Hahaha!!! Raha ya sigara ujiachie
 
siku moja nikiwa china tumeenda shopping nikawakimbia masela , nikaingia kwenye mall moja kubwa sana nikapanda lift huyo hadi maduka ya ghorofani... nimemaliza shopping nikapotea na nisijue pa kutokea na huku nje jamaa wananitafuta kuona hawanipati wakatoa taarifa polisi then wale polisi wakawataarifu wenzao waliomo ndani ya ile mall kuwa wakiona black man wam'escort to the exit. Kimbembe kimekuja hapa sasa, askari alivoniona akawa anakuja na mm nikaanza kumkimbia aisee tulitimuana mle ndani sitakaa nisahau. Mpaka nimechoka jamaa akanipeleka kwa masela huku nimepata aibu ya karne
We jamaa umeniacha hoi sana
 
Kuna siku tukiwa sehemu moja yenye mandhari nzuri nilimuona babe wa ukweli kila sifa anayo ,mtu mzima nikajikaza kisabuni nikaenda kumtongoza alikuwa na besti zake 2

Ile nampiga sound nikapiga chafya ase makamasi yakanitapakaa mashavuni,puani halafu nilikuwa sina leso . aibu ya karne niliipata sina haja ya kuendelea kilichofuata


Siku nyingine namtongoza demu Fulani hivi tukiwa kwenye katikati ya kumshawishi ushuzi ukanitoka dah usiombe wakuu nilitoka nduki

Utatamani ardhi ipasuke uingie
[emoji23] [emoji23] [emoji23] dah
 
Likizo ya mwezi wa sita form three mzee alinipa kazi ya kulipia mambo yake TRA, kama mnavyokumbuka mwanzoni mwa 2000's kulipia TRA ilikuwa na milolongo mingi sana mtu ukiwa bize unaweza ukazira. Kwa hiyo mzee alinipa ya usumbufu pamoja na rushwa.
Basi nilipomaliza kila kitu nikawa nimebaki na chenji ya kutosha kabisa. Siku hiyo nimetoka TRA narudi hom, njiani nimekutana na classmate nammezeaga mate sana nikasema leo nina nyenzo nang'oa huyu mtoto.
Tukasalimiana nikamkaribisha kwenye hoteli jirani hapo tule lunch wala hakuvunga. Msosi ukaletwa chips kuku nusu mara mbili bonge la advataizi, niksona hapa ndo wakati wa kuchomekea kama JPM. Ile sijamaliza hata mistari yangu mtoto akasimama kwa hasira akaanza kunifokea kwa sauti kali sana. Hapo meza zote zimejaa wafanyakazi wamekuja lunch wote wamegeuka wanashangaa hawa watoto vipi! Mimi hata cha kujibu sina mate yamekauka. Nakumbuka maneno machache tu "yani vichipsi vyako ndo unitongoze?" mengine sikusikia kwa kweli. Akaondoka zake mimi sielewi cha kufanya, akaja dada mmoja mhudumu na mfuko akaniambia lipia mdogo wangu tukufungie.
Sikutongoza tena hadi form five na huyo huyo akawa girlfriend wangu wa kwanza.
Eti lipia mdogo angu tukufungie [emoji23] [emoji23]
 
Ngoja nicheke Kwanza kabla cjasema YA kwangu


Kipindi hicho Nilikuwa form pale makongo.
Nilikuwa naumwa mafua ambayo yanaelekea kupona wakati huo ukipiga chafya basi yanatoka makamasi mazito, tukiwa darasani tukifundishwa physics na Afande mataula basi nikapiga chafya YA ghafla baada YA kumaliza hiyo chafya USO Mzima ulijaa kamasi zile nzito Halafu mfukoni hata kitambaa sina, Yaani darasa zima wakawa waniangalia mm kucheka wanataka Lkn wanamuogopa teacher basi nilitoka nduki hadi bombani kunawa Kisha nikaelekea kantini kununua kitambaa nikasuburi mapumziko nikamuomba rafiki yangu aniletee begi langu nikasepa zangu hom sikuenda shule Wiki nzima kwa aibu.
Hahhaa
 
Wakati huo nilikuwa form one nimekuja mjini 'daslam' kumsalimia mpwa wangu aliyekuwa anaishi kota za udsm geti maji. kimbembe kwenda chooni nikakuta vyoo ni vile vya kukaa bwana, hapo sijawahi kuvitumia hata mara moja maishani mwangu nikaona isiwe tabu nikaenda zangu kumaliza shida zangu msikiti wa chuo cha maji ule njia ya msewe.

Nilikuwa naomba likizo iishe kusema kweli nirudi zangu mkoani maana mwezi mzima nilikuwa nashusha 'kubwa zangu' msikitiniiiii ambako nilihisi nitakua comfortable.
 
Nakumbuka iyo siku nimetoka kukoga na futa geto limeisha ikabidi nivae suruali fasta nifate mafuta duka lilipo jirani na nipoishi,nikavaa na kuchomoka haraka nilipofika dukan nikakosa mafuta niliyokuwa nahitaj nikazingunga kama maduka3 hivi yalipo mbali kidg nikapata duka moja wapo sasa ile narud tu home ile nataka fungua kifungo cha suruali kujicheki maeneo ya zipu kupo wazi na jimuwa linaonekana kabisa live bila chenga,nikakumbuka kuna baadhi ya maduka niliyopita kuna kinadada walikuwa wakiangua vicheko pacpo mimi kujua nn kiliwafurasha.....OGOPA SANA KUSAHAU KUFUNGA KUFULI.
 
Nakumbuka iyo siku nimetoka kukoga na futa geto limeisha ikabidi nivae suruali fasta nifate mafuta duka lilipo jirani na nipoishi,nikavaa na kuchomoka haraka nilipofika dukan nikakosa mafuta niliyokuwa nahitaj nikazingunga kama maduka3 hivi yalipo mbali kidg nikapata duka moja wapo sasa ile narud tu home ile nataka fungua kifungo cha suruali kujicheki maeneo ya zipu kupo wazi na jimuwa linaonekana kabisa live bila chenga,nikakumbuka kuna baadhi ya maduka niliyopita kuna kinadada walikuwa wakiangua vicheko pacpo mimi kujua nn kiliwafurasha.....OGOPA SANA KUSAHAU KUFUNGA KUFULI.
Na afazali waone mwili wa dushe na sio kichwa cha dushe
 
kuna binti aliagiza mabia bar kwa kunikomoa .sasa mfukoni nikawa na buku ten tu bill ikaletwa kama 35 elfu.enzi hizo ni ela mingi. nikavizia kaenda toilet nichukue handbag yake nichomoe ela tushare pamoja bill.akanifuma naingiza mkono kwenye mkoba.nilipata aibu ya mwaka.nafwaaa
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Siku moja nilianguka darasani wanafunzi walicheka sana badala ya kunipa pole,na nilikuwa sister du balaa,nilibinuka skert ikanifunika kichwa ilikuwa charanga.
wakaona yaliyomo?
 
Haha ikabidi tu utoe hela mwee. Umenikumbusha story ya kimini

Kuna siku nilikuwa darasa la 5 au 6 hivi, nikawa napita mitaa ya sokoni. Nimevaa kakimini kangu ka kuchanua, najishaua tu. Basi bana kuna kichaa fulani hivi, akaninyatia kwa nyuma huyoo akanifunua mwaaaaaa, jamani nashukuru nilivaa teitei. Miguu ilistuck jamani, I felt so embarrassed khaa
Kumbe ndio wewe mkuu
 
Back
Top Bottom