Je, ulishawahi kuaibika katika mazingira mabaya?

Je, ulishawahi kuaibika katika mazingira mabaya?

Mimi nakumbuka kuna siku nipo darasa la saba naendesha baiskeri phonex yale makubwa sasa nilikuwa nimevaa suluar pana chini ile nimefika kilabuni nataka kushuka tu ule mguu wa kushukia suluari ikajishika sehemu ya kuwekea pampu ya kujazia upepo ,nikaanguka chini ilikuwa aibu nainuka nikachukua baiskeli nikasepa watu walikuwepo lakin sikuwaona watu kwa aibub
Hahaha aseeh hizi aibu zenu ni za karne [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Duh, mie nakumbuka kipindi hicho nipo na watasha sasa nikawa natakiwa ni present nilivyofika kwenye FAQs, mie niliwatukana kwa ku spell https://jamii.app/JFUserGuide...sema kuna mdada kwa sasa yupo boston ndo alinisaidia kuitamka kwa kirefu.
 
siku moja nikiwa china tumeenda shopping nikawakimbia masela , nikaingia kwenye mall moja kubwa sana nikapanda lift huyo hadi maduka ya ghorofani... nimemaliza shopping nikapotea na nisijue pa kutokea na huku nje jamaa wananitafuta kuona hawanipati wakatoa taarifa polisi then wale polisi wakawataarifu wenzao waliomo ndani ya ile mall kuwa wakiona black man wam'escort to the exit. Kimbembe kimekuja hapa sasa, askari alivoniona akawa anakuja na mm nikaanza kumkimbia aisee tulitimuana mle ndani sitakaa nisahau. Mpaka nimechoka jamaa akanipeleka kwa masela huku nimepata aibu ya karne
Hahahaaaaaa dahhh nimecheka hadi watu wananishangaaa...

Nawaambia ni jf maana wenyewe wanadhani humu ni siasa tuu...

Ahsante kwa kunipunguzia stress
 
Mimi nakumbuka nipo chuo Iringa wakati wa group presentations si unajua tena ushapiga jumba lako jeusi ili uongezee marks walau, sasa shughul ikawa tunataka kupanda group zima stejini lecturer akasema no need apande tuu mmoja...straight akanipoint mimi na hata kazi nlikua siijui inafananaje 🙂
Macho yalinitoka na lisuti lako kijasho kwa mbali..basi ile hofu kupanda stejin nikaikosa ngazi nlibiringita hadi chiniiii..kuficha aibu wallah sikuinuka nkajifanya kuzimia!!!
...that was my embarrassing moment ever
 
Hahaha...pole mkuu hukuwa na demu class
 
Nakumbuka nikiwa darasa la 4 kipindi cha mwisho kabla ya mapumziko ya saa nne nimebanwa na mkojo hatari, kwenda kuomba ruhusa lazima useme kwa kingereza maana ilkua kipindi chake,
Uvumilivu ukanishinda nkatoka kwenda kwa mwalimu kuomba ruhusa, sasa lugha inanipiga chenga nkasema kwa kiswahili akanichapa fimbo mguuni akitaka niseme kingereza nikajikuta nimeumwaga palepale kiasi, nkatoka nduki sikurudi tena darasani nikaenda kujificha vichakani hadi kaptula ikauke maana ilkua ya kaki huko njiani wangeniona,
Na nilikua na demu darasani ambae ni binamu yangu, asubuhi nampitia tuende shule akanicheka huku akisema hanipi tena nkamtandika vibao akasema kwa shangazi yake sababu ya kumpiga nikajiongezea tena aibu kwa wajomba wakajua nilijikojolea shuleni.
 
Namshangaa Raimundo mkuu.. may be akiingia hotelin anakunywa juice...
Pale natron palace 2015 one cup nililipa 5800 kwa naura..kilimanjaro..Serena..east africa(wamebadili jina silikumbuki) ngurudoto sijui bei zake

Mkuu nimeomba chenji hapo kwenye 22,000/- kwa vikombe viwili vya kahawa.
 
Rai don't you believe kuna hotel za bei hiyo bongo??
Oasis ya morogoro navyoongea now kahawa 1 cup ni 4500. Na ni hotel ya kawaida saana kwa wanaoifahamu...

Hata Morogoro Hotel najua bei yake ni kubwa, ila kinachofanyika unaletewa Kikombe kikubwa cha bati na kingine kidogo na vitu vyote kama sukari, kahawa nk unakuwa unajipimia wewe mwenyewe, ukimaliza sawa, ukibakiza sawa.

Ila kwa bei ya 22,000/- mmh, bado. Labda nyota tano, ngoja nitauliza Kempiski kukoje ila Serena najua bei haifiki huko.
 
Kuna siku tukiwa sehemu moja yenye mandhari nzuri nilimuona babe wa ukweli kila sifa anayo ,mtu mzima nikajikaza kisabuni nikaenda kumtongoza alikuwa na besti zake 2

Ile nampiga sound nikapiga chafya ase makamasi yakanitapakaa mashavuni,puani halafu nilikuwa sina leso . aibu ya karne niliipata sina haja ya kuendelea kilichofuata

Siku nyingine namtongoza demu Fulani hivi tukiwa kwenye katikati ya kumshawishi ushuzi ukanitoka dah usiombe wakuu nilitoka nduki

Utatamani ardhi ipasuke uingie
 
siku moja nikiwa china tumeenda shopping nikawakimbia masela , nikaingia kwenye mall moja kubwa sana nikapanda lift huyo hadi maduka ya ghorofani... nimemaliza shopping nikapotea na nisijue pa kutokea na huku nje jamaa wananitafuta kuona hawanipati wakatoa taarifa polisi then wale polisi wakawataarifu wenzao waliomo ndani ya ile mall kuwa wakiona black man wam'escort to the exit. Kimbembe kimekuja hapa sasa, askari alivoniona akawa anakuja na mm nikaanza kumkimbia aisee tulitimuana mle ndani sitakaa nisahau. Mpaka nimechoka jamaa akanipeleka kwa masela huku nimepata aibu ya karne

Khaaaa ahsante kwa kunichekesha jioni hii

C.c kui espy

[emoji28] [emoji28] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Hii kiboko...LOL!
 
Kuna siku tukiwa sehemu moja yenye mandhari nzuri nilimuona babe wa ukweli kila sifa anayo ,mtu mzima nikajikaza kisabuni nikaenda kumtongoza alikuwa na besti zake 2

Ile nampiga sound nikapiga chafya ase makamasi yakanitapakaa mashavuni,puani halafu nilikuwa sina leso . aibu ya karne niliipata sina haja ya kuendelea kilichofuata

Siku nyingine namtongoza demu Fulani hivi tukiwa kwenye katikati ya kumshawishi ushuzi ukanitoka dah usiombe wakuu nilitoka nduki

Utatamani ardhi ipasuke uingie
Umefanya usiku niumalize vzr aiseee hahaaaaaaaa daaah nimeipenda ya kamasi
 
Me niliwah kugombania daladala yan ule mbanano na mvutano wa mlangoni mpaka nafika kwenye siti vifungo vya blauzi vyote vimetatuka brazia hii hapa
Me niliwah kugombania daladala yan ule mbanano na mvutano wa mlangoni mpaka nafika kwenye siti vifungo vya blauzi vyote vimetatuka brazia hii hapa
Hahaha aisee we mdada umenitia [COLOUR=#0000cc] ashki sana mwenzio[/COLOUR]
 
Nakumbuka ilikua 2012 hiyo naenda kuanza chuo Dom sasa kufika na njaa zangu nikavamia hotel. Basi nikaagiza wali samaki nikijua ni kama uswazi kwetu, kushangaa nikaletewa samaki mkubwa vibaya nikaona simalizi huyu nikauliza mbona mkubwa punguza!!! Nikaambiwa ndo kipimo basi nikala pale bili ikaja elfu kumi hahahah kidogo nigome kutoa maana samaki nilikula kidogo sana yani.

Kuanzia siku hiyo nikawa siingii hotel nikiwa town naenda kula stend ya hombolo cha buku 2.
 
Back
Top Bottom