Kwa upande wa marafiki.
Wakati nasoma kipindi hicho, nilikua na rafiki yangu ambaye nilikua namjali sana, tulikua tunaishi wote nyumba yetu hii ya kwao inafuata mbele,
Huyu rafiki tukifika nyumbani ni marafiki wakubwa tu, ila tukifika shule urafiki hakuna tena anakuona huna maana tena, anakuwa na marafiki zake wengine.
kipindi cha utoto nilidhani sitoweza kusurvive peke yangu bila ya mtu yoyote pembeni,
Ila nikaja gundua kwamba mtu ukimjali sana anakuona huna maana, anajua wewe huna cha kufanya bila ya yeye, lazima akuendeshe, lazima akudharau, lazima akupuuze.
Nilichokifanya nikajijengea msimamo kwamba "naweza kufanya chochote bila ya yoyote, yaani mimi na akili yangu tu nitaweza kufanya chochote kile" nikaanza kujiamini, japo nilitambua haitokua rahisi.(na ni kweli haikuwa rahisi)
*Nilianza kujipenda mwenyewe kwamba mimi ni wa muhimu kuliko yoyote yule mimi ni wathamani sana, sitokuja kujidharau tena, so haitotokea tena niumie sababu ya mtu mwingine
*nitafanya kila njia nipate Amani/furaha na Nitafanya kila njia furaha/amani yangu isipotee (japo sio rahisi pia)
*Sitosikiliza yoyote na hakuna atakaye badirisha msimamo wangu, sababu binadamu wengi ni wanafiki.
*Familia yangu ndio marafiki pekee wa kweli japo kila mtu yuko mbali na yake.
Na mpaka leo sijabadirika sina rafiki wa kweli zaidi ya salamu kila mtu na yake,
Hata wale niliosoma nao wachache ndio huwa tunaongea kwa bahati mbaya mwaka mara 1.
Maisha yangu ni
Job
Movies
Music
Books
Games
TV shows nk au kushinda kwenye magroup ya introverts wenzangu.
Unaweza dhani mimi ni alien ila ndio maisha yangu na hakuna kilichoaribika, na mambo ya kuumizana nilishayasahau,na furaha muda wote ipo nami, na sina mpango wa kuishi kama binadamu wengine, nikaishia kuumia tu.
Kiufupi haitokuja kutokea hiyo kitu.
Mtanisamehe kwa Uzi mrefu.
"Magic is believing in yourself if you can do that, you can make anything happen".