Je, ulishawahi kulazimisha mpenzi au rafiki aendelee kubaki maishani mwako?

Mkuu,

Kama nimekuelewa vizuri ni kuwa kila urafiki unaoupata unakuwa mzuri tu pale mwanzo. Mkishafahamiana au kuzoeana sana basi unapotezewa. Kama hicho ndicho kweli na kimetokea zaidi ya mara mbili kwa marafiki tofauti; nashawishika kuamini shida inaanzia kwako.

1. Labda wewe ni mtu generous sana, kama ndip basi unapataga marafiki wale wa kuchuma tu. Wakishapata walichodhamiria wanaanza kuwa wa kweli na nafsi zao, na ukweli wenyewe ni kuwa wao sio marafiki zako bali walikuja kwa purpose.

2. Labda wewe ni yule rafiki anae-suffocate mwenzake. Yaani muda wote lazima uwe na rafiki yako mpaka anakosa muda binafsi wa kufanya yake binafsi.

3. Labda wewe ni yule rafiki tegemezi kwenye kila jambo kuanzia mawazo mpaka kiuchumi.

4. Labda wewe ni rafiki mbinafsi, chako ni chako ila cha mwana ni chenu.

5. Labda wewe ni yule rafiki asiejua mipaka yake. Katika urafiki/mapenzi kuna inaginary boundaries. Mfano wewe ni mwanangu sana lakini mimi sipendagi mtu wa kuazima nguo zangu, au sipendagi mtu wa kila siku kuwa nyumbani kwangu etc na wewe unaamini urafiki ni kuazima nguo zangu au kushinda kwangu. Hapo lazima nitasepa.

Mkuu siri hapa ni kuweza wewe binafsi kuwa chanzo cha furaha na amani yako kwanza. Ni kuweza kujipenda wewe binafsi kwanza kabla ya kumpenda mwingine yeyote. Rafiki/mpenzi awe ni baada ya hayo.
 
Napenda misitu au nyika hivi. I recharge nikiwa mojawapo ya hizo sehemu.

Huku mjini nakuwa kama msukule tu.
 
Kuna mtu (binti) Niko naye karibu, naamini ananipenda, lakini katika kuongea na kujadili mambo kadha wa kadha, naona kama upeo wake wa kufikiri na kupambanua mambo in mdogo, walakini kwa kiasi fulani anawaza baadhi ya vitu vinavyonivutia.

Nifanyaje katika hili? Maana kwa upande fulani, ni vigumu Mimi kuwa karibu na mtu ambaye naweza kuongea jambo akatafsiri tofauti na nilichokuwa nimekusudia...!!! Hii inaleta mabishano mara nyingi...
 
Hebu mpe muda endelea kumsoma afu egemea zaidi kuangalia mambo postive kutoka kwake hopefully atakufaa. Hutampata mwenye vigezo vyote utakavyo kuna sehemu atapwaya tu ndio ubinaadamu. Endelea kua nae with time anaweza kufunguka akili
Ooh ok. Lo mimi sijui sana haya mambo kaka, kumbe inawezekana kufunguka kiakili/kifikra...
 
Ooh thanks brother. Introversion yetu hii ni kazi kukaa na mtu ambaye hawezi ku-fit kwenye friendship (kupiga stories na mijadaka ya hapa na pale kuhusu mambo tofauti tofauti) chief, walakini nimekuelewa vizuri mno. Mungu ni mwema na aliyoazimia hayawezi kuzuilika.
 
Basi jitenge mbali na huyo binti udimsababishie maumivu kama unaona hamuendani.
Ukiona introvetism yako inakufanya uwe too picky unaweza kua kama mimi tu. Just me and my phone and my world is enough
Naam nakuelewa kaka, najitahidi kuwa 'fair', nimekupata vema tangu jana hata sasa. Maandiko yako yamenipa nuru, na sipendi kumuumiza mtu. Ahsante sana.
 
Naam ahsante sana kwa hii elimu na hekima kaka
 
Mimi hua nikiona tu huyu mtu hanitaki tena najiweka pembeni mapema sana

Kikubwa usijipe umuhimu kwenye maisha ya mtu
 
Hii kitu sitaki itokee tena katika maisha yangu ilinitesa sana, Yaani mtu furaha yake ni kukuona unateseka tu kwaajili yake.
 
Sometimes huwa najihisi labda mimi ndo na matatizo ama sijui binadamu wanahitaji nini hasa, muda mwingine hunisema na dharau na majigambo kwa kua sio muongeaji na simu yangu ndo rafiki angu, sehemu za utulivu na isiyo na watu kabisa ndo huwa furaha yangu haswa, huwa najihisi amani sana naweza weka kambi asubuhi mpaka jioni jua likisha zama ndo ntaonekana home, kuna muda kama sauti huwa inaniambia i have to make friends, but nashindwa jinsi ya kuishi nao, sio ndugu sio marafiki binafsi huwa sielewi binadamu haswa wanahitaji nini?

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…