Je, ulishawahi kulazimisha mpenzi au rafiki aendelee kubaki maishani mwako?

Je, ulishawahi kulazimisha mpenzi au rafiki aendelee kubaki maishani mwako?

Sasa mkuu hapo si atakua amenunua heshima, kama ili uheshimiwe na moenzi wako lazima uwe na pesa[emoji45][emoji45]
Tafuta hela mdogo wangu.
Mapenzi bila hela hayaendi kabisa,muda wote uwe mtupu mfukoni tena mtoto wa kiume!
Hakuna Malaika atakayekuvumilia hadi mwisho,
Si kununua mapenzi, ni wajibu wako kutafuta.
 
Ni wajibu wangu kuhudumia na kutafuta kwa ajili ya mpenzi na familia.. lakini pia wewe mwanamke inatakiwa uridhike na kile nachokipata. Tatizo ni kutokujishughukisha kabisa...
Kumbe anajua ni wajibu wako!
Sasa kwanini hapo juu unatetea kutokuwa na pesa
Mapenzi si pesa ila pesa ni muhimu katika mapenzi.
 
Thank you Bro kwa thread nzur imayagusa maisha yangu moja kwa moja nilikuwa napata wakat mgum nilikuwa nawang'ang'ania watu wasio niitaji baada ya kusoma hii thread yako imeniimpower na kuona naweza ishi tu good life hata bila wao... Be blessed
 
Katika maisha yangu sijawahi kuendekeza kitu kinachoitwa kujipendekeza au shobo.Kwenye mapenzi ukisema haiwezekani usifikirie nitarudi nyuma na kubembeleza?kwenye urafiki nikiona huelewi au unajiona keki aisee kwangu huwa nakuwa keki kupita kiasi!!Kimsingi mtu akiniletea nyodo huwa nageuka kuwa mwalimu wa nyondo naweza pita hata bila kukusalimia kimsingi nina misimamo katika maisha yangu na siwezi ishi kwa kutegemea uhai au uwepo wa mtu mwingine!!Starehe yangu ni muziki,kuwa na hela nyingi kwenye wallet,tungi ila kwa upande wa ma- chicks huwa wanakuja wenyewe sina ujinga wa kutukuza may.

I HUMBLY SUBMIT.
 
Mimi huwa sipendi kudeal na watu wasio na hisia. Huwa nawaona kama majini na huwa natokea kuwachukia sana.

Binadamu hatukuumbwa kuishi pekee yetu lazima uwe karibu ya watu na mtu anaekupenda kwa dhati.

Mtu anae kusalimia asubuhi mnapoamka aidha kwa kukupigia simu au kukutext, mtu ambaye atataka kujua unakula chakula vema, atakae pokea simu na kuwasikiana na wewe hata akiwa busy, atakae kuwa anataka kupanga maisha na wewe na kuweka kila alichokuwa nacho mezani ili kitumike kuyapata hayo maendeleo.

Ambaye hata ikaimu nafasi yako kwa mtu mwingine na kukuonyesha wewe ni mtu pekee kuwa nae.

Sasa usipopata wa hivi ndio unakutana na hayo madudu yenye ubinafsi umeongelea hapo.
 
Kwenye Million ni Mmoja
Wengi ni wawili
 
Rafiki sina up to moment naandika hivi sina rafiki yule wakusema naweza mwita rafiki

nina marafiki ila sio (best friends) ni marafiki tu ambao hata awe kimya mwaka sishtuki

mpenzi ilitokeaga zamani sijui ni kwasababu nilikua new comer kwenye mahaba sijui

yule dada tulitengana kama miezi kwasababu ya likizo za shule,baada ya likizo kuisha

kurudi najua bado sisi ni wapenzi kumbe mwenzangu kashatafuta mtu wake mwingine

akaniambia hatuwezi kuwa wapenzi tena labda tuwe marafiki tu,aiseee nilishamtishia hadi

kujinyonga ili tu ajue nampenda ila wapi,nikaenda kwao nikalala nnje getini usiku hadi pakakucha ila wapi

mwisho kabisa nikaona asintanie,nikaandika wosia kisha nikaenda fata sumu ya panya ya maji nikanywa yote

watu wakaniokoa kimbiza hospital nikapona baada ya pale nikapewa counselling 1 hatari sana

ikanisaidia nikaweza anza ishi kwa shida na kukubali matokeo,up to moment sirudii penda kisenge vile

ila kama ni ku force yule dada anirudie,niliforce sana hamna mbinu sijatumia.
[emoji16][emoji16][emoji16]aisee kuna watu mmepitia mambo mazito sana aise .... Nashukuru mitaa ilinikomaza vya kutosha ... Muda wa kuli Lia mapenzi huwaga Sina if tukigombana na m-bebe nitajaribu kumbembeleza na kujishusha kwa siku 1 au 2 tu nikiona bado anakaza shingo naachana nae ...no texting even calls ..simtafuti mpaka anitafute na akinitafuta sionyeshi makasiriko na mpatia ushirikiano bila hiyana Kama hakuna kilichotokea Ila nakuwa tayari nimeshapata fundisho na kuanza kuishi nae kimitego yaani mguu 1 ndani 1 nje ...
 
Kwa upande wa marafiki.

Wakati nasoma kipindi hicho, nilikua na rafiki yangu ambaye nilikua namjali sana, tulikua tunaishi wote nyumba yetu hii ya kwao inafuata mbele,
Huyu rafiki tukifika nyumbani ni marafiki wakubwa tu, ila tukifika shule urafiki hakuna tena anakuona huna maana tena, anakuwa na marafiki zake wengine.
kipindi cha utoto nilidhani sitoweza kusurvive peke yangu bila ya mtu yoyote pembeni,
Ila nikaja gundua kwamba mtu ukimjali sana anakuona huna maana, anajua wewe huna cha kufanya bila ya yeye, lazima akuendeshe, lazima akudharau, lazima akupuuze.

Nilichokifanya nikajijengea msimamo kwamba "naweza kufanya chochote bila ya yoyote, yaani mimi na akili yangu tu nitaweza kufanya chochote kile" nikaanza kujiamini, japo nilitambua haitokua rahisi.(na ni kweli haikuwa rahisi)
*Nilianza kujipenda mwenyewe kwamba mimi ni wa muhimu kuliko yoyote yule mimi ni wathamani sana, sitokuja kujidharau tena, so haitotokea tena niumie sababu ya mtu mwingine
*nitafanya kila njia nipate Amani/furaha na Nitafanya kila njia furaha/amani yangu isipotee (japo sio rahisi pia)
*Sitosikiliza yoyote na hakuna atakaye badirisha msimamo wangu, sababu binadamu wengi ni wanafiki.
*Familia yangu ndio marafiki pekee wa kweli japo kila mtu yuko mbali na yake.
Na mpaka leo sijabadirika sina rafiki wa kweli zaidi ya salamu kila mtu na yake,
Hata wale niliosoma nao wachache ndio huwa tunaongea kwa bahati mbaya mwaka mara 1.

Maisha yangu ni
Job
Movies
Music
Books
Games
TV shows nk au kushinda kwenye magroup ya introverts wenzangu.

Unaweza dhani mimi ni alien ila ndio maisha yangu na hakuna kilichoaribika, na mambo ya kuumizana nilishayasahau,na furaha muda wote ipo nami, na sina mpango wa kuishi kama binadamu wengine, nikaishia kuumia tu.
Kiufupi haitokuja kutokea hiyo kitu.

Mtanisamehe kwa Uzi mrefu.

"Magic is believing in yourself if you can do that, you can make anything happen".
Niliwahi pitia break up moja 7bu nilijiattach sana na yule bint

Basi kila ulichosema hapo juu n ukweli:
Ukmjali sana mtu anakudharau ana kupuuza na pia atakuumiza tuu
Njia nilitumia kupona na kumsahau n kuadd wigo wa vitu huwa nafanya kwa hio nikawa napoteza muda mwingi huko na maisha yakasonga

Ujinga wa hivi viumbe vya Mungu alinitafuta baadae, nilikuwa mwenywe bado ila hakuipata hio nafasi tena.
 
[emoji16][emoji16][emoji16]aisee kuna watu mmepitia mambo mazito sana aise .... Nashukuru mitaa ilinikomaza vya kutosha ... Muda wa kuli Lia mapenzi huwaga Sina if tukigombana na m-bebe nitajaribu kumbembeleza na kujishusha kwa siku 1 au 2 tu nikiona bado anakaza shingo naachana nae ...no texting even calls ..simtafuti mpaka anitafute na akinitafuta sionyeshi makasiriko na mpatia ushirikiano bila hiyana Kama hakuna kilichotokea Ila nakuwa tayari nimeshapata fundisho na kuanza kuishi nae kimitego yaani mguu 1 ndani 1 nje ...

Inatwa wanaume tuwe hii sasa
 
Back
Top Bottom