Kitu kinachofanya tunashindwa kupata yale yanayofaa tuyapate ni kutokua na Subira! Tunapenda kuwahisha mambo ili tupate yale ambayo tunayataka kwa muda Fulani tunaotaka ila tunasahau kua yatakiwa tupate yale yanayostahili/yatufaoyo kuyapata kwa muda ufaoa. Subira na utii wako ndio ghalama pekee ambayo unatakiwa uilipe kwa Mungu ili upate yale unayostahili kupata. Kama huwezi kusubiri upate yale unayostahili kwa muda unaostahili ila unataka upate yale unayoyataka kwa muda unaoutaka hivyo jua unamkaribisha Shetani maishani mwako maana utakua huna tena subira, tama itakua imejaza moyo wako na shetani ndie anayetoa vitu vya tamaa.
Haijalishi umekaa nyumbani bila ajira, umekaa muda gani bila mume,umekaa muda gani bila mtoto kamwe usiruhusu matatizo yako yakawa Advantage ya kukupata kirahisi, wewe ni wa thamani na mwili wako ni wa thamani ndio maana Mungu kakuamini na kukupa heshima ya kuufanya mwili wako ukamilishe uumbaji. Shida zako na mateso yako yasikufanye uishushe hadhi hiyo uliyopewa kwa kuwaacha mameneja wakutumie kadri wawezavyo. Muda ukifika utapata yote mazuri yaliyoandaliwa ajili yako..Huna haja ya kuwahisha mambo hadi unaamua kugawa penzi ili upate ajira. Jithamini, U wathamani mno!
PS. Natambua binaadamu tumeumbwa na madhaifu na moja ya dhaifu letu/langu ni kukata tamaa pale mambo yanapokua magumu! Lakini nivyema pale unapokata tamaa na kujirudi kwamba hukujiumba wewe, aliyekuumba anakuona na ana kusudi nawe.
Please God understand us bless our family guide us all before we fall to this insanity. It's gonna take the man in Us, to conquer this insanity
-Vinjiii