wewe ndio unaweza kujenga au kubomoa hatima ya maisha yako kutokana na matendo yako, fanya kila aiana ya upuuzi kwenye sinia hili tunaloita dunia ila HESHIMU MWILI WAKO NI WATHAMANI (A wonderful made) . Lakini pia kwenu watu mliopewa dhamani ya kua kwenye ngazi za juu katika mashirika na makampuni jitahidini muwe na utu na kujali maadili ya kazi zenu. Kama unataka kumsaidia mtu saidia then mwache aende sio umtake kimapenzi, hata usipomtaka kimapenzi basi msaada wako usiwe fimbo ya kumchapia. Umnyanyase kiakili na kimwili kisa bila wewe asingepata kazi hiyo. Saidia kisha futa kabisa katika kumbukumbu zako kua uliwahi kusaidia mdada Fulani kupata kazi katika kampuni uliyopo. Hupati faida yoyote ukitangaza kama uliwahi msaidia mtu Fulani.
-Life is full of Surprises and Possibil
Kuwa katika nafasi za nyadhifa inashauriwa kutendea wengine mema kama ulivyoshauri.
Lakini kuna hizi rushwa za ngono ni hatari, hauombi unaletewa, inakufuata pamoja na gharama zote za "gesti" na vinywaji, usipokuwa na moyo wa subira, ni rahisi sana kuingia mkenge wa kashifa!
Mara nyingi rushwa ya namna hiyo ikiletwa ukakataa kuipokea, huleta taharuki kwa mtoaji na hujisikia dhalili sana.
Nafasi za kazi ni haki ya applicants wenye sifa zilizotangazwa kama wanazo.
Wakati flani nikiwa katika wadhifa na mamlaka, niliwahi kuletewa rushwa za ngono mara nyingi na zote nilizipangua bila jazba wala lawama.
Watu walioniletea rushwa hizo wengi walikuwa wanazo sifa stahiki hadi nikawa ninashangaa kuwa hii imekaaje!
Kwanza kabla nilikuwa sielewi mtoa rushwa ataanza anzaje kunishawishi, yaani kiaje na kwa namna gani!
Kumbe ni rahisi tu, hasa chanzo kikiwa ni simu!
Natoa mfano wa mtego mmoja wa rushwa nilioupangua.
Zilipotangazwa nafasi za ajira pale hamashauri, sikujua huyo mama alipataje namba zangu za simu pamoja na jina langu kamili kisha akanipigia simu..."mkuu upo wapi?"
Mimi: "nipo nyumbani".
Yeye: "ntakuonaje sasa nnashida".
Mimi: "shida gani, nnaongea na nani kwanza?"
Yeye: akanitajia jina silijui, nikavutiwa kuonana naye kwa utambuzi zaidi, nikampatia appointment.
Huyo mama alikuja kajiandaa kwa rushwa ya ngono pamoja na pesa za gharama ya gesti wazi wazi.
Baada ya kukutana:
Yeye: "mkuu mimi- - - ni mmojawapo wa applicants tulioleta maombi ya kazi leo ofisini kwako".
Yeye: "Dunia ya leo bila kujitoa ninajua hauwezi fanikiwa lolote hata uwe na sifa vipi, hivyo mkuu ninaomba unisaidie kunipitishia maombi yangu na mimi niko radhi kujitoa kwa chochote upendacho kama shukrani ya utangulizi kwa unachoenda kunifanyia".
Rushwa hiyo niliikataa kuipokea lakini nilimsaidia kumpatia nafasi aliyoiomba bila ya masharti yoyote.
Wakati tunaachana alikosa raha na alinywea kabisa akijuta kwa kuhisi angelipoteza nafasi kwa kihere here chake hicho.