Je, ulishawahi kushuka na begi/mzigo wa abiria mwenzio kwa bahati mbaya? Mtu aliyeshuka na box langu la samaki mwaka 2012 sasa ni family friend

Ndugu yangu mmoja yeye alitelekeza dumu la lita 20 la pombe aina ya gongo kwenye treni. Alikua anasafirisha kama mafuta. Ile mtikisiko na mkanyagano si mfuniko ukafunguka kitu kikaanza kutema smell kama ya spirit, watu kuuliza dumu la nani mshikaji akakauka. Polisi wakaja kulibeba nadhani walienda kufanya sherehe huko
 
Haya ya kubebea watu mizigo hasa airport Kama abiria inafaa kuwa makini Sana yanaweza yakakupata ya ushahidi haujakamilika kwa usamaria wema wako.
Heri upige self na unaemfanyia usamaria wema Ili kikinuka wakabidhi mtu wao
 
Mimi katika harakati zangu. Nilitoka Unguja kufika bara. Kushuka kwenye boti pale bandarini. Vijana wa Azam wameniambia mizigo yote unayifwata mbele ya mlango wa kuelekea Custama. Mie nimetii naelekea sehemu iliomwaga mizigo ya abiria... Vijana wa pale bandarini wanachagamkia kugombania mizigo ya kubeba. Vijana wawili wamejitokeza wamechagua begi langu. Moja kati yao amesema ndo hilo livute. Na mimi nimenyamaza nawangalia kwa jicho la huruma ila aliekuja kuharibu shoo yote ndo ule niliefwatana nae.

Kusema kusema Sheikh begi lako si ndo hilo vijana yanaolinyanyua? Nilimwambia ndio ila ananiletea hapa. Ghafla abiria yote wameshangaa. Kwa upole nilionyesha na bila kubishana nao wale vijana. Niliwambia nimenyamaza kusudi ili nijue mwisho wa mchezo wenu? Ili mkichezecha begi langu rafu. Na mimi niwapoteze kimya kimya huko baharini.
 
Hahahahaaa eti uwapoteze kimya kimya. Ulionesha uvumilivu wa hali ya juu sana
 
Hahahahaaa eti uwapoteze kimya kimya. Ulionesha uvumilivu wa hali ya juu sana
Ndio. Nilikua nimetulia kuona mwisho wao. Tulikua tunapata habari mbalimbali za wizi na utapeli wa bongo. Kwahiyo mimi nilikua tayari kujipanga mapema. Wangeondoka na begi langu. Na mimi ningeondoka nao. Bila kupiga kelele. Kwanza nilijiona kazi yangu ingekua nyepesi....
 
Kuna siku Songea tumekesha bar Planet sijui bado ipo! Asubuhi nikaunganisha na superfeo hadi Njombe. Wakati natoa bag nikachukua ambalo sio langu, nikapanda bus za kwenda Ludewa.
Kufika milima ya gangitoroli nikapokea simu kuwa tumechanganyana mabag, mwenye langu kaliweka ofisi za superfeo kwa hiyo nitalikuta pale.
Nilivyofika kituo cha nyumbani nikaliacha tu stand kwa jamaa then nyumbani nikaenda kama le baharia yaani sina kitu mkononi hata peni.
Siku ya pili nikalipitia na kwenda kubadilishana Njombe.
 
Huo uandishi sasa... dah!
 
Sasa kazi yako ingekuwaje nyepesi wakati mngetumbukia wote huko baharini sheikh?
 
Kwenye chatting kama hizi za JF mpangilio wa maandishi sio muhimu kiviiiile mkuu
Mbona panatokea wajuaji humu ndani? Jambo la busara ndio kukubaliana nao ili usilete majibizano na watu wa dizaini kama hivyo. Utagundua wengi wao ni vitoto vya millenium.....
 
Mbona panatokea wajuaji humu ndani? Jambo la busara ndo kukubaliana nao.ili usilete majibizano nawatu wa dizaini kama hivyo. Utagundua wengi mwao ni vitoto vya millenium.....
Sawa mkuu. JF siku hizi ina watu wengi wa kila hulka na tabia tofauti na zamani miaka ya 2012.
 
Ungewaacha watu wachangie kwanza,hizi siti za mbele hutakiwi dereva kuzimiliki mwenyewe😁
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…