Grand Canyon
JF-Expert Member
- Jan 2, 2020
- 545
- 1,191
we are on the road so we can't type right now!.WanaJF wenye magari mbona mmeususa huu uzi
Naona tumepata wa kutoa dukuduku letu,asante.Sina chochote ila tu wale wadada wanaofanya mazoezi barabarani wasivae taiti jamani, kuna siku gari litauvaa mtaro kwasababu yao.
PoleniKipindi Nipo Chuo Rafiki Yangu Alikuwa ni Trucker Binafsi Nikawa Nasafiri Naye Sana Congo,Rwanda nk. Nilikuwa Napata Experience Kubwa Sababu Muda Akichoka Nakamatia Chuma Mimi Kaseja Mdogo Mdogo Nimekuja Kuzoea ile FAW nikawa ni mwendo spidi kukimbizana Siku Napata Ajali ilikuwa Alfajiri Tunang'oa Nanga Wenzangu Wengine Wamelala Wengine Zinapigwa Stori za Mpira Sasa Nimegeuza Shingo ile Narudisha Natahamaki Mbele Naona Majani yamewekwa barabarani mbele kuna Lori limeharibika haikuwa issue kubwa kwangu sasa ile nahama barabara nimpite Nakutana na Tandam Fuso ipo Spidi Yule Mshenzi Akawasha Taa Full Halafu Akazima. Sikuona Tena Vizuri Nikaitoa Chuma Kwenye Site ya ile Fuso Hapo Nimeshaingia Nje ya Barabara Kufumba na Kufumbua Chuma Imepinduka Wote Tupo Nje Kila Mtu Kadondokea Kivyake Cabin ya ile FAW Haitamaniki Ni Mungu Tu Siku Zetu Zilikuwa Bado.the end!
Asante Mkuu Tulishapoa Nilichojifunza ni kuwa Makini Muda WotePoleni
Siku moja miaka ya 2014 nimeenda kule rudy's farm. Kijana kabisa nina moto nina altezza. Nimekula nyama nyingi na pombe zipanda kichwani. Basi tumetoka kama saa 2 au 3 hivi usiku mimi na jamaa yangu yeye alikuwa na mark x. Sasa akawa anaipeleka moto na mimi namfukuza mbio tunefika pale ledger plazza nikampita kwenye kile kilami kinachoenda hadi kuungana na barabara ya ununio.Mimi niliendesha gari kutoka Dar, nikiwa maeneo fulani ya Singida, kuna sehemu imenyooka kweli kweli malori mawili na gari ndogo moja yalikuwa mbele.
Nilikanyaga mafuta gari ikawa spidi kali sana. Nakaribia kuovateki gari ndogo nayo ikataka kuovateki. Nilipiga honi akarudi ndani nikaovateki mbele kulikuwa na bodaboda akatoka barabarani akanipisha, naye alikuwa spidi sijui ilikuwaje baada ya kumpita.
Mpaka leo huwa najiuliza yule jamaa wa gari dogo angeendelea kuovateki na ile spidi yangu sijui ingekuwaje!
Je wewe umewahi kufanya misteki barabarani ambayo haikuleta madhara?
Boda boda akili zao wanazijua wenyewe.Ilikuwa mwaka Jana Maeneo ya Sido kuelekea Jet rumo. Nilipanda gari Maeneo ya Vingunguti zile gari za Special Hire full kiyoyozi ilipakia Abiria wachache Tu na ni level seat tukaongoa nanga uelekeo G/mboto.
Dakika chache baadae tulipitwa na Pikipiki Ikiwa na Abiria wanne wote wakiwa ni watoto chini ya Miaka 18 hivi. Wakike wawili na wakiume wawili inaonekana walikuwa wanatokea kwenye Ngoma, wanavibe mixer kujiyumbisha yumbisha kwenye Pikipiki. Lile Jambo likawa kama Mjadala huku safari ikiendelea.
Sekunde chache baadae ikatupita Pikipiki nyingine tena hii ikiwa na Abiria watano nao wakiwa chini ya Miaka 18. Ile yenye Abiria wanne ikaovartake na kuzidi kupotea, Yule mwenye Abiria watano wakati anajitahidi kuhama Sasa naye aovertake, Nyuma yetu ikatupita tena klugger nyeusi, Yule boda akawa anaifata ile krugger pasipo kujua anashtuka ameshaigemea.
Mwenye krugger akakataa Kwa kuongeza mwendo ili Hali balance ya Yule boda ilikuwa ni Yeye, boda akarudi kushoto Kwa Nguvu, baadae kulia akayaingia Yale machumachuma ya nembo ya Tanzania yaliyowekwaga na makonda akiwa RPC.
Kukawa vumbi kubwa, Vile vyumba vikawa vinaruka juu Kwa Kasi. Kiufupi walipona wawili, Dereva na Binti mmj Abiria.
Kinachoniumiza ni Kuwa wakati Dereva Yule anapotea kutoka kushoto kuja kulia na Kukosa balance kwenye krugger, Tulikuwa tukimpigia kelele ndani ya gari,.ila changamoto ilikuwa ni gari vioo vyote vimefungwa na AC on. Kama lingekuwa gari vioo viko wazi Tungewaokoa wasipate ajali.
Kingine Dereva Wa klugger kama angeendelea kupunguza mwendo taratibu taratibu Hadi anasimama wale wasingekufa wala kupata ajali Ile maana Dereva Alikuwa ameegemea Ile gari na mkono Wa kulia aliishikiliaile gari kabla haijaongeza mwendo na Kumkataa.