Je uliwahi kufanya mistake wakati ukiendesha gari, unalojutia mpaka leo?

Je uliwahi kufanya mistake wakati ukiendesha gari, unalojutia mpaka leo?

Ilikuwa December 2023 niko na Harrier old model na familia natoka Moro napeleka watoto Tanga, mida ya saa 6 na dakika 10 usiku nimepita Segera nakaribia Hale kuna vile vilima vilima na kona, ghafla natokea kwenye kona nakutana na scania semi trailer 2 zimepakia cement zina overtekiana, nashukuru Mungu nilikuwa chini ya 60kph, ilibidi niingie kwenye kichaka na nashukuru hakukuwa na msingi vinginevyo ilikuwa ni balaa, ninachokumbuka ni mke wangu alipiga kelele na kutaja jina la Yesu na watoto wangu wa2 wakiwa wamelala siti ya nyuma, tulikuwa wa4 kwenye gari, nashukuru nilipata ujasiri sikupaniki na nikapata haraka wazo la kuhama na kutoka nje ya barabara na wakapita kwa spidi kali wote wa2 na hawakusimama kunijulia hali, nilirudi barabarani gari ikiwa na mikwaruzo na tatizo kwenye tairi ya mbele kushoto lakini nilifika Tanga salama.
 
Back
Top Bottom