Je uliwahi kufumaniwa na mke wako hata meseji(za mapenzi) kwenye simu Yako?

Je uliwahi kufumaniwa na mke wako hata meseji(za mapenzi) kwenye simu Yako?

Mi siwezi kukukomesha sababu huwezi kuwa na mwanamke aina yangu tunaotumia akili za bibi zetu Eva na Delilah, komaa na vilaza wenzio
Wewe ndo kilaza zaidi yangu. Maana huwezi fatilia Uzi wa kilaza na unajinasibu wazi Mimi sio wa aina Yako. Maajabu unafatilia Uzi wa kilaza umechelewa kulala na umeamkaje nao Uzi wa kilaza Mimi badala ya kuwa na mmeo upo na Mimi twende kazi kilaza mwenzangu
 
Kwanza niliporudi nyumbani sikumkuta, simu sizioni, nikipiga anakata tu, nikajua tu hapa tayari mambo yameshatibuka.

Mbaya zaidi akaenda kwenye gari, akakuta Kuna simu ndogo Ina text zingine na tkt mbili za majina yetu. Hapakua na namna ningekataa.

Akaondoka na gari na bag yake akisema harudi Tena nyumbani na watoto anawaacha.

Baada ya kuomba sana tuonane, akasema Yuko Sleep way. Nikaacha gari Kwa askari wa SGA Makumbusho hata bila makabidhiano maalum ( hili ni balaa lingine nililiibua, gari ilipelekwa Oyster bay police).

Nilipofika mahali yupo tunaondoka huku naendesha sikuongea kitu, wakati huo analia tu na kutoa maneno ya uchungu. Nakumbuka nilisema tu naomba msamaha bila maelezo mengi huku naendesha kuelekea kanisani. Hadi wakati huo bag yake ipo kwenye gari na ameshikilia msimamo wake wa kutorudi nyumbani.

Nilijuafika wachungaji wameshaondoka ilikua kwenye saa mbili jioni. Akaniuliza Sasa unakuja kufanya Nini kanisani? Nikamwambia nataka niombewe...alijikuta anacheka Kwa sauti na kutamka, yaani ujinga wako ndio umeona uje kusumbua watu usiku huu?

Nikasema basi twende nyumbani, nipe muda wa mwezi mmoja nikatafute nyumba na Dada wa kazi Kisha ntakuja kuwachukua watoto. Kwa nilichokukosea, una haki ya kufanya chochote.

Nikasema hichi ulichokiona ni kitu kidogo sana, mie nna Pepo kama sio nguvu za Giza, nnakunywa pombe, balaa la wanawake siwezi kulielezea, huyu sio mimi. Alitoa macho kusikia nnakunywa pombe ( nilikua sijawahi hata kuonja, hata sikua na wanawake ila Sasa katika kusuluhisha, ikabidi nijipatie ubaya wote).

Nilifanikiwa kuondoka kurudi kazini, uzuri usiku japo kishingo upande kimasihara ikachukua mkondo wake.

Hapo balaa la gari niliyoiacha Makumbusho likaibuka. Liliunguruma Kwa wiki Moja nikafanikiwa kuichukua gari Kituo Cha polisi.
Hebu na hili la gari lisemee kidogo naona nalo lina jambo la kukomaa nalo
 
Wewe ndo kilaza zaidi yangu. Maana huwezi fatilia Uzi wa kilaza na unajinasibu wazi Mimi sio wa aina Yako. Maajabu unafatilia Uzi wa kilaza umechelewa kulala na umeamkaje nao Uzi wa kilaza Mimi badala ya kuwa na mmeo upo na Mimi twende kazi kilaza mwenzangu
Kwa akili hizi we kweli kilaza
 
Kumbe ndio maana una jeuri yote hiyo mkeo ni mama anaesubiri uweke mkwanja mezani so inabidi tu akubaliane na lolote maana hana namna ingekuwa na kipato chake mkuu ungepata majibu. Hingera sana kwa kumfanya mkeo inferior hapo umewin sana
Eee na Kwa hili mkuu mwanamke wangu lazima awe na ni mama wa nyumbani.

Analisha kuku chotara na Hela yake sigusi na ana awasaidizi wa2 kwahiyo kuhusu Hela anazo tu kushika m5+ baada ya miezi 4 nikawaida na ana machine ya kusaga karanga nk
 
Hongera mkuu mwanaume kweli kukataa ni silaha ya kwanza ila inaonekana mkeo ni jobless hana lolote kila kitu anategemea toka kwako or anacho cha kwake ila wewe una pesa nyingi sana kwahiyo anaona kabisa akitoka atamiss kitu. Trust me mwanamke kama ana kipato chake na wewe kipato chako ni cha kawaida halafu umfanyie hivyo kuna mawili either atabaki hapo ila ndoa yenu inakuwa imekufa kwa ndani kila mtu atafanya lake ni nje tu watu wataona mko pamoja au ataondona na kuendelea na maisha yake. The only way to control woman ni mwanaume kuwa na uchumi mkubwa mara tatu zaidi yake hapo atakutii na ndio maana siku zote hapa tunawaambia NDOA NI

Labda uamue kuwa single, kwa haya ninayoyaona kwa mwanaume wa kibongo ukijumuisha na kaka na baba zangu, ni asilimia ndogo au hakuna kabisa mwanaume asiyechepuka.
Wanawake wanaamua wakubali yaishe maana hawana uhakika watapata asiyechepuka huko mbeleni.
 
Umeacha kuchepuka au unaendelea tajiri?
Lile tukio lilinipa mafunzo mengi sana. Kwanza nilijiona mjinga wa kiwango Cha juu kuchepuka. Shida nyingine Kwa kutokua na uzoefu kwenye kuchepuka, kukamatika ilikua rahisi sana.

Pili, nikaona jinsi Gani namuumiza mwenzangu wangu Kwa kuchepuka. Ikafika mahali naogopa kuchepuka sio Kwa kuogopa kukamatwa au kugundulika, nikawa sitaki kabisa kumuumiza mwenzangu hata asipojua au kugundulika.

Machungu aliyokua nayo yalinifanya nichukue kabisa kuchepuka....

Back to your question...au basi
 
Lile tukio lilinipa mafunzo mengi sana. Kwanza nilijiona mjinga wa kiwango Cha juu kuchepuka. Shida nyingine Kwa kutokua na uzoefu kwenye kuchepuka, kukamatika ilikua rahisi sana.

Pili, nikaona jinsi Gani namuumiza mwenzangu wangu Kwa kuchepuka. Ikafika mahali naogopa kuchepuka sio Kwa kuogopa kukamatwa au kugundulika, nikawa sitaki kabisa kumuumiza mwenzangu hata asipojua au kugundulika.

Machungu aliyokua nayo yalinifanya nichukue kabisa kuchepuka....

Back to your question...au basi
Umeacha kuchepuka tajiri?
 
Wakuu salama.

Hii special Kwa wanaume wasiokubali kutikiswa Wala kujambiwa na wife hata kama anampenda na amemkosea

Kauli mbiu ni:MWANAUME HALISI HAKUBALI KOSA.

Ilinitokea siku Moja nilikuwa naacha simu nyumbani naenda kazini (maana sikuwa na ruhusa ya kuingia na simu kazini kipindi hicho)

Nilkuwa na manzi mmoja Ambae tulipendana sana pengine ilibaki manusura tu nimuone.

Siku hiyo natoka kazini nikamkuta wife kanuna kavimba uso Na ana Angalia kama hanioni.

Kwa kawaida Mimi nishamkataza kunisalimia mbele ya Watoto ama mbele ya wageni.

Ni lazima anifate chumbani anisalimie na kunipa lineup yote ya nyumbani ilivyoenda kutwa nzima

Hii ndo kawaida yangu. Baada ya kuona Kuna dalili isiyo ya kawaida nikauliza unaumwa?

Akajibu si heri hata kuumwa

Nikamuuliza basi umefiwa?

Akajibu mara 100 ningekuwa nimefiwa!

Majibu haya yalinifanya nijiongeze kuwa Leo Kuna kimeo asee.

Sikubabaika hata kidogo. Nikawahi kuangalia simu Ile nafungua msg!!

Aiseee sikuamini nilichokiona

Wamechat na manzi angu Hadi uvumilivu ukamshinda akamtukana!!

Baadhi ya chatting zao zilikuwa Hivi

Manzi:My...
Wife :nambie mpenzi upo poa

Manzi :Nipo poa tu

Wife :nambie ....

Manzi: baby ahadi yetu si Iko palepale Mme wangu maana wewe Kwa kusahau mambo

Wife: mmmh ahadi yetu Tena ipi jamaniii

Manzi:akafunguka story yte na hapa ndipo wife akajitamburisha)

Story ilikuwa Hivi.

Huyu manzi ni mtoto wa 3 kwao na alikuwa Bado hajaolewa ndo ametoka chuo kipindi anatoka chuo yupo tu mzee wake akawa amepta mafao yake baada ya kustaafu ualimu.

Mzee akamwambia mtoto wake achague biashara atakayoweza kusimamia apewe mtaji muda huo akiwa Kwa wazee wake.

Manzi bila kupoteza muda akanidokeza akiniomba ushauri.

Nami nipo vzr nikamuuliza kwanza wewe unapenda biashara Gani?

Akasema anapenda duka la nguo ama vipodozi.

Nikamjibu fanya vipodozi maana mtaani kwao kulikuwa na duka Moja tu la vipodoz Wala sio kubwa na limekata kizamani sana na muuzaji hna customer care

Vilevile hapo nyuma nimewahi simamia pia duka la vipondozi la nyumbani kwetu baada ya dada yangu kuolewa aliyekuwa anauza.

Kama haitoshi dada yangu huyohyo alienda kufunguiwa duka la vipodozi ambalo analo Hadi Leo!

Inshort

Tulipanga kwenda Dar kununua vipodozi Mimi, dada na yeye (3)huku dada akijua kabisa mchezo.

Manzi alifunguka Kwa wife kuwa..... Ile ahadi ya kwenda dar kununua vipodozi umesahau Tena na uliniahidi mwenyewe?

Wife kusikia vile basi akajua Hela ya mtaji nimetoa Mimi ndo akamwambia unachti na mke wake mbwa wewe usiekuwa na haya Kwa wanaume wa wenzio

Malaya ndio maana hujaolewa unachezewa tu(hapo sijabadiri nguo ndo nasoma jasho linatiririka wife hata hajui yupo nje bado)

Nikavaa nikatoka huyoo mtaani

Nikaendelea kusoma nikakaa sehemu Moja Hivi uwanjani watu hufanya mazoezi ya mpira.

Manzi alipoona katukanwa nae kajibu mapigo alimtukana wife vya ndani kuwa hujui kuosha k ndio maana anakuacha anakuja kwangu na Kwa taarifa Yako Hadi gari itanunuliwa!!

Hii vita ilikuwa sio poa
Walipochoka wakapigiana simu maana nilkuta manzi kapiga na wife kapiga kama mara4.

Ilipofika saa2 nikarudi home nimenunua matunda nikakuta amepika akanikaribisha kula ila yeye Hali.

Nikanawa nikamuuliza mbona wewe huli? Akasema kula tu nikamwambia haiwezi tokea

Umenuna nimekuulza unaumwa hajajibu umefiwa hujajibu

Je kama umeweka Sumu humu? basi kula mwenyew au mwaga.

Nikarudi kula mgahawani nikarudi kulala.

Nikajifanya kama sijui kitu Wala sijaona kitu kwenye simu yangu.

Kumbuka nikiwa uwanjani nilimpigia manzi nikamuomba msamaha Kwa yaliyo tokea nikamwambia Mimi nimeshamwambia kabisa nimeoa

hivo alikuwa anakutukana kama mke mwenza sorry baby haya yamepita kuwa na amani hayatajirudia Tena.

Kesho yake nikaenda job kama Kawa nikarudi hivyo hivo kanuna Nami sijali nacheza na dogo tu (mtoto) Wala Sina hofu yoyote Ile.

Siku3 natoka kazini Sasa ndo akanikalisha kikao

Akanieleza wee Mimi nikamwambia sijui kabisa Wala msg sijaona hata Moja kule.

Alinibana lkn wapi nikamwambia Mimi sijui na Mimi nilijua labda una mawazo Yako tu hutaki nishirikisha.

Ikabidi apige simu amuite mzee

Mzee akaja kweli wakanikalisha kikao. Nikajibu mzee sikuona msg Wala Nini ila hiyo no anayosema ni ya rafiki yangu tu aliniomba nimpeleke dar mi nikaona haitakuwa sawa kwenda dar na mwanamke

Ni bora nimuungamishe na dada na Kwa sababu yeye dada ni mzoefu wa biashara hii itakuwa vizuri zaidi

Hata dada tukimpigia simu saivi kumuuliza hii kitu atawaambia kama nilivyo waambia hapa.

Simu ikapigwa na mzee mwenyew dada akajisahaulisha simu nikapewa Mimi nikamwambia yule dada × niliyekuambia mwende nae dar

Dada akajiongeza ukumbuke hapo hajapangwa

Akadakia hata Leo amenipigia anaulizia tunaenda lini mzee wake anauliza vipi Kuna shida kwani?

Maelezo ni mengi lakini Kwa kifupi
Sikukubali kabisa Wala msamaha sikuomba Wala kutingishwa hakunitingisha Tena.

Akanyoooka

Ila mzee akawa amejua akaniambia hakikisha simu Yako unafunga kabisa na umzuie asishike au kama atatumia asipokee simu Yako Wala kusoma msg zako akimaliza kutumia aendelee na simu yake.

Ni hivyo wakuu. Share hapa nww kisa chako uli
Pichani ni bibi akiniambia mwanaume haombi msamaha Bali husema yameisha basii jamani
Mkuu uliupiga mwingi ,mzee nae akajua ila akakupa na njia sahihi ya kupitia🙌
 
Mimi sijawahi shika simu y mwenza wangu, ili iweje sasa. Ni kukosa kujiamini. Huwezi mzuia mtu kuchepuka kwa kukagua simu yake kila mara. Halafu pia ni kosa kisheria kukagua na kujibizana na watu kwenye simu ambayo si yako.

Unaweza pata msala kwa mwenza wako kumtukana au kutishia mtu kwa kutumia simu yako.
Namimi Huwa nashangaa kabisa mtu kudili na simu ya mke wake Mimi Huwa ni emergency mno Tena muda mchache mno kushika simu yake

Nakumbuka mwanzoni ndo tumefunga ndoa akitongwa ananimbia nikampiga STOP kubwa.

Nikamwambia najua kutongozwa lazima utongozwe Hivi ni wajibu wako kujitambua kama mke wa mtu Mimi Sina muda wa kudili na simu Yako na kuku winda huo muda Sina jirinde mwenyew na kufata maagizo yangu

Siku ukikengeuka jua hakutakuwa na lugha nyingine utakayoniwmbia nikakuelewa kabisa.

Hii ikaisha hakuwahi nambia Tena labda itokee usumbufu Sasa kina midume ukiambiwa nimeolewa huwa haielew kwahiyo ni wajibu wangu ku block no maana yeye kwenye simu anajua vichache tu.
 
Namimi Huwa nashangaa kabisa mtu kudili na simu ya mke wake Mimi Huwa ni emergency mno Tena muda mchache mno kushika simu yake

Nakumbuka mwanzoni ndo tumefunga ndoa akitongwa ananimbia nikampiga STOP kubwa.

Nikamwambia najua kutongozwa lazima utongozwe Hivi ni wajibu wako kujitambua kama mke wa mtu Mimi Sina muda wa kudili na simu Yako na kuku winda huo muda Sina jirinde mwenyew na kufata maagizo yangu

Siku ukikengeuka jua hakutakuwa na lugha nyingine utakayoniwmbia nikakuelewa kabisa.

Hii ikaisha hakuwahi nambia Tena labda itokee usumbufu Sasa kina midume ukiambiwa nimeolewa huwa haielew kwahiyo ni wajibu wangu ku block no maana yeye kwenye simu anajua vichache tu.
Ni ujinga kukagua simu ya mtu. Hiyo sio account ya pamoja kusema kila mtu ana haki nayo.
 
Ukamuonyesha umwamba kabisa na kukana juu kama hujui kitu vile
Kama angekuwa na simu mkononi kwamba huyu ni nani Yako nakwann anitukane.

Hapo ningejitetea Kiaina na Bado nisingekubali vilevile kuwa ni mchepuko. Shida yake akijua nikiona alivyo nitarudi kuuliza Kwa undani na pia nikiona msg ndo kabisa nianguke miguuni mwake nitubu.

Ikawa tofauti na siwezi badirika naona wananishambulia kuliko hata mzee baba yangu 😂😂
 
Back
Top Bottom