Je uliwahi kufumaniwa na mke wako hata meseji(za mapenzi) kwenye simu Yako?

Je uliwahi kufumaniwa na mke wako hata meseji(za mapenzi) kwenye simu Yako?

Wewe sasa ndo unatujulia wanawake, achana na mtoa mada amesahau kiburi huishi kwa mpumbavu

Kwanza niliporudi nyumbani sikumkuta, simu sizioni, nikipiga anakata tu, nikajua tu hapa tayari mambo yameshatibuka.

Mbaya zaidi akaenda kwenye gari, akakuta Kuna simu ndogo Ina text zingine na tkt mbili za majina yetu. Hapakua na namna ningekataa.

Akaondoka na gari na bag yake akisema harudi Tena nyumbani na watoto anawaacha.

Baada ya kuomba sana tuonane, akasema Yuko Sleep way. Nikaacha gari Kwa askari wa SGA Makumbusho hata bila makabidhiano maalum ( hili ni balaa lingine nililiibua, gari ilipelekwa Oyster bay police).

Nilipofika mahali yupo tunaondoka huku naendesha sikuongea kitu, wakati huo analia tu na kutoa maneno ya uchungu. Nakumbuka nilisema tu naomba msamaha bila maelezo mengi huku naendesha kuelekea kanisani. Hadi wakati huo bag yake ipo kwenye gari na ameshikilia msimamo wake wa kutorudi nyumbani.

Nilijuafika wachungaji wameshaondoka ilikua kwenye saa mbili jioni. Akaniuliza Sasa unakuja kufanya Nini kanisani? Nikamwambia nataka niombewe...alijikuta anacheka Kwa sauti na kutamka, yaani ujinga wako ndio umeona uje kusumbua watu usiku huu?

Nikasema basi twende nyumbani, nipe muda wa mwezi mmoja nikatafute nyumba na Dada wa kazi Kisha ntakuja kuwachukua watoto. Kwa nilichokukosea, una haki ya kufanya chochote.

Nikasema hichi ulichokiona ni kitu kidogo sana, mie nna Pepo kama sio nguvu za Giza, nnakunywa pombe, balaa la wanawake siwezi kulielezea, huyu sio mimi. Alitoa macho kusikia nnakunywa pombe ( nilikua sijawahi hata kuonja, hata sikua na wanawake ila Sasa katika kusuluhisha, ikabidi nijipatie ubaya wote).

Nilifanikiwa kuondoka kurudi kazini, uzuri usiku japo kishingo upande kimasihara ikachukua mkondo wake.

Hapo balaa la gari niliyoiacha Makumbusho likaibuka. Liliunguruma Kwa wiki Moja nikafanikiwa kuichukua gari Kituo Cha polisi.
 
Sikutaka kuvutana sana Kwa jambo lipo wazi. Mtu mwenyewe ana misimamo kama Kapeace , akili nyingii, hapo ukiendelea kumletea ujinga ujinga kitu atakachokufanyia utajutia maisha Yako yote. Kwanza haongei sana Wala maneno mengi.

Hata wewe usifikirie ulishinda hiyo kesi, ulituliza vurumai tu lakini mapambano yanaendelea. Hiyo ni endless battle!
Huyo kilaza asikusumbue kama hawezi kuishi na mwanamke kwa akili anatumia ubabe ataishi na wanaume wenzie
 
Kuna watu wanakamatwa live kabisa. Kuna mkasa wa jamaa mmoja sitataja mkoa ila nilihusika sana kusuluhisha kile kisa. Jamaa kaenda club usiku kapiga pombe alafu kabeba mwanamke na kumfanya naye mapenzi kwenye gari. Kawasha gari hadi nyumbani, kaingia kalala, asubuhi anaamka choka mbya kwa pombe na lazima aende kibaruani, kama kawaida anampitisha mke wake kibaruani alafu yeye anaendelea.
Mke wa ndoa anaingia kwenye gari anakuta siti ya nyuma kuna mwanamke amelala uchi wa mnyama na michupa ya pombe kibao. Kumbe ule usiku jamaa baada ya kumgonga yule demu alimuacha kwenye gari akarudi club akaendelea kunywa, na akarudi naye nyumbani bila kukumbuka siti ya nyuma alimuacha yule mwanamke. Ilikuwa kesi kubwa sana kuwahi kukutana nayo maishani kwangu, ila yaliisha na wanaendeleza famili
Finally jamaa alikubali?
 
Kwanza niliporudi nyumbani sikumkuta, simu sizioni, nikipiga anakata tu, nikajua tu hapa tayari mambo yameshatibuka.

Mbaya zaidi akaenda kwenye gari, akakuta Kuna simu ndogo Ina text zingine na tkt mbili za majina yetu. Hapakua na namna ningekataa.

Akaondoka na gari na bag yake akisema harudi Tena nyumbani na watoto anawaacha.

Baada ya kuomba sana tuonane, akasema Yuko Sleep way. Nikaacha gari Kwa askari wa SGA Makumbusho hata bila makabidhiano maalum ( hili ni balaa lingine nililiibua, gari ilipelekea Oyster bay police).

Nilipofika mahali yupo tunaondoka huku naendesha sikuongea kitu, wakati huo angalia tu na kutoa maneno ya uchungu. Nakumbuka nilisema tu naomba msamaha bila maelezo mengi huku naendesha kuelekea kanisani. Hadi wakati huo bag yake ipo kwenye gari na ameshikilia msimamo wake wa kutorudi nyumbani.

Nilijuafika wachungaji wameshaondoka ilikua kwenye saa mbili jioni. Akaniuliza Sasa unakuja kufanya Nini kanisani? Nikamwambia nataka niombewe...alijikuta anacheka Kwa sauti na kutamka, yaani ujinga wako ndio umeona uje kusumbua watu usiku huu?

Nikasema basi twende nyumbani, nipe muda wa mwezi mmoja nikatafute nyumba na Dada wa kazi Kisha ntakuja kuwachukua watoto. Kwa nilichokukosea, una haki ya kufanya chochote.

Nikasema hichi ulichokiona ni kitu kidogo sana, mie nna Pepo kama sio nguvu za Giza, nnakunywa pombe, balaa la wanawake siwezi kulielezea, huyu sio mimi. Alitoa macho kusikia nnakunywa pombe ( nilikua sijawahi hata kuonja, hata sikua na wanawake ila Sasa katika kusuluhisha, ikabidi nijipatie ubaya wote).

Nilifanikiwa kuondoka kurudi kazini, uzuri usiku japo kishingo upande kimasihara ukachukua mkondo wake.

Hapo balaa la gari niliyoiacha Kwa Makumbusho likaibuka. Liliunguruma Kwa wiki Moja nikafanikiwa kuichukua gari Kituo Cha polisi.
Ulijitoa ufahamu ili akuonee huruma na kweli ulifanikiwa, mliambiwa tumieni akili sio mabavu na hii ndo akili yenyewe hakuna kitu kinatulainisha chap km mwanaume akitumia udhaifu wetu kujitetea hayo maigizo ya wachungaji usiku usiku mara una pepo aaah hata mimi ningelainika na ningeokoka kabisa ili nikusaidie
 
Mkuu hayo yte usemayo ni juu yake/Yao but msimamo wangu ni huo.

Kuhusu uchumi

Hayo ndo mnayatafutaga wenyewe yaani mnapenda mseleleko au 50/50.

Na ukifika hapo jua wazi huna mwanamke. Mwanamke ni mama wa nyumbani ni mlezi wa familia hayo ya kipato umeyatoa wapi?

Wazee wetu hawakuwa wajinga mkuu walijua hayo ndio maana wapo wote na mama Hana kipato chochote na anafuraha kwenye ndoa yake.

Mimi mwanamke akiniambia aanze kujighulikisha Nje na familia na mwambia achague familia ama kujishughulisha.
Kumbe ndio maana una jeuri yote hiyo mkeo ni mama anaesubiri uweke mkwanja mezani so inabidi tu akubaliane na lolote maana hana namna ingekuwa na kipato chake mkuu ungepata majibu. Hingera sana kwa kumfanya mkeo inferior hapo umewin sana
 
Ulijitoa ufahamu ili akuonee huruma na kweli ulifanikiwa, mliambiwa tumieni akili sio mabavu na hii ndo akili yenyewe hakuna kitu kinatulainisha chap km mwanaume akitumia udhaifu wetu kujitetea hayo maigizo ya wachungaji usiku usiku mara una pepo aaah hata mimi ningelainika na ningeokoka kabisa ili nikusaidie

Nikamwambia, hapa mtu wa kunisaidia ni wewe tu. Nipo kwenye dimbwi ambalo sijui ntatokaje na sijui kama naweza kujinasua.

Ila kama na wewe unaniacha, sitakulaumu Kwa sababu nimejitakia mwenyewe. Na Kwa huu mwendo hata kazi na mambo mengine sijui kama yanaendelea Kwa ufanisi.

Baadae ndio akaja kuniambia, Yale maneno yalimwingia akanihurumia mno...akaona sina pa kutegemea zaidi ya yeye ili nikae sawa.
 
Nikamwambia, hapa mtu wa kunisaidis ni wewe tu. Nipo kwenye dimbwi ambalo sijui ntatokaje na sijui kama naweza kujinasua.

Ila kama na wewe unaniacha, sitakulaumu Kwa sababu nimejitakia mwenyewe. Na Kwa huu mwendo hata kazi na mambo mengine sijui kama yanaendelea Kwa ufanisi.

Baadae ndio akaja kuniambia, Yale maneno yalimwingia akanihurumia mno...akaona sina pa kutegemea zaidi ya yeye ili nikae sawa.
Mkuu Mimi.kuyasema hayo basi kitanzi kimeshalengeshwa shingoni hapo Sasa naona Sina namna hata kumlamba kwenye kisigino naweza lkn sio hivihivi.SIWEZI.
 
Back
Top Bottom