The Monk
Platinum Member
- Oct 12, 2012
- 20,242
- 45,930
Wewe sasa ndo unatujulia wanawake, achana na mtoa mada amesahau kiburi huishi kwa mpumbavu
Kwanza niliporudi nyumbani sikumkuta, simu sizioni, nikipiga anakata tu, nikajua tu hapa tayari mambo yameshatibuka.
Mbaya zaidi akaenda kwenye gari, akakuta Kuna simu ndogo Ina text zingine na tkt mbili za majina yetu. Hapakua na namna ningekataa.
Akaondoka na gari na bag yake akisema harudi Tena nyumbani na watoto anawaacha.
Baada ya kuomba sana tuonane, akasema Yuko Sleep way. Nikaacha gari Kwa askari wa SGA Makumbusho hata bila makabidhiano maalum ( hili ni balaa lingine nililiibua, gari ilipelekwa Oyster bay police).
Nilipofika mahali yupo tunaondoka huku naendesha sikuongea kitu, wakati huo analia tu na kutoa maneno ya uchungu. Nakumbuka nilisema tu naomba msamaha bila maelezo mengi huku naendesha kuelekea kanisani. Hadi wakati huo bag yake ipo kwenye gari na ameshikilia msimamo wake wa kutorudi nyumbani.
Nilijuafika wachungaji wameshaondoka ilikua kwenye saa mbili jioni. Akaniuliza Sasa unakuja kufanya Nini kanisani? Nikamwambia nataka niombewe...alijikuta anacheka Kwa sauti na kutamka, yaani ujinga wako ndio umeona uje kusumbua watu usiku huu?
Nikasema basi twende nyumbani, nipe muda wa mwezi mmoja nikatafute nyumba na Dada wa kazi Kisha ntakuja kuwachukua watoto. Kwa nilichokukosea, una haki ya kufanya chochote.
Nikasema hichi ulichokiona ni kitu kidogo sana, mie nna Pepo kama sio nguvu za Giza, nnakunywa pombe, balaa la wanawake siwezi kulielezea, huyu sio mimi. Alitoa macho kusikia nnakunywa pombe ( nilikua sijawahi hata kuonja, hata sikua na wanawake ila Sasa katika kusuluhisha, ikabidi nijipatie ubaya wote).
Nilifanikiwa kuondoka kurudi kazini, uzuri usiku japo kishingo upande kimasihara ikachukua mkondo wake.
Hapo balaa la gari niliyoiacha Makumbusho likaibuka. Liliunguruma Kwa wiki Moja nikafanikiwa kuichukua gari Kituo Cha polisi.