KITU kilichonipa umaarufu O-LEVEL nilipendwa na mtoto mkali kuliko wote shule nzima (baba yake alikua mhindi mama yake muarabu), walimu, mabishoo, ma genius wa shule wote walimuimbisha dogo lakini dogo aligoma akawa ananielewa mimi tu,, (Pitia ID yangu kuna uzi nimesimulia kisa hiki unaitwa "KOSA LANGU")
Kilichonipa umaarufu baada ya kupendwa na uyu mtoto mkali, ni kwamba nilikua domo zege, dogo alijilengesha lakini wapi mzee sina habari, jamaa yangu alikua anakula rafiki yake, wote wanajadili pamoja na demu mwenyewe jinsi gani niwe na mtoto lakini wapi, mzee sina habari kichwani mwangu nilikua naiwaza man u, mpira na kutumikia altare kupiga chetezo.. .
Sasa siku moja katika harakati za hapa na pale skuli natembea mara paah mtoto uyu hapa anakuja mbele yangu, mimi ni nani bwana mpaka nikutane nae, mzee uyo nikakunja njia kwenda ofisi ya waalimu ile kuingia tu ndani nikakuta kupo kimyaa kumbe kulikua na kikao, ticha mmoja akaniuliza eenh vipi? mi lile wenge nikasema mwalimu ABC kanituma chaki kumbe lile wenge yule ticha alikuepo mle ofisini sikumuona akasema we dogo mi si nipo hapa.
Basi ticha alokua anafukuzia yule dg na anajua mi ndio kikwazo akadakia show wazee fimbo nilizochezea pale kama ingekua ni mtaji basi leo hii ningekua milionea, nilivopigwa nikajua kesi imeisha kumbe wapi bwana kesho yake parade yule ticha akaja kaniita kama wewe ni kijana upo kidato cha nne na kuna demu unamuogopa yupo kidato cha kwanza njoo hapa mbele utoe morning speech, mzee nikakaza wapi ticha kanifuata kanishika mkono mpaka pale mbele akani dis kinoma afu akanipachika jina la Domo gundi, mwisho akanipa adhabu ya kutoa morning speech wiki nzima, na viranja walivokua wananiita Welcome domo gundi ilifanya niwe maarufu sana shule nzima
Ilikua mwaka 2010 au 11 kitu kama hicho, Leo hii uyo dada ni best yangu sana sema kila tuki chat ananitania sana, mwisho wa siku tumebaki kua marafiki wakubwa na mimi niliishia kua mpenzi mtazamaji lakini maarufu.
Sent using
Jamii Forums mobile app