Huku duniani tumekuja kuchuma ila matumizi ya kile tulichokichuma tutakuta huko maisha ya peponi.
Kila mmoja atapata neema ya pepo kulingana na thawabu alizozichuma huku duniani.
Mitume ya Mwenyezi Mungu ipo mingi sana ila wapo wale mitume ambao daraja lao ni kubwa zaidi kuliko wengine mfano Muhammad, Issa, Ibrahimu, Mussa nk.
Na hao hao mitume wakubwa nao madaraja yao ni tofauti pia, na kwa kuwa peponi hakuna namna utafanya kuongeza daraja lako, ina maana kuwa maisha yako yatakuwa ni yale yale, raha ni zile zile, hakutakuwa na uwezo wa kumpiku mtu aliyekuzidi pepo/daraja.
Hivyo je hao mitume umeshawahi kufikiria wakiona wivu baina yao nini kitatokea?
Au je hao mitume kutaka daraja la zaidi na zaidi nini kitatokea.
Maana hata Ibilis alikuwa mcha Mungu sana kwa miaka mingi sana lakini mwisho wa siku kiburi kikamponza kwa kujiona bora zaidi na kuashia kupata laana.