Ngoja nikupe hoja za kuonesha Mungu hayupo 👇
Watoto wachanga wasio elewa chochote kile, Kuzaliwa na matatizo kama unjiti, vichwa vikubwa, uchizi na kasoro nyingine nyingi, Ni uthibitisho wa kwamba Mungu Mkamilifu mwenye kuumba binadamu wakamilifu kimwili na kiakili tangu wawapo tumboni mwa mama zao Hayupo.
Majanga ya asili kama radi, mafuriko matetemeko ya ardhi na vimbunga yanayo Ua watu wasio na hatia mpaka watoto wachanga wasio na ufahamu wowote ule, Ni uthibitisho wa kwamba Mungu mwenye huruma na upendo Hayupo. Mfano tetemeko la Syria na Uturuki lililo ua maelfu ya watu na watoto.
Uwepo wa uovu, mabaya, maasi na dhambi Ni uthibitisho wa kwamba Mungu muweza wa yote na mwenye kujua yote tangu mwanzo na hata milele Hayupo. Angekuwepo ange dhibiti maovu haya tangu mwanzoni.
Watu kufariki kwenye Ajali mbalimbali licha ya kumwomba Mungu awalinde wawapo safarini na hata kabla ya ajali yenyewe kutokea wengine hulia na kumwomba Mungu sana azuie ajali hiyo lakini hakuna kinachotokea, Mfano kuzama kwa meli, kuanguka kwa ndege, Ajali za mabasi, na vyombo vingine vya moto. Ni uthibitisho wa kwamba Mungu huyo anaye ombwa Hayupo.
Walemavu na wagonjwa mbalimbali wenye magonjwa yasiyo tibika kuendelea kuteseka na magonjwa yao, Licha ya kusali kila mara na kuomba Mungu wapone, Ni uthibitisho wa kwamba Mungu hayupo.