Je, umewahi kujiuliza kuhusu ukimya wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na uuzwaji wa Bandari za Tanganyika?

Katika kichwa chako cha habari ondoa neno "UUZWAJI" Hakuna bandari inayouzwa unachofanya ni uchonganishi kwa umma.
Bosi usinifokee, naumia sana na nchi yangu kuliko siasa zenu, narudia tena sijaandika uuzwaji kwa bahati mbaya, au kwa kupotosha umma. nimeandika kwa tafsiri ya kisheria ambayo tayari nilishaitolea maelezo huko nyuma katika maandiko mengine.

narudia tena swali lako lilipaswa kuwa kwa nini unasema uuzwaji? ningekujibu kistaarabu kadili nilivyosoma mkataba, kwa sababu unajifanya ujuaji kaa na maana yako, sisikilizi wanasiasa wanitafsirie mkataba, kama wewe nimesoma na kuuelewa ndio maana natoa tafsiri kadili ninavyoelewa na ilivyo katika sheria. tofauti yako mimi na wewe ni tuna line of diference, your making politics and am not a politician.

usinifundishe eti niseme imekodishwa kwa sababu hakuna bei iliyowekwa au nieleze imeandikwa shilingi ngapi? sasa , kwani umeambiwa imekodishwa kwa shilingi ngapi?, au umeelezwa bei ya ukodishwaji? au imekodishwa bure?

nasisitiza ule ni uuzwaji, na sio ukodishaji, kama issue ni pesa hata kukodisha wangesema imekodishwa kwa shilingi ngapi. period
 
Eleza wewe, bandari imefanywa nini?

Nakubaliana nawe kuwa haijauzwa maana kama ingekuwa imeuzwa, angalao tungeambiwa imeuzwa kwa bei gani.

Hatuwezi kusema imekodishwa maana kama ingekuwa imekodishwa, tungeambiwa inakodishwa kwa dola ngapi, na imekodishwa kwa kipindi gani.

Kwa hiyo, kwa ujumla, kwa lugha rahisu, IMEPOR
ahsante kwa mjibu mazuri mkuu mpigania nchi mwenzangu
 
Bosi usinifokee, naumia sana na nchi yangu kuliko siasa zenu, narudia tena sijaandika uuzwaji kwa bahati mbaya, au kwa kupotosha umma. nimeandika kwa tafsiri ya kisheria ambayo tayari nilishaitolea maelezo huko nyuma katika maandiko mengine.

narudia tena swali lako lilipaswa kuwa kwa nini unasema uuzwaji? ningekujibu kistaarabu kadili nilivyosoma mkataba, kwa sababu unajifanya ujuaji kaa na maana yako, sisikilizi wanasiasa wanitafsirie mkataba, kama wewe nimesoma na kuuelewa ndio maana natoa tafsiri kadili ninavyoelewa na ilivyo katika sheria. tofauti yako mimi na wewe ni tuna line of diference, your making politics and am not a politician.

usinifundishe eti niseme imekodishwa kwa sababu hakuna bei iliyowekwa au nieleze imeandikwa shilingi ngapi? sasa , kwani umeambiwa imekodishwa kwa shilingi ngapi?, au umeelezwa bei ya ukodishwaji? au imekodishwa bure?

nasisitiza ule ni uuzwaji, na sio ukodishaji, kama issue ni pesa hata kukodisha wangesema imekodishwa kwa shilingi ngapi. period
samahani chief, nilikuwa najibu uliyemjibu,
 
Wa kuwapuuza tu hao, wanataka mwanasheria wa serikali ajiropokee tu kama wao? Ana utaratibu wake na muda wake ukifika ataongea km kuna ulazima wowote
Kiongozi kutoa ufafanuzi kwa wananchi kwa wakati ni muhimu na ni wajibu. Hawezi kuacha nyumba inateketea kwa moto eti aje kuzima kwa wakati wake. Tunataka nchi yetu iendelee kuwa kisiwa cha amani na utengemano.
 
Moto huo uko wapi unaoteketeza nchi hii?!!! Haupo na wala hakuna chanzo (source) cha uwepo wa moto huo. Kilichopo ni mpango kabambe na wa kisasa wa naendeleo ya kiuchumi ambao hata wawakilishi wetu bungeni wameona tija kubwa iliyopo ndo maana wakapitisha......mpango km huo hauwezi kuwa chanzo cha moto sababu watanzania wanataka maendeleo.

Kakikundi kadogo ka wezi na mafisadi na wenye chuki za kikabila na dini kenye wasomi uchwara kadhaa wanaohaha kutafuta fursa na umaarufu kwa watz walioonyesha kuwakataa tayari huku mtaani, hakina hadhi ya kuitwa moto wala vuguvugu........watashindwa kuitikisa nchi hii hata wajitahidi vp! Watz wapo macho na wanajua wanachokitaka. Hivyo futa kauli kuwa kuna moto; hakuna mtz mwenye akili timamu atakayeabzisha moto kwa ajili ya wachache hao waovu!!
 
Lakini mwanasheria mkuu kukaa kimya ni udhaifu.yeye anafanya kazi kwa mujibu wa sheria na siyo matakwa ya rais.kwa jambo kubwa kama hili la bandari inatakiwa na yeye aitishe kikao na waandishi wa habari kutoa ushauri wake na siyo kukaa kimya.
 
Moto huo uko wapi unaoteketeza nchi hii?!!! Haupo na wala hakuna chanzo (source) cha uwepo wa moto huo. Kilichopo ni mpango kabambe na wa kisasa wa naendeleo ya kiuchumi ambao hata wawakilishi wetu bungeni wameona tija kubwa iliyopo ndo maana wakapitisha......mpango km huo hauwezi kuwa chanzo cha moto sababu watanzania wanataka maendeleo.

Kakikundi kadogo ka wezi na mafisadi na wenye chuki za kikabila na dini kenye wasomi uchwara kadhaa wanaohaha kutafuta fursa na umaarufu kwa watz walioonyesha kuwakataa tayari huku mtaani, hakina hadhi ya kuitwa moto wala vuguvugu........watashindwa kuitikisa nchi hii hata wajitahidi vp! Watz wapo macho na wanajua wanachokitaka. Hivyo futa kauli kuwa kuna moto; hakuna mtz mwenye akili timamu atakayeabzisha moto kwa ajili ya wachache hao waovu!
Moto huo uko wapi unaoteketeza nchi hii?!!! Haupo na wala hakuna chanzo (source) cha uwepo wa moto huo. Kilichopo ni mpango kabambe na wa kisasa wa naendeleo ya kiuchumi ambao hata wawakilishi wetu bungeni wameona tija kubwa iliyopo ndo maana wakapitisha......mpango km huo hauwezi kuwa chanzo cha moto sababu watanzania wanataka maendeleo.

Kakikundi kadogo ka wezi na mafisadi na wenye chuki za kikabila na dini kenye wasomi uchwara kadhaa wanaohaha kutafuta fursa na umaarufu kwa watz walioonyesha kuwakataa tayari huku mtaani, hakina hadhi ya kuitwa moto wala vuguvugu........watashindwa kuitikisa nchi hii hata wajitahidi vp! Watz wapo macho na wanajua wanachokitaka. Hivyo futa kauli kuwa kuna moto; hakuna mtz mwenye akili timamu atakayeabzisha moto kwa ajili ya wachache hao waovu!!
jibu swali, nenda kwenye hoja mama
 
Utangulizi:
Ukisoma katiba ya JMT ibara ya 59 (1) imeanzisha ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali, na ibara ndogo ya (3) ya ibara hiyo ya 59, inaeleza wajibu mkuu ni kuishauri serikali katika mambo yote yanayohusu sheria, zaidi sana ibara ya 59 (5) kwa hadhi ya ofisi yake mwanasheria mkuu amepewa hadhi ya ubunge, kwa kifupi ni Mbunge wa JMT.

ukienda zaidi kusoma kwa pamoja sura ya 268 ya sheria ya ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali kazi na wajibu wake yaani, the office of the Attorneys General ( Discharge of Duties Act), Cap. 268, hasa kifungu cha 8 1) (a), (section 8 (1) (a) ya sheria hiyo inaeleza kazi mbalimbali za mwanasheria mkuu, ikiwa pamoja na kushauri serikali kuu, serikali za mitaa, wizara mbali mbali, taasisi za serikali, mashirika ya umma.

Nimefanya tafiti kidogo kwenye tovuti yao, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AGCTZ) | Mikataba na Makubaliano, utagundua na utaona wana hadi department (division ya mikataba) imegawanyika katika sehemu tatu yaani; mikataba ya ununuzi wa umma, mikataba ya makubaliano ya kimataifa na mikataba ya uwekezaji wa maliasili.

Je, mwanasheria wa taasisi au wizara ana mamlaka ya kuishauri serikali kuingia kweye mikataba ya kimataifa?

1.
Kulingana na katiba yetu na sheria zetu tajwa hapo juu ni hapana. lakini kumekuwa na mwanasheria anaitwa Hamza Johari, kutwa kuchwa anatolea ufafanuzi kuhusu mikataba walioingia kati ya JMT na Manispaa ya Dubai, lakini kwangu mimi nadhani anatukosea watanganyika, kwa sababu kusoma kwangu sijaona mamlaka yake, au anawajibika vipi kwenye taifa letu la mikataba aliyoiingiza yeye katika nafasi yake, au utueleze ana uhusiano gani na mikataba hiyo?

Je, Spika wa Bunge alikuwa sahihi, kuchukua nafasi ya mwanasheria mkuu bungeni?
2. Jibu ni hapana
, katika kuongoza nchi, kuna mihimmili mitatu, yaani serikali, bunge na mahakama, kwa muktadha huo serikali ilipeleka mkataba ule kwenye mhimili wa Bunge, na kazi ya Bunge ni kuangalia nini, serikali imeleta, je ni kwa manufaa ya nchi na wananchi wake?, na kama wawakilishi wa wananchi, wana wajibika kuangalia maudhui yake na faida zake, kwa kuihoji serikali yaani, (check and balance, )hiyo Spika aliingilia kazi ya serikali, na kwa kuwa ilihusu mikataba na mikataba ni sheria basi ulikuwa ni wajibu ambatano wa mwanasheria mkuu wa serikali kutolea ufafanuzi, kwa nini serikali wameridhia, kifungu fulani wana nini wanatarajia. maana waliokuwa kwenye negotiation ya mkataba huo ndio "wao" kwa maana wenye mamlaka hayo.
kwa hiyo, kwa kuingilia nafasi ya mwanasheria mkuu, spika analitaarifu taifa alichukua, au alikuwepo wakati wanakubaliana (negotiation), na hivyo anajua maudhui ya nini kinachoelezwa.

3. Je, ukimya wa mwanasheria mkuu unamaanisha nini? (mtazamo binafsi)
katika dhana ya uwajibikaji, alipashwa ajihudhuru kwa upendo, si kwa sababu ameshindwa kazi, lakini kwa sababu ya mazingira hayo hapo juu. yaani bungeni na mitaani;

(a) inaonekana hakushirikishwa vizuri kadili ipaswazo kwa mujibu wa katiba na sheria, kutoa ushauri wa kisheria kuhusu mkataba huu, ndio maana sehemu zote ambazo anapashwa kuongea ameaamua kuchagua kukaa kimya, bungeni ni kama alinawa mikono. kuashiria sihusiki na kinachoendelea malizaneni wenyewe.

(b) huku mitaani, Hamza Johari amekuwa ndio mwanasheria mkuu, akitolea ufafanuzi wa kwa nini waliamua kuingia mkataba.

4. Je, nani alimshauri Rais wa JMT kuridhia kuingia makubaliano hayo ya uwekezaji?
Bado Sina Jibu, najua wazi kuwa Rais wetu si mwanasheria, sina shaka lazima atakuwa kaomba ushauri kabla ya kutoa ruhusa ya kuiingiza nchi katika mkataba huu aliomba ushauri wa kisheria,

Je, kama aliyemshauri ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, basi ndio alipaswa kuwa msemaji mkuu wa kadhia yote iliyotufikisha hapa, au kama si yeye nadhani wasiwasi wangu unarudi kwa mwanasheria Hamza Johari, Je ni nani hasa na ana interest gani katika mkataba huu?

5. Nani alaumiwe? na nini kifanyike?
kwanza sitaacha kuwalaumu waandishi wa habari, kwani wametuangusha sana, katika tafiti zote za habari kabla hujaenda site, lazima ujue key informers (nani atakupa habari sahihi?), si kila mtu anapaswa kuulizwa kwenye vitu ambavyo vinaitaji majibu ya moja kwa moja, mpaka sasa nimeona midahalo, magazeti, radio, tv, kwa bahati mbaya sana wanaoalikwa si watu sahihi.

Nimalizie, hapo.
In law concept "silence means admit or admission of the stated fact"
 
Huyo binti ataitumbukiza nchi kubaya hiyo nafasi haiwezi kabisa
 
Kama hukuandamana wewe ni mnafiki
ndio maana upo uko jamii forum unatetea chama chako mama hii ni digitalization age kuandamana ni analogia inaweza kuwa altenative ya digitalization to supliment the desired effects ,

we shall speak out through out and the massage is sent to the whole world, kwamba Tz ilishawahi kuwa na chief mangungo wa msovero katika karne ya 21, ndio maana wenzako wameenda kushitaki instagram, kuomba poo, kama digital ni mbaya kaandamane wewe.

digitalization msg ni zalidi ya physical maandamano.

ndio maana hamuishi kutetea upuuzi wenu,
 
Samia alikuwa anawahadaa na maridhiano feki kumbe ilikuwa ni gia ya kuwapumbaza auze nchi.

Ndio maana mimi kila siku nililuwa nawauliza machadema humu kwamba mnaridhiana kitu gani? Sikuwahi kupewa jibu.

Jiulizeni kwanini Ndugai alitoka hadharani kutamka yale kisha hangaya akaja kumkaripia mbele ya hadhara hadi akajiuzulu?
 
Kama kwenye ule mjadala wa juzi sikuona chochote cha maana alichosema Rostam, heri kutila mkumbo ni mwanasiasa, lakini Rostam hakustahili kuwa pale , aheri wangemuweka lema au zitto.
Inawezekana Usichokijua ni kwamba huyu Rostam ndiyo yupo katikati ya hilo deal na hivi anahangaika kuwa-brainwash Watanzania kupitia media mbalimbali na midahalo ya kutengenezwa kama hii. na kuna muda wanataka kupenyeza agenda za kidini ili kushinikiza wenye maamuzi katika jambo hili waamue katika mlengo huo/ au wale wanaopingana na vipengele vya mkataba basi waonekane hawana hoja za msingi zaidi ya msukumo wa udini au kuwatisha wasiendelee na mjadala. Ukiangalia kwa umakini wote wanaotaka kulibariki jambo hili hawataki kabisa kuongelea vipengele vya mkataba husika, sanasana unakuta wanaongelea nadharia tu za faida ambazo kimsingi hazijawa stated popote kwenye mkataba husika.
Nafikiri watanzania wameona na tuwashuru wale wote walioweza kuangalia mkataba kwa jicho la tofauti kwakweli wamewasadia sana Watz. na hasa kama yupo alievujisha mkataba huo kwenye mitandao huyu anastahili pongezi zote.
 
Samia alikuwa anawahadaa na maridhiano feki kumbe ilikuwa ni gia ya kuwapumbaza auze nchi.

Ndio maana mimi kila siku nililuwa nawauliza machadema humu kwamba mnaridhiana kitu gani? Sikuwahi kupewa jibu.

Jiulizeni kwanini Ndugai alitoka hadharani kutamka yale kisha hangaya akaja kumkaripia mbele ya hadhara hadi akajiuzulu?
Katiba mpya bora ni muhimu ! Ili kuepuka makaripio mengine huko mbele ya safari !!
 
Inawezekana Usichokijua ni kwamba huyu Rostam ndiyo yupo katikati ya hilo deal na hivi anahangaika kuwa-brainwash Watanzania kupitia media mbalimbali na midahalo ya kutengenezwa kama hii. na kuna muda wanataka kupenyeza agenda za kidini ili kushinikiza wenye maamuzi katika jambo hili waamue katika mlengo huo/ au wale wanaopingana na vipengele vya mkataba basi waonekane hawana hoja za msingi zaidi ya msukumo wa udini au kuwatisha wasiendelee na mjadala. Ukiangalia kwa umakini wote wanaotaka kulibariki jambo hili hawataki kabisa kuongelea vipengele vya mkataba husika, sanasana unakuta wanaongelea nadharia tu za faida ambazo kimsingi hazijawa stated popote kwenye mkataba husika.
Nafikiri watanzania wameona na tuwashuru wale wote walioweza kuangalia mkataba kwa jicho la tofauti kwakweli wamewasadia sana Watz. na hasa kama yupo alievujisha mkataba huo kwenye mitandao huyu anastahili pongezi zote.
kuna haja ya kuwa na Rais wa Tanganyika katika kusimamia rasilimali za watu wa tanganyika
 
Haya yote chiefs of contract negotiation .. Lord denning na covax wanakuja kutolea ufafanuzi juu ya hoja zako mkuu!!

Back
Top Bottom