Je, umewahi kukutana na mtumiaji wa JF katika maisha ya uhalisia (Jamii)?

Je, umewahi kukutana na mtumiaji wa JF katika maisha ya uhalisia (Jamii)?

Habari za muda huu wanajamvi!

Je, umewahi kukutana na mtumiaji wa Jamii Forums katika maisha ya uhalisia (Jamii)?
🔹 Ulijisikiaje?
🔹 Ulijitambulisha kuwa na wewe ni mwanachama, au ulifanya kama hauijui kabisa?
🔹Baada ya kujitambulisha mlikuwa na mazungumzo ya aina gani?

Nimeuliza hivi kwa maana watumiaji wengi wa JF hutumia huu mtandao kwa Siri sana

Share nasi uzoefu wako! 📢👇
Naamini kila mtu ana hadithi ya kipekee ya kusimulia.

#JamiiForums #Jamii #Uhalisia #UzoefuWako
Wengi mno
 
Kabisa, wanawakosesha wengine uhondo.
Sahv asilimia kubwa ya wadada na Id za kike wamefunga Pm zao.
Sio kama wanapenda, la hasha! ni kutokana na jinsi matumizi ya mitandao inatumiwa ndivyo sivyo.

Zamani tulikuwa tunakutana pasi na shaka,ila kwa sasa uoga ni mwingi mno
Na uaminifu umebaki kwa wale tunaowafahamu personal tu.
Naomba unifungulie.

Kumbuka Mimi ni mtu mwema.
 
Kwa nini mkuu iwe vizuri usifamike?
Unakuwa huru kueleza mambo kwenye majukwaa unakuwa open na honest kwenye discussion

Kwa mfano member anayejulikana na wengine hawezi kuwa huru kuzungumzia baadhi ya mambo akitumia ID inayofahamika na wengine. Lazima kuna mambo ili afunguke anaruka na ID ambayo hawaifahamu

Kuna baadhi ya nyuzi humu watu wanazipost kwa sababu tu hakuna anayewafahamu kwa ID wanazotumia kwa mfano nyuzi za matatizo ya kifamilia, ndoa, magonjwa, kuomba ushauri n.k Na hilo linaongeza participation

Kwa sababu za kiusalama member ambaye hajulikani na members wengine anafeel safer hata kuchangia mijadala ambayo ni mizito kwa taifa. Wengine humu kwa sababu ya kujulikana wanajikuta lazima walogin account ambayo watu hawamfahamu ili accoment

Kihalisi kwenye social media or forums yoyote haitakiwi watu wakufahamu kwa ID yako halisi



 
Unakuwa huru kueleza mambo kwenye majukwaa unakuwa open na honest kwenye discussion

Kwa mfano member anayejulikana na members wengine hawezi kuwa huru kuzungumzia baadhi ya mambo akitumia ID inayofahamika na wengine lazima kuna mambo ili afunguke anaruka na ID ambayo hawaifahamu

Kuna baadhi ya nyuzi humu watu wanazipost kwa sababu tu hakuna anayewafahamu kwa ID wanazotumia kwa mfano nyuzi za matatizo ya kifamilia, ndoa, magonjwa, kuomba ushauri n.k Na hilo linaongeza participation

Kwa sababu za kiusalama members ambaye hajulikani na members wengin anafeel safer hata kuchangia mijadala ambayo ni mizito kwa taifa. Wengine humu kwa sababu ya kujulikana waajikuta lazima walog account watu hawamfahamu ili accoment

Kihalisi kwenye social media or forums yoyote haitakiwi watu wakufahamu kwa ID yako halisi
Naunga mkono hoja yako mkuu, ni kweli kabisa kuna vitu unakua hauna uhuru navyo kuchangia.
 
Hapana.
Sisi wanawake tuna maadui wengi humu.
Kwanza kwetu wanawake kwa wanawake na pia wanawake kwa wanaume.
Kuna ishu pia ilitokea, mwanamke kampa mwanaume picha ya mgomvi wake wa kike ili mwanaume aifungulie mada
Hapo mwisho wa maelezo yako unaweza kuwa umeelewa nilichomaanisha...Mwanaume kutoa picha za mgomvi wake ili iweje...

Ukifuatilia hata Drama nyingi humu wanaume ndiyo huwa wanazileta..kaenda kakutana na KE wa JF anarudi jukwaani kuanza kumtoa kasoro na mengineyo....kitu ambacho kwa KE wa JF ni nadra sana kukiona
 
Back
Top Bottom