Je, umewahi kukutana na mtumiaji wa JF katika maisha ya uhalisia (Jamii)?

Je, umewahi kukutana na mtumiaji wa JF katika maisha ya uhalisia (Jamii)?

1.2019 nipo kwenye Coaster natoka Arusha kwenda Moshi...Nilikaa ile siti karibu na mlangoni...nipo JF kuna Uzi mmoja ulikuwa hot sana na Dada mzuri Heaven Sent kuna ushauri alikuwa anautoa kwenye hiyo mada..nikawa nafuatilia kwa makini sana wakati huo sikuwa active sana hapa jukwaani...kufika Machame road kuna Abiria akashuka Mkaka( si haba)😃wakati anashuka akaniambia kumbe wewe ndiyo Makiseo( ID yangu ya mwanzo).

2. Kibaruani kwangu...Kuna mmojawapo alinibamba...Kipindi App ikiwa ipo poa...Ila hakuona ID...Akaniambia kumbe Familia😄
Yaani nilivyoshtuka hapa, nikajua ulinichungulia kwenye coaster afu hukunishtua daah🤣🤣🤣
I'm humbled Maki🙏🙏

Btw ulikuwa uzi gani huo kama unaweza kuumbuka?

Naamini husiano lako linaendelea vizuri kabisa; mimi nalifurahia tu bila sababu
 
Jf ina watu wa maana sana

Nimepata wateja wa kutosha huku.Asanten sana kwa kuwa sehemu ya biashara yangu.

Nna washkaj pia ambao ni members ilaa huwa hatuna story nyingi kuhusiana na JF japo tunajuana tupo huku.

Ilaa kuna watu mnajua kuzificha ID zenu🙌.
 
Mambo ya ndoa, mkewe alikuwa nyanda za juu kusini huko sijui ndio kisa kilianzia huko. Uzi wake wa msiba umo humu jf ila siukumbuki title yake, unaweza utafuta unaelezea mkasa wake. Nilisikitika sana kwa kifo chake ukizingatia ni mtu niliyekwisha muona ana kwa ana. I think id yake ilikuwa shayo ama shio, sina uhakika bado jina limenitoka
Aisee nakumbuka hiyo story ya huyo kaka
 
Habari za muda huu wanajamvi!

Je, umewahi kukutana na mtumiaji wa Jamii Forums katika maisha ya uhalisia (Jamii)?
🔹 Ulijisikiaje?
🔹 Ulijitambulisha kuwa na wewe ni mwanachama, au ulifanya kama hauijui kabisa?
🔹Baada ya kujitambulisha mlikuwa na mazungumzo ya aina gani?

Nimeuliza hivi kwa maana watumiaji wengi wa JF hutumia huu mtandao kwa Siri sana

Share nasi uzoefu wako! 📢👇
Naamini kila mtu ana hadithi ya kipekee ya kusimulia.

#JamiiForums #Jamii #Uhalisia #UzoefuWako
JF ya zamani watu walikuwa wanaandika nondo haswaa tena zile za ndaaaani kuhusu serikali,, ila JF ya siku hizi ni ka Facebook tu, haina haja ya kujificha.
 
Habari za muda huu wanajamvi!

Je, umewahi kukutana na mtumiaji wa Jamii Forums katika maisha ya uhalisia (Jamii)?
🔹 Ulijisikiaje?
🔹 Ulijitambulisha kuwa na wewe ni mwanachama, au ulifanya kama hauijui kabisa?
🔹Baada ya kujitambulisha mlikuwa na mazungumzo ya aina gani?

Nimeuliza hivi kwa maana watumiaji wengi wa JF hutumia huu mtandao kwa Siri sana

Share nasi uzoefu wako! 📢👇
Naamini kila mtu ana hadithi ya kipekee ya kusimulia.

#JamiiForums #Jamii #Uhalisia #UzoefuWako

JF is a zombies world. Utakuta mtu anamtukana baba mkwe. Binti anamfokea mama yake kama mke mwenza.
 
Kuna mada moja ililetwaga humu miaka kama 4 au 5 iliyopita
Kipindi hiko humu Jf kila mwanamke anajiita pisi
Jamaa akaomba mchezo na pisi moja pm, akakubaliwa, kumbe bwana ulikuwa mchongo.
Yule dada kafika lodge kumbe jamaa kategesha camera chumbani.
Yule dada hatakuja kusahau ile aibu halafu wote tulikuwa tunamuona bonge la demu na mkali balaa hapa jukwaani, kumbe hakuna kitu na ni aibu sana.
Pia kosa kubwa alilofanya yule dada ni kuchati kupitia Pm mpaka sura yake.
Jamaa aliscreenshot kisha akaja na uzi wenye naked video ya yule dada pamoja na picha zake.
Jamaa alikula life ban na ile Id ya yule dada last seen yake imesimama July 2019 mpaka leo.

Kwahiyo hizi ndizo sababu za wengi kukataa kufahamika
Demis
 
Habari za muda huu wanajamvi!

Je, umewahi kukutana na mtumiaji wa Jamii Forums katika maisha ya uhalisia (Jamii)?
🔹 Ulijisikiaje?
🔹 Ulijitambulisha kuwa na wewe ni mwanachama, au ulifanya kama hauijui kabisa?
🔹Baada ya kujitambulisha mlikuwa na mazungumzo ya aina gani?

Nimeuliza hivi kwa maana watumiaji wengi wa JF hutumia huu mtandao kwa Siri sana

Share nasi uzoefu wako! 📢👇
Naamini kila mtu ana hadithi ya kipekee ya kusimulia.

#JamiiForums #Jamii #Uhalisia #UzoefuWako
Mimi sijawahi
 
Kuna ki IST Cha mshikaji wangu mmoja huwa tunapitianaga kwenda Job/ mishe mishe.

Huwa asubuh jamaa anasanya 2500 kariakoo siku moja mwezi ulio pita tulimpakiza dada mmoja kavaa full HIJABU tumeenda nikiwa nimekaa nae siti ya nyuma nikaona ana soma vitu jamii forum.

Tulikua watatu nyuma Mimi na jamaa mmoja na huyu dada ikanibidi nikate story na jamaa nianze kuongea na bi dada.

Maongezi.

Mimi: mshangao kumbe upo jamii forum.

Dada: ndio nipo muda tuu.

Mimi; nimeshangaa kuona mdada Kama wewe unamfaham jamii forum

Dada: nipo kitambo Mimi ni memba naendelea Sana kusoma soma nyuzi tofauti tofauti.

Tukaanza kujadili member mbali mbali akamtaja mshana jr, gwajima, gentamicin, faizafoxy n.k

Piga story Sana akasema wasomi, makabwela na viongozi na watu mbali mbali wengi na wapo Jf tunapigana vikumbo.

Huyu dada alikua amevaa HIJABU fully.

NB.
Pia Kuna washikaji baadhi hapa Jf nafanyanao business tupo kwenye field moja ya pharmaceutical industry.
Mkuu habari.....

kindly, ulichapisha comment kwenye uzi mmoja ukisema utaandaa baadhi ya info za pharmaceutical industry... Nauliza ulichapisha huo uzi if yes naomba nitag nikaupitie.. good luck
 
Najua kuna ambao wanakutana kwa matukio maalum.
Ila si ile ya ghafla kwenye daladala au sehemu ya mkusanyiko.
Watu wengi sana simu zao naona zina App ya Jf, na wanafungua kisirisiri😂😂 wakiwa kwenye halaiki za watu🤣
Mimi nna hii app nafungua kwa uwazi bila kuogopa nimeifatilia jamii forum toka nipo form one, mpaka sasa kwahiyo nipo confidently kuingia na kutoka..
 
Back
Top Bottom