Je, umewahi kula mnyama ama wadudu gani Hadi ukajisemea nilikuwa wapi siku zote hizo? Nimekula wanyama wengi sana.

Kuna wanyama ukila nyama yake ni sumu..

Unazungumziaje hilo
Ni kweli mkuu. Nakumbuka hata siku tunakula kenge, jamaa mmoja akatutisha kwamba tusitafune mifupa yake ikikuchoma mwili unatutumuka!

Kuna mahala nilishudia mchina kafa mara baada ya kula nyoka aina ya kifutu!
Ikasemekana kwamba alikosea vipengele namna ya kumuandaaa.

Kuna heresay nyingine kwamba wakati wa kula mbayuwayu inatakiwa uwe unakimbiakimbia coz ndo nature yake.

Na hata unapokula pimbi ili utamu ukoleee na kunoga, nenda kamlie kwenye miamba huku ukiwa una rukaruka toka jiwe moja hadi jingine!
 
Utakuwa na harufu ya mwili ya asili mbaya sana. Unakula vitu vya ajabu
 
Kuna hii nyingine sijui ni uroho au kutaka kuingia kwenye kitabu cha guiness!

Wajita wanakula wadudu flani wadogo wadogo jamii ya mbu. Wenyewe wanaita masami.
Ukamataji wake ni kipengele. Wanachukua kalai wanalilowanisha maji kisha wanaanza kupunga hewani kipindi hao wadudu wanapaa!

Na kuna kabila moja wanaitwa Wanguu-Wajumbi, wao wanakula wadudu flani jamii ya "dudu washa" ila shariti wapatikane kwenye miti ya mikarati.

Funga kazi ni Waluguru, wao hula panzi flani wazubaifu/mazoba wanaitwa ngeda au mbulumundu. Wanakuwa wa kijani. Hupatikana kwa wingi kipindi cha masika wanapenda kutembea kundi au wawili wawili. Hawawezi kupaa na mara zote utawakuta njiani wamezubaa.
Usukumani wanaitwa "kafula"

Wamakonde salute kwenu. Mnakula konokono wale wenye utelezi. Wenyewe hujisifia eti wana nyama nzuri kama firigisi ya kuku!
 
Watu ni walafi aiseeee!
 
siku moja tukiwa chaka tulikua tumepigika ile mbaya alafu njaa ilikua inatuhuma vibaya mno. unga ulikuwepo wa kutosha tatizo ilikua ni mboga akuna. mwana mmoja kutoka umakondeni akasema yani tunapata shida ya bure wakati apo nyuma kwenye mkondo wa maji mboga ipo naiona kila siku. wote tukasema acha masiala mboga gani iyo mwana akasema si kuna kenge pale watu wote tukachoka. ni kweli kwenye huo mkondo kulikua kuna bonge moja la kenge ambalo ukiliona ata kama ni kwa bahati mbaya likiwa limejisahau lilikua linapotea chapu kama upepo mwana baada ya kuona wote atusomeki alinyanyuka na kwenda zake. uko alikokwenda sijui ata alitumia mbinu gani ila ata aikuchukua mda sana tulimuona yule mwana akirudi akiwa kambeba yule kenge mkononi. wala akuongea na mtu alimuandaa yule kenge kisha akakata kata stek stek za kutosha na kuwasha moto kisha kubanika punde tu tukahanza kushuhudia mafuta mafuta kwa mbali kutoka kwenye nyama ya kenge. mwana akasonga ugali wa kutosha na kutamka kauli moja tu anaeitaji kula aje
 
Matunda gani hayo mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…