Je, umewahi kula mnyama ama wadudu gani Hadi ukajisemea nilikuwa wapi siku zote hizo? Nimekula wanyama wengi sana.

Kaka noma sanaaaaaa
 
Kaka noma sanaaaaaa
Hahahaaa hakika mkuu!
Haya mambo uyasikie tu kwa watu ila usiombe ku experience!
Siku madogo wamemnasa kobe mtoni wakaja nae mi nikawa nashangaa tu wao wananiambia bro hii mboga ya leo!
Shughuli kwenye kumvua lile jumba lake sasa na ni vp watamchinja, make awali nilikuwa nasikia msemo kwamba ukitaka kumchija kobe timing!
Jamaa walichemsha maji yalipotokota wakamdumbukiza mzima mzima walivyomvabua mle tayari akawa kafa na kutoa shingo nje halafu lile jumba wakagonga kiulaini tu likatoka.

Kimbembe kingine ni kwenye kumchuna mnyama Fungo.
Kule kwenye masab.uri kunatoa harufu hatari hatari! Wanachofanya ni kumziba na mti kisha wanachuna fresh tu yaani.
Nyama yake hapana chesea kabisa pungo kwa nchele ananoga balaa!
 
Fungo sijui ni mnyama gani yupo kama komba kama sikosei

Au ndio wale vicheche/ NGUCHIRO
 
Fungo sijui ni mnyama gani yupo kama komba kama sikosei

Au ndio wale vicheche/ NGUCHIRO
Fungo ni mnyama mkubwa kama mbwa ila ni mtata mbwa hawagusi pale.
Ana madoa doa na mara nyingi mawindo yake hufanya usiku.
Anakula matunda jamii ya ngobe(koloto), wadudu jamii ya kumbikumbi n.k
Ana tabia ya ajabu sana make kawaida yake haja kubwa hujisaidia sehemu moja tu!
Mathalani kaenda mawindoni mbagala ikatokea kabanwa na haja kubwa, anacho fanya ni kujaza majani matak.oni then anaendelea na kusaka msosi mpaka atakapo rudi sehemu yake maalum ndo anashusha kimba hata kama ni mbali let say tegeta huko!

Kwa tabia yake hii ya kubana inyaa hupelekea kutoa harufu kali muda wote kiasi kwamba mbwa akimsogelea karibu huvurugwa na kukarahishwa na ile harufu kiasi cha kutoka nduki au ampishe njia aendelee na misele yake.
 
Likwegese a.k.a KANU
 
😀😀😀
 
Kama wapi mkuu embu hoja Yako isindikizwe na picha mnato😀
Hahaha...

Kama umewahi kuona makao ya siafu, na matini hua na nyumba za aina hiyo mkuu...

Matini hupatikana kwa kutwanga ile nyumba na mchi...

Ukipata shimo unaweka majani ya mti(mala nyingi mzima) matini yanang'ata na hutolewa kwa njia hiyo...
 
Nyoka wote wana nyama safi sana
 
Hao fungo wanaonuka ndo wanaliwa ? Ulishawahi kula ?

Kisima
Nimekula vizuri tu.
Ilitokea siku moja narudi zangu misele usiku wa manane akajichanganya nikampiga tairi kwa pkpk akafa!
Kambini kwangu kulikuwa na makonde flani shabab ikabidi nimbebee kama maskhara, nilipomfikisha makonde hakulala akakesha anambanika.
Asubuhi yake nikaamka nae na vile nilikuwa na hang-over, nilimfakamia na ofcoz alikuwa mtamu sanaaa!
 
Nina stori kama tatu hivi za kula wanyama pori wa ajabu kwangu.
Nimekula nyama pori za wanyama wengi kuliko wanyama wafugwao.
Ila ambao bado nakumbuka nyama zao ni tembo, pimbi, Nungunungu na nguruwe pori
 
Fungo asee ananuka sio poa😹😹 ila fresh TU jamaa
 
Kobe wa majini anakunya funza kabisa mkuu mliwezaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…