Je umewahi kutumia sarafu hizi za kitanzania?

Je umewahi kutumia sarafu hizi za kitanzania?

Kuna siku niliokota shilingi 60 uwanja wa mpira. Nilijisikia kama mfalme wiki nzima.
Binafsi niliwahi kuokota shilingi hamsini, ilikuwa tunasafisha darasa. Nikawa nina hofu sana kumiliki ukwasi mkubwa kiasi kile hadi kufikia hatua ya kuwa rank moja kiuchumi na afisa elimu 😂😂😂.. ilibidi niwatonye wanangu wawili ili tukaponde
 
Enzi zile mtoto ukimiliki shilingi hamsini au sitini inabidi uifiche, kwa sababu ikijulikana una hela hiyo kitu cha kwanza watu watafikiri ni kwamba umeiba tu hiyo hela.

Mtoto mdogo huna kazi wala biashara utapata wapi shilingi hamsini au sitini?

Hiyo hela hata zawadi hupewi.
 
Liliitwa dala kwa sababu thamani yake ilikuwa sawa na US dollar moja.

Na hiyo ndiyo ilikuwa nauli ya kwanza ya "Daladala", nauli ilikuwa hiyo "dala" ndiyo maana mabasi yakaitwa "daladala".

Makondakta walikuwa wanatangaza nauli "dala dala" ndiyo jina la mabasi likapatikana.
Umenikumbusha tamthiliya ya miaka ya nyuma iliyoandikwa na Mbunda Msokile inaitwa usiku utakapokwisha ndani yake kulikuwa na nukuu inayohusu maswala ya madala yaani pesa, nukuu inasema.
"Gonza: Nini hasa shida yako.
Askari: kitu kidogo...
Gonza: Kama nini.
Askari: Madala kadhaa"
 
Hakika kila zama na kitabu chake, nimetumia shilingi tano shilingi kumi na shilingi ishirini.........hazikuwa pesa ndogo kipind hiko zlikuwa zeny thamani hasaa.
 
Niliwahi kuhonga demu wa utotoni/ujanani senti 5. Hela yenyewe niliiokota! Kweli muda umesonga . Shikamoo zinazidi kuongezeka kila siku!
 
Back
Top Bottom