Je, Umewahi Kuvunjia Kichwa cha Plug kwenye Cylinder Head?

Boeing 747

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2018
Posts
3,515
Reaction score
9,415
Leo tarehe 9/3/2020 nilikuwa nina ratiba ya kubadili Spark plugs kwenye kausafiri kangu..

Niliponunua nikarejea nyumbani, nikachukua vifaa vyangu nikaanza zoezi la kutoa plugs za zamani na kuweka mpya..

Nikaweka plug kwenye Cylinder namba 1, 2 ,3 na 4... Cylinder 1, 2 na 4 nilikaza kiasi ya 1/2 (nusu) ya mzunguko wa spana yangu ambacho ndicho kiwango kinachopendekezwa kwenye ukazaji wa spark plugs.

Wakati ninakaza plug ya cylinder namba 3, mawazo yalikuwa mbali, nikachanganya na stress za jana Simba tulivyofungwa, nikajikuta nimeikaza kama mtu anayekaza nati na tairi la scania....Kichwa cha plug kikakatika kikabaki kwenye Cylinder head...[emoji51][emoji51][emoji51]

Nilihisi homa kidogo, Nikawa nawaza namna ya kufungua cylinder head ili kutoa kile kichwa. Namshukuru Mungu nilipata wazo la kutumia kipande cha nondo nyembamba, pliers,pamoja na nyundo...nikafanikiwa kukitoa hicho kipande cha plug. Ilinichukua kama lisaa limoja hivi....Kipande cha nondo nilikigonga na nyundo kikawa chembamba nchani, nikakipenyeza pale kwe kichwa cha plug ndani ya cylinder, nikakigongea taratiiiibu kwa nyundo mpaka nikahisi kimekaza, nikatumia pliers kuzungusha hiyo nondo ili kugungua kupande kilichonasa....Nilifanikiwa kukitoa bika shida .

Mbinu niliyotumia usijaribu kama wewe si mtundu wa magari..
Je, kwa wale ambao wameshawahi kupata tatizo kama hili, mlitumia njia gani kutatua tatizo...?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vizuri sana jambo la kijasiri, kama ulifanya kitu tofauti ukituliza kichwa kuna uwezekano mkubwa ukafanya kwa ufasaha.
 
Sema na spark plug unazotumia nano hazina Ubora, kwa kawaida plug haikatikagi Kiivo, kuna quality issues hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa namna nilivyokaza lazima tu ikatike..
Sikujua ni shetani gani alipita nikawa kama vile nakaza natinza tairi..

Kuhusu ubora wa plug hizo ni NGK standard kabisa kwa Nissan...Kuna denso ni nzuri...

Na ubora wa plug si ugumu wa kile kichwa...ubora wa plug ni madini yaliyotumika example...copper, iridium au platinum...

Umbo la nje wanatumia metal za kawaida tu..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hii habari sitaki kuikumbuka iligharimu hela nyingi mpaka gari ikarudi kwenye ubora wake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka 2017, natoka msibani,nikafungua kizibo cha maji,nikaweka maji mengine,kumbe kile kizibo kimekaa pembeni,hakijakaza vizuri..

Nikaanza safari,kufika tinde,temperature iko juu,gari ikazima tu,kumbe nishachinja cylinder head tayari,ilinibidi ni overhaul engine nzima!!

Engine ya Klugger, cha moto mbona nilikiona,yaani nilitoboka sitasahau hii safari!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cylinder head ni kitu cha kuchunga kama mboni ya jicho...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…