Boeing 747
JF-Expert Member
- Mar 30, 2018
- 3,515
- 9,415
Leo tarehe 9/3/2020 nilikuwa nina ratiba ya kubadili Spark plugs kwenye kausafiri kangu..
Niliponunua nikarejea nyumbani, nikachukua vifaa vyangu nikaanza zoezi la kutoa plugs za zamani na kuweka mpya..
Nikaweka plug kwenye Cylinder namba 1, 2 ,3 na 4... Cylinder 1, 2 na 4 nilikaza kiasi ya 1/2 (nusu) ya mzunguko wa spana yangu ambacho ndicho kiwango kinachopendekezwa kwenye ukazaji wa spark plugs.
Wakati ninakaza plug ya cylinder namba 3, mawazo yalikuwa mbali, nikachanganya na stress za jana Simba tulivyofungwa, nikajikuta nimeikaza kama mtu anayekaza nati na tairi la scania....Kichwa cha plug kikakatika kikabaki kwenye Cylinder head...[emoji51][emoji51][emoji51]
Nilihisi homa kidogo, Nikawa nawaza namna ya kufungua cylinder head ili kutoa kile kichwa. Namshukuru Mungu nilipata wazo la kutumia kipande cha nondo nyembamba, pliers,pamoja na nyundo...nikafanikiwa kukitoa hicho kipande cha plug. Ilinichukua kama lisaa limoja hivi....Kipande cha nondo nilikigonga na nyundo kikawa chembamba nchani, nikakipenyeza pale kwe kichwa cha plug ndani ya cylinder, nikakigongea taratiiiibu kwa nyundo mpaka nikahisi kimekaza, nikatumia pliers kuzungusha hiyo nondo ili kugungua kupande kilichonasa....Nilifanikiwa kukitoa bika shida .
Mbinu niliyotumia usijaribu kama wewe si mtundu wa magari..
Je, kwa wale ambao wameshawahi kupata tatizo kama hili, mlitumia njia gani kutatua tatizo...?
Sent using Jamii Forums mobile app