Je, una imani na jeshi la polisi kuomba escort unapokuwa na fedha au madini?

Daah kesi ya Mtwara bado ipo mbichi harafu tena uwatumie Wauaji kupeleka dhahabu kupimwa ni bora ukakutane na majambazi Road kuliko ukasafiri nao huku wakiwa na uhakika wa Mzigo waliobeba na ukienda kutoa taarifa kesi unapewa nyepesi mno maana mashahidi ni wenyewe.

Mtuhumiwa aliiba dhahabu na kutaka kuwatoroka Polisi kwenye kizuizi na siraha itawekwa ubaoni kama kidhibiti ndugu watagomea kuchukua maiti mpaka ipimwe ila baadae watachukua tuu na ndio mwisho wa Movie yenyewe.
 
Mawazo/ushauri wake ni mzuri tunauheshimu wote lakini unakuja wakati jeshi la polisi wanazo damu za watu mikononi mwao, umekuja wakati sio sahihi kwa jeshi la polisi.

Fikilia raia kufia mikononi mwao

Yule kijana mpambanaji wa Mtwara ndoto zake zikifikishwa mwisho na hao jamaa japo haijadhibitishwa lakini kutuhumiwa tu hiyo ni kupoteza imani,

Juzi tu hapa mlinzi kala chuma hapo kwa Chalamila.

Polisi hao hao mara wanakamatwa wakisindikiza madawa ya kulevya

Raia anakamatwa na polisi anafikishwa kabisa kituoni mara mnaambiwa kafa sababu et kajinyonga kwa dekio!! aisee kwa selo zetu hizi za bongo inawezekanaje wakati selo zimejaa watuhumiwa!!

Polisi anakuja kukamata mtu kama anakamata jambazi wakati ni raia tena mtuhumiwa tu.


Acha nife nazo lakini sio kwenda kukitafuta kifo kibaya
 
Wizi ni tabia ya mtu na sio tabia ya Jeshi.
 
sasa wakiomba escort gharama ya kulipia hiyo escort itatoka wapi? Kwanza haitakiwi mtu mwingine ajue nina kiasi gani cha pesa nasafirisha. Je hao polisi wakiingiwa na tamaa usalama wangu na pesa zangu utakuaje? Labda niandae bajeti ya kulipia hiyo escort na niridhike nitakuwa salama mimi na fedha zangu
 
Kuna kaukwel ndan yake
 
Point
 
Hata BOT escort wanalipia. Hata serekali yenyewe kutoka benki kwenda halmashauri tu, ndani ya KM 01 tunalipa escort kwa polisi ili tuwe salama, na hatujawahi pata shida kwa uwepo wao, lakini watu kila siku wanalizwa na pesa zao hapa hapa mtaani wakitoka kuchukua pesa benki.
 
Jeshi la polisi lina kazi kubwa sana kurudisha imani ya wananchi. Naona hata hawajishughulishi na hilo hata yakitokea matukukio mabaya yanayo wahusu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…