Je, una imani na Jeshi la Polisi?

Je, una imani na Jeshi la Polisi?

Una imani na utendaji wa Jeshi la polisi?

  • Total voters
    111
Nahisi wananchi walio wengi wamepoteza imani kwa jeshi lao la polisi,ni bora taratibu zikafuatwa na jeshi hili likavunjwa na kuundwa upya,hata yale maelezo wanayoyatoa Polisi hawa baada ya tukio na wao wakiwa ndio wasemaji wakuu katika kutoa maelezo yawe ya wizi,ya ubakaji,ya mauaji ya uchaguzi ,kwa kweli wananchi walio wengi wanawabeza na kurusha madongo.

Nahizi sio vizuri kwa jeshi hili kuwepo kama lilivyo linahitaji ukarabati wa uweledi sana,maana kwa masikizi ya wananchi hili jeshi ni mzigo usio na faida,hata wakuu wa polisi kama wataweza kusema ukweli bila ya shaka yeyote watakuwa na la kusema juu ya imani ya wananchi dhidi yao.tulimsikia mmoja juzi akitoa maelezo mengi,,huku akionesha kusikitika kuwa huko mitandaoni kunasemwa hili na lile,wananchi mitaani wanasema hivi na hvyo,mradi alisikitika sana kwa kuona wananchi hawana imani na yale wanayoyatenda.
Kipindi limevunjwa na wakati wa mchakato wa kuliunda tena nani atakuwa anasimamia ulinzi na usalama? Mawazo mfu haya. Pendekeza mageuzi na maboresho unapoona pana kasoro ila kulivunja haiwezekani
 
Livunjwe tu ili tuone wananchi watavyofilimbwa.
 
Nahisi wananchi walio wengi wamepoteza imani kwa jeshi lao la polisi,ni bora taratibu zikafuatwa na jeshi hili likavunjwa na kuundwa upya, hata yale maelezo wanayoyatoa Polisi hawa baada ya tukio na wao wakiwa ndio wasemaji wakuu katika kutoa maelezo yawe ya wizi,ya ubakaji,ya mauaji ya uchaguzi ,kwa kweli wananchi walio wengi wanawabeza na kurusha madongo.

Nahizi sio vizuri kwa jeshi hili kuwepo kama lilivyo linahitaji ukarabati wa uweledi sana,maana kwa masikizi ya wananchi hili jeshi ni mzigo usio na faida,hata wakuu wa polisi kama wataweza kusema ukweli bila ya shaka yeyote watakuwa na la kusema juu ya imani ya wananchi dhidi yao.tulimsikia mmoja juzi akitoa maelezo mengi, huku akionesha kusikitika kuwa huko mitandaoni kunasemwa hili na lile,wananchi mitaani wanasema hivi na hvyo,mradi alisikitika sana kwa kuona wananchi hawana imani na yale wanayoyatenda.

alafu utalinda wewe nchi?
 
kwa wananchi imani imepotea kwa watawala imani imekua
 
Ni rahisi kuandika mkiwa nyuma ya keyboard,ila ulishawahi kuimagine hata masaa 3 tu bila jeshi la police?,yaani mateja,wezi,majambazi na wahalifu wote wajue kwa mda huu hakuna bank police,hata wakifanya uhalifu wowote hawataguswa,wabakaji wote wajue wanaweza kula dem yoyote kwa mda huu bila kuguswa,bado hatujawagusa watu wenye visasi vyao.Labda kama haujaandika fanya simple observation uone ni kesi ngapi zinaripotiwa kwa siku kwa kituo kimoja tu kama cha buguruni.
 
Kipindi limevunjwa na wakati wa mchakato wa kuliunda tena nani atakuwa anasimamia ulinzi na usalama? Mawazo mfu haya. Pendekeza mageuzi na maboresho unapoona pana kasoro ila kulivunja haiwezekani
Kwani hivi sasa nani anasimamia! Si wanapiga deal tu na kabambikia watu kesi.
 
Inaonekana ufahamu umepungua na kuwa finyu ,mtu anauliza eti jeshi la polisi likivunjwa nani atalinda nchi,hivi kazi ya polisi ni kulinda nchi ? Wengine eti nina duku duku la hamza ,wengine eti tunaandika tukiwa nyuma ya kiibodi,labda mwenzetu kibodi unaikalia. sawa iwavyo vyovyote vile.

kama ni msikilizaji wa vipindi rushwa ,ukiangali gearhabib utaona watu wanavyoilalamikia polisi open kabisa,wakati wa Magu wananchi walifika kusema Magufuli ingilia kama unatusikia maana polisi hakuna faida na sasa utasikia mama kama unatusikia hivi vilio vyetu kwani wazalilishaji wakifika polisi jioni asubuhi wanakuwepo mitaani na majilabu..hafungwi mtu ni masikitiko kabisa,ukivuka bahari nao wana tv za mitandaoni wazalilishaji wanakamatwa na ushahidi juu wanapelekwa polisi siku ya pili unawakuta wazalilishaji mitaani,kwenye TV wanalalamika polisi wameshindwa kazi au wanapokea rushwa --Mbona vipindi vingi tu,polisi wanalaumiwa kwenye mambo ambayo yana vielelezo kabisa.

Tukio la Hamza ndio usiseme japo Mkuu amejaribu kulinganisha na ya polisi kukutwa na maafa wakati wa kazi zao na wananchi hawakuwasifu au kuwapa hongera.

Hamza alianza kuzungumziwa na vyombo vingi vya habari na watu wengi kuhojiwa kabla ya polisi kutoa tamko au taarifa rasmi.

Umilikaji wa madini ambao polisi wameukana inaweza kuwa watu hawajagawana urisi kwa hio huwezi kuona kama Hamza anamiliki machimbo,kutoka Chunya waliohojiwa wakimjua Hamza kama msimamizi au mmiliki wa machimbo ya baba yake na wananchi wa eneo waliohijiwa walimpa sifa kedekede hadi kuwajengea ofisi ya Chama,sio jambo dogo hilo na sidhani kama mwenye Imani ya kidini anaweza kujenga ofisi ya CCM tena huko kwa vigagula na kusaidia watu wa aina zote bila ya kubagua.

Kwa upande wangu leo Humphrey Polepole akipigwa risasi na polisi unafikiri nitashugulika sana nitaguna tu,wenziwe wameshamuona mbaya anawaharibia.CCM kuonana wabaya ni jambo jepesi sana sana maana wote ni wezi wa kura sasa wezi kuzikana ni jambo la kusidiana mbinu tu,

Wanazinguana ,unalikuta jeshii la polisi lipo katikati limezungukwa na CCM ,limatumika katika mikakati mbalimbali ya CCM japo wenyewe wanakataa lakini mwenye macho haaambiwi tazama tunayaona hapa Pemba. Polisi wanakimbia na masanduku ya kura,imani yetu kwao itatoka wapi ? Wanaiba magunia ya karafuu usiku nyumbani kwa mtu,imani hio ni imani gani ya kuendelea kuwapenda na kuwapa sapoti.

Kila siku tunawasikia polisi wakinadi ,bila ya wananchi hatuwezi kufanikiwa ni lazima tushirikiane watupe info na mambo ya kiintelijensia ili kuwadhibiti wahalifu na kuweka na kutunza amani na utulivu, Hivi huwa najiuliza wanamwambia mwananchi gani ? Huyu huyu wanamvamia usiku na kumuibia karafuu zake ?

Hivi mnataka kusema hakuna nchi imewahi kulivunja jeshi la polisi ?
 
Kuvunjwa si sawa hata kidogo inabidi mambo madogo tu yabadilishwe ili imani irejee
 
1630744157782.png
Huyu unafikiri amezeeka au ameondolewa ?
 
Back
Top Bottom