Je, una imani na Jeshi la Polisi?

Una imani na utendaji wa Jeshi la polisi?


  • Total voters
    111

waliomuua prof.jwani mwakusa????? Mpaka leo uchunguzi unaendelea!!
 

Samaki mmoja akioza.......... Serikali inabidi iacghe kutumia vyombo vyakje kisiasa!!

Watu wanajisahau kupita kiasi, ukiwaona kwenye press na mavazi yao utadhani waungwana!!! Kidooogo naweza kuwa na imani na JWTZ! Wengineo ni mzoga ya wansiasa!!!

Mfumo mfumo mfumo....
 
Nyie ambao mko kwenye mji mikubwa kama dar dodoma arusha mwanza mnalalamika kuhusu polisi embu nendeni huko vijijini ndo muone mambo polisi wanayofanya. Jeshi limechafuka na hata cdm au chama kingine kikitawala nchi itachukua karibia miaka 10 kuweza kunadilisha watu na mfumo wa rushwa na unyanyasaji unaofanywa na polisi sasa hivi.
 
Nkicomment ntakula ban
ngoja nipite tuu...
 
Nkicomment ntakula ban
ngoja nipite tuu...
 

Ndugu
Yaani ulichosema hapa ndicho kabisa kilichopo kwa jeshi letu hili la kipuuzi!!! Yaani ni aibu tupu!!
 
Yapo mengi sana yanayowahusu Polisi katika levels mbalimbali. Tuhuma dhidi yao zinaongezeka sana. Traffic Police usisieme huko barabarani, wanachukua rushwa kama waziwazi siku hizi baada ya kumnyofoa Jerry Muro. Kwenye vituo vya Polisi ni jehanamu, mtuhumiwa hana tofauti na mhukumiwa. Polisi wadogo wanashindwa tu kugoma, wanatamani na wao wangekuwa madaktari!!!! ili wapate nafasi ya kugoma! Sijui tunaelekea wapi!
 
Usiku wa kuamkia jumapili yalivunjwa maduka 3 mtaa wa rwagasore mwanza,ilipotimu asubuhi wenye duka wakaenda kituo cha polisi pamba wakatoa taarifa wakaambiwa na polisi waende wakamshike mlinzi wampeleke kituoni na wahakikishe wanatafuta mlinzi mwingine,ni nani atakuwa na imani na polisi?
 

Sasa hapa mhusika au mhanga atajuaje kama Kova au Mwema atampangia hao 'wachapa kazi hodari' na siyo hao waovu kwenye hiyo timu ya uchunguzi? Piga teke chungu cha mboga kama kafia panya, uanze upya kupika au ulale hata njaa!
 
Ili Nchimbi afahamu hilo kuwa hawa jama hawaaminiki ngoja asubili hapo 2015 mmagamba wakiwa wapinzani
 
Mimi sielewi Nchimbi anatumiaje usomi anaodai anao kuchambua issue. Hawa viongozi wa chadema wametoa tuhuma nzito pia wakatoa historia ya tuhuma kama hizo walizowahi kuzifikisha polisi hadi leo hakuna taarifa za uchunguzi juu ya tuhuma hizo, je bado Nchimbi anataka waendelee kuamini chombo ambacho hata victims of criminality hawakujulishwa matokeo ya uchunguzi wa polisi? Lakini pia hakuna sheria ya polisi au nchi inayolipa jeshi la polisi kumlazimisha mtu asiyetaka kutoa malalamiko? Mimi km nimeibiwa kuku au nimepigwa nikaamua sitaki kutoa taarifa polisi siwezi kuja kushitakiwa au kulazimishwa na polisi kutoa maelezo eti tu wamesikia nimelalamika. Kama serikali inataka kujisafisha waunde tume huru au chombo huru kuchunguza tuhuma za aina hizi ama basi serikali itoe taarifa za uchunguzi wa tuhuma ambazo zilishawahi kuripotiwa polisi siku za nyuma km Dr. Slaa kuwekewa surveillance appliance kwenye chumba cha hotelini kwake, etc. Kwa nini serikali huwa inakimbilia kujisafisha eti haihusiki na tuhuma hizo hata kabla ya uchunguzi kuanza?
 
Kweli umempa maelezo ya kina Mh. Nchimbi kuhusu wananchi kukosa imani na chombo chao. Aidha Mh. Nchimbi anapaswa kuelewa kuwa sio dhambi mtu kukosa imani na chombo chochote kile ndio maana watu huweza kubadili hata dini zao pale wanapokosa imani na dini waliyokuwa wakiiamini awali.
Mh. Nchimbi kwa nyongeza tu, viashiria vya wananchi kukosa imani na Jeshi la Polosi ni pamoja na ujasiri ambao tumeuona kutokana na vitendo vya wananchi kuvamia na kuharibu au kuvichoma moto vituo vya Polisi katika miaka ya hivi karibuni katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu. Hii ni dalili kuwa wananchi hawana imani na chombo chao.
Mh. Nchimbi nadhani utakumbuka vema kuwa wakati ule ukiwa unaishi "laini" baba zako walifanya kazi kwa moyo wa upendo katika mazingira magumu sana bila kuhasimiana na wananchi. Elewa endapo utaendelea kuwalinda Polisi waovu imani ya wananchi itatoweka kabisa na nchi inaweza kugeuka Syria ya Africa. Mungu inusuru Tanzania, mtumumie Mtoto wa "Laini" kufanya mabadiliko ya kimfumo ili jeshi la Polisi lirudishe heshima yake kwa wananchi.
 
Mimi mwenyewe mlala hoi naunga mkono hoja. Upelelezi hapo wa nini? Ikigundulika ni kweli upo mpango wa kuwauwa na watuhumiwa kutajwa watachukuliwa hatu gani! Mheshimiwa mmechemsha sana na serikali yenu dhaifu. Mfano
1.Waliotajwa na Mheshimiwa Mwakyembe ktk njama za kutaka kumuua wametiwa mbaroni lini wakati wanajulikana? Huyo afande Sabasitasaba humjui wakati ni mwajiriwa wako?
2.Aliyetajwa na Dr.Ulimboka arudishe Pochi na Cm yake humjui na umemuajiri kwenye Wizara yako? Hadi hapo hauoni wote ninyi ni Dhaifu.
3.Wale wauza madini waliopelekwa na kuuawa kwenye ule msitu wenu wa Serikali Dhaifu,nani waliopandishwa kizimbani kama sio waajriwa wa wizara yako?
Yaani kama mimi siku nikuta polisi kagongwa na gari na mimi namkanyaga hata na miguu
Kikubwa hatuna imani ng'o na ninyi mafedhuli. NAUNGA MKONO HOJA.
 
Hebu nchimbi,uuwe unafanya mishtukizo kama mwakyembe,hawa POLISI hujui dhambi zao au UNAZUGA????
JANA MWENZIO KAWASHUSHUA SUMATRA HAPO BUS TERMINAL
Yeye mwenyewe Nchimbi amekulia kwenye mabaracks ya polisi, anafahamu sana matatizo ya mapolisi ikiwa ni pamoja na baba yake. Hapa alikuwa anajishaua tu kama ilivyo kawaida ya wana CCM wote.
 


Ulicho kizungumza kuhusu raia kupoteza imani na chombo hiki cha dola ni sahihi kabisa,mambo mengi yanadhalilisha jeshi hili kwa kuchangiwa na watendaji wake na mdororo wa serikali husika kushindwa kuyafanyia kazi malalamiko ya wananchi dhidi ya tuhuma zinazo lilenga jeshi letu la Polisi.

Mathalani,mimi binafsi niliwahi kuibiwa na mtu niliyemtuhumu alikamatwa na kuachiwa bila kuhojiwa kwa kuwa tu baba yake alitoa rushwa.Kitendo hicho kilisababisha wananchi kumkata raia huyu kupitia serikali ya mtaa kwa kumtaka ahame mtaani hapo lazima wananchi watajichukulia sheria mkononi.

Jana tumeshuhudia askari polisi ana mfukuzia raia na kutaka kumbambikia kesi ya mauaji,lakini kutokana na msimamo wa raia na kutaka kujua hatima ya mwananchi huyo ilibidi askari wlae wamuachie.Wakati mwingine utakuta mkuu wa upelelezi wa wilaya ana shirikiana na majambazi kiasi cha kuvujisha siri na kujenga uhasama kati ya raia wema na wahalifu.Tuhuma kuhusu jeshi hili ni nyingi kiasi ambacho ukimya unaofanywa na serikali ipo siku utapelekea kuvunjika kwa amani.Askari hawa tunaishi nao majumbani mwetu lakini kwa kuwa tu hawana akili wanakubali kupandikiziwa chuki dhidi ya raia.
 

Mkuu hii ya kumuita Dr Ulimboka Hitler kama ina ushahidi ni kesi nzuri kabisa mahakamani, ambayo Manyanya anaweza kujutia kinywa chake.

Ukitaka kujua hali ya uaminifu wa polisi kwa umma, nenda pale Redet walifanya utafiti matokeo yako wazi kabisa, lakini ripoti imefunikwa tu.
 
Reactions: FJM

Nilijua ipo na kama nakumbuka vizuri polisi na mahakama walikuwa wanaongoza, watu hawana imani na hivyo vyombo.
 
6. Waliowaua wafanyabiasha madini wa ulanga huko Mabwepande ni akina nani? 7. Waliopanga mpango wa kumwekea madawa ya kulevya mtoto Mzee Mengi kwenye mizgo yake pale airport wakati anataka kusafiri to India ni akina nani hao?
 
imekua ni jambo la kawaida kwa utawala huu wa hawamu ya nne kwa jeshi la polisi kujiamulia kuua raia badala ya kuwalinda kama wajibu wao, lakini kinyume chake wanajenga uhasama na chuki katika jamii.
hali hii inanipa mashaka kwa jeshi hili kutumia risasi za moto na mabomu kutuliza ghasia zinazozuka kuna agenda gani ya siri au tuamini kuwa wameagizwa?
jeshi hili la polisi sio siri sasa limepoteza imani kwa walio wengi kufuatia vitendo hivi vya kikatili na unyama huku wachache wakidiliki kutetea hali hiyo kwa madai kuwa linatelekeza wajibu wake, ni wajibu gani huo wa kuua raia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…